Pamoja na chuki zao lakini wameshindwa kuyaacha mawazo ya Hayati Magufuli

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa??

*Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.
*
Muda utaongea .
 
unaonaje ukaenda pale Chato alipozikwa kuna nafasi pembeni kazikwe nawe pale kulinda legacy ya huyo Magufuli.

Nakukumbusha tu kwamba kesho bwanako Jambazi Sabaya atapandishwa kizimbani pale Moshi,kisha atasafirishwa chini ya Ulinzi mkali kupelekwa Arusha kusubiria Hukumu yake ya tarehe 10 ambayo iwe jua iwe mvua lazima agongwe miaka 30 Jela,tukutane Mahakamani tarehe 10
 
Nijuavyo hiyo miradi inaendelea japo kwa spidi ndogo, punguza pressure.
 
..Ujenzi wa mji mkuu Dodoma ni ufujaji wa fedha za umma.

..Manunuzi ya ndege ni makosa, kwani Atcl inatutia hasara kila mwaka.
 
Ila duniani kuna baadhi ya medula oblangata ni ishu asee.

Hivi kwanini mnajinyima raha kiasi hiki? Unapambana na vivuli hujionei huruma? Unakaa roho inakuuma kabisa eti watu wanapambana na legacy, Sikia dogo legacy hata siku moja huwa haipiganiwi huwa inajipigania yenyewe! Acha kujipa pressure bure, amka fanya kazi maisha yanaenda kasi sana.
 
Back
Top Bottom