Pamoja na kuungana, Trump awagaraza wapinzani wake

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,842
4,794
160427025551_sp_trump_640x360_afp_nocredit.jpg


Donald Trump ameshinda mchujo wa kuteua mgombea urais wa chama cha Republican katika majimbo matano ya Marekani yaliyopiga kura Jumanne.

Mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton ameshinda majimbo manne kati ya matano yaliyoshiriki mchujo.

Baada ya matokeo kubainika, Bw Trump alijitangaza kuwa “mgombea mteule” wa Republican.

Ushindi wake Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania na Rhode Island unamfanya kukaribia sana kutimiza idadi ya wajumbe inayohitajika kumhakikishia ushindi kabla ya kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha mgombea Julai.

Upande wa Democratic, Bi Clinton amenyimwa ushindi kamili na Bernie Sanders ambaye ameshinda katika jimbo la Rhode Island.

Bw Sanders ameaoa kuendelea na mchujo.

160427012320_hillary_clinton_624x351_reuters_nocredit.jpg


Bi Clinton amesema kampeni yake ina "malengo jasiri"
Akiongea katika ukumbi wa mikutano wa Philadelphia baada ya kushinda majimbo hayo manne, Bi Clinton amesema kampeni yake inaweka “malengo jasiri na ya kupiga hatua mbele” katika kuimarisha maisha ya watu Marekani.

“Sisi tunaamini katika wema wa watu wetu na ukuu wa taifa letu,” alisema.

Naye Bw. Trump aliwaambia wafuasi wake New York kwamba hatabadilisha sera zake iwapo atachaguliwa kuwa rais.

"Sibadiliki,” alisema. “Mnafahamu kwamba nilisomea shule bora zaidi. Mimi ni mtu mwerevu sana. Nitaiwakilisha nchi hii kwa heshima na vyema sana.

"Lakini sitaki kubadilisha sifa zangu binafsi. Mnajua, ndizo zilizonifikisha hapa.”

Wapinzani wake, Ted Cruz na John Kasich, tayari wameanza kuangazia majimbo yajayo, wakiungana kusaidiana kushinda majimbo ya Indiana, Oregon na New Mexico.

Bw. Trump ameshutumu ushirika wao akisema ni ishara ya kukata tamaa.

Chanzo: BBC Swahili
 
ISIS na waislam wanaojilipua ndio watasababisha Trump ashinde Urais, kwa kampeni yake ya kuzuia waislam magaidi kuingia Marekani, kutokana na mauaji ya ovyo ovyo yanayofanywa ulaya na marekani, yanawakera wamarekani wengi.
 
Back
Top Bottom