Pamoja na kuijenga CHADEMA kwa mikono yake, Ndesamburo hakupewa heshima kama Lowassa na Sumaye

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Marehemu Mzee Ndesamburo kama almaarufu kama Ndesa Pesa, ni watu waliojiondoa CCM mara baada ya vyama vingi kuanza rasmi nchini Tanzania, huku akiwa muasisi na mwenyekii wa kwanza wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro. Alikijenga chama huku Sumaye akiwa waziri mkuu alitamka kejeli akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro miaka ya mwanzoni 2000 kuwa ''ukitaka biashara yako ifanikiwe jiunge na CCM''.

Ndesamburo alitumia rasilimali zake na ushawishi kuijenga Chadema katika kipindi chote hicho bil kuchoka, Huku akiwa Mwenyekiti wa Mkoa alikuwa pia mjumbe wa Baraza kuu la chama Taifa hivyo kimadaraka ndani ya chama ni 'mzito' kuliko akina Lowassa na Sumaye ambao kimsingi walikuja kugombea uraisi na si kuijenga Chadema.

Haikuwahi kutokea katika uhai wake Mzee ndesamburo kukaa meza kuu lakini ghafla wajumbe wapya wawili wasio viongozi wa sekretariet wanaketi meza kuu huku Mzee Ndesamburo akiketi viti vya nyuma kabisa.

18740623_1402265173199833_869632989688142884_n.jpg

Hayati Mzee Ndesa katika mkutano wa Baraza kuu Dodoma hivi karibuni.

Upumzike kwa amani Mzee wangu Ndesamburo, Leo kila mtu anataka kupata sifa na umaarufu kupitia msiba wako wakati walikutenga kipindi cha uhai wako.

APEPE
 
Mkoa alikuwa pia mjumbe wa Baraza kuu la chama Taifa hivyo kimadaraka ndani ya chama ni 'mzito' kuliko akina Lowassa na Sumaye ambao kimsingi walikuja kugombea uraisi na si kuijenga Chadema.
hao wametoa fedha yao kununua chama, chama ni chao sasa, RIP P K N
 
Hivi pesa alizolipa Lowasa kuingia kugombea urais zilifanyiwa nini? Au wenye chama waligawana?
 
Wakudadavua,

Trust me, I am serious!!! Aliyekupa hii kazi kwa kweli hana huruma kabisa na wewe!!! Yaani kabisa kabisa na wewe ukakubali kuwa kwenye hicho kitengo ambacho ukilala CHADEMA, ukiamka CHADEMA!!! Mbona hao jamaa hawana huruma namna hii?

Umewazidi hata wakongwe kama akina Rejao!!! Sijui kapotelea wapi!!! Lizaboni kimtindo lazima atakuwa anaku-mind manake unataka kumpokonya crown yake!!
 
Marehemu Mzee Ndesamburo kama almaarufu kama Ndesa Pesa, ni watu waliojiondoa CCM mara baada ya vyama vingi kuanza rasmi nchini Tanzania, huku akiwa muasisi na mwenyekii wa kwanza wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro. Alikijenga chama huku Sumaye akiwa waziri mkuu alitamka kejeli akiwa katika ziara mkoani Kilimanjaro miaka ya mwanzoni 2000 kuwa ''ukitaka biashara yako ifanikiwe jiunge na CCM''.

Ndesamburo alitumia rasilimali zake na ushawishi kuijenga Chadema katika kipindi chote hicho bil kuchoka, Huku akiwa Mwenyekiti wa Mkoa alikuwa pia mjumbe wa Baraza kuu la chama Taifa hivyo kimadaraka ndani ya chama ni 'mzito' kuliko akina Lowassa na Sumaye ambao kimsingi walikuja kugombea uraisi na si kuijenga Chadema.

Haikuwahi kutokea katika uhai wake Mzee ndesamburo kukaa meza kuu lakini ghafla wajumbe wapya wawili wasio viongozi wa sekretariet wanaketi meza kuu huku Mzee Ndesamburo akiketi viti vya nyuma kabisa.

18740623_1402265173199833_869632989688142884_n.jpg

Hayati Mzee Ndesa katika mkutano wa Baraza kuu Dodoma hivi karibuni.

Upumzike kwa amani Mzee wangu Ndesamburo, Leo kila mtu anataka kupata sifa na umaarufu kupitia msiba wako wakati walikutenga kipindi cha uhai wako.

APEPE
Wewe mchonganishi. Acha biashara hiyo mara moja.
 
Halafu kwenye msiba utawasikia alikuwa ni kamanda!!

Ndesa amewasaidia Chopa kina Nassari hadi wakashinda ubunge lakini kama unavyosema hajawahi kupewa heshima kama aliyopewa lowassa...Mbowe alidiriki kubadilisha salamu ya Chama kutoka peoploooz power hadi mabadilikool lowassa...
 
Kungekuwa kuna ranking za dunia kwa nchi zinazo ongoza kwa majungu , fitna na ramli chonganishi
basi Tanzania ingeshika nafasi 3 bora . Maana sio kwa kupika na kupakua habari feki feki kama hizi.
Sijaona ufeki wa habari hapa...naona facts tupu...
Lowassa hukaa meza kuu kama nani?

Ndesamburo hajajenga chama hasa maeneo ya kaskazini kwa fedha zake za mfukoni?
 
Hukaa meza kuu kama mmiliki wa CHADEMA kwa sasa, mkuu ama umesahau kuwa kila zama zina
historia na watunzi wake..?
 
Back
Top Bottom