Pamechimbika Ubungo

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,585
Reaction score
11,260
Mida hii maeneo ya Ubungo Polisi wameamua kusheherekea sikukuu ya wajinga kwa kufukuza Machinga wote. Haikuweza kufahamika maramoja nikosa gani wasakatonge Hawa walilifanya lakini wameonekana Polisi hawa wakiwaswaga kama mbuzi wavujajasho hawa huku wakipora mbao na mabati nakupakia katika gari. Sura ya hapa niyakitumwa wananchi wamezunguka wakiwa hawana comment. Vijana wanakimbia na mizigo mizito vichwani huku wakielekezewa mitutu ya bunduki.

Eneo la darajani mamantilie wamekaa porini wakipika vyakula vyao. Gari la FFU lenye askari limeonekana mlimani likienda kuongeza nguvu.vilio vya uchungu vinasikika pia. Sijui Mnyika yuko wapi asaidie wananchi Hawa wasio na dhambi.
 
Si wako busy na kutafuta pesa kuliko kushuglika na mambo ya siasa wacha wakome polis ccm wambie wajaribu Mwanza waone jiji litakavyochafuka. Mnyika pekee hatoshi cha kufanya ni kuunganisha nguvu ya umma tuu kama Mwanza. Wacha waswagwe kama vipunu ili akili iingie. Police kimbisa hao mpaka akili iingie vichwani waache uchiro uchiro. Teh teh teh!.
 

mnyika ndio nani huyo aliye shindwa kumaliza shule
 
ndio maana watu wakisikia polisi kauliwa na majambazi au kagongwa WANAFURAHI, utakuta hao polisi hao wanaowafukuza kuna ndugu zao hapohapo.
 
ifike mahali walala hoi wawe na maamuzi yao binafsi, ikiwa ni pamoja na kuwaswaga policcm mpaka kituoni, kama wanavyofanya waarabu katika maandamano yao kwaniwako tayari hata kuwapiga polic wenye mitutu kwa mawe, ila sisis ni wapole sana
 
Kumbe wanasherehekea fools day! Wale na pilau za mamantilie
 
ifike mahali walala hoi wawe na maamuzi yao binafsi, ikiwa ni pamoja na kuwaswaga policcm mpaka kituoni, kama wanavyofanya waarabu katika maandamano yao kwaniwako tayari hata kuwapiga polic wenye mitutu kwa mawe, ila sisis ni wapole sana

nikweli hapa RAIA wapo wengi ila wamezunguka wanatazama tu kunagari la policcm linakuja na mbwa hapa
 
Ninapata hofu kuitambua taswira ya nchi hii kama wapinzani wakichukua nchi watawaacha machinga mjini. Mambo mengine si ya kutetea. Fuateni taratibu. Mbona nchi za wenzetu pia yapo?? Au ndo sie kujifanya tunaresist kila kitu only for the sake of being seen as mpinzani. Machinga wana maeneo yao. Waende huko ili tuwaone hao polisi watakaowafata huko
 
mnyika ndio nani huyo aliye shindwa kumaliza shule

Elimu ya chuo haiishi mkuu.ndio maana hata wewe unatamani kujiendeleza.kama unadhani mnyika elimu yake ni ndogo tuwakutanishe wewe na mnyika kwenye mdhalo wa wazi tukupime wewe mwenye hiyo elimu na mnyika ambaye hakumaliza shule tuone mziki wake.

Acheni kutumika bhana mimi nimemfahamu mnyika bungeni kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja bila shaka unamuonea wivu tu kwa kuwa ndiye mbunge anayeongoza bungeni kwa kujenga hoja mpaka sasa.hongera mnyika
 
mnyika ndio nani huyo aliye shindwa kumaliza shule

pengine bora zaidi mnyika sababu ni mbunge wa jamhuri ya tanzania,taizo laja kwako msomi unafua boxer za nape jion unalipoti lumumba bku7.
 
Anza kusahau jina lake kabla ya 2015.
 
Anza kusahau jina lake kabla ya 2015.

Nimeamini mnyika kiboko.mtamwaga pesa nyingi sana tutakula mwisho wa siku wanao tetea maoni ya wananchi wataibuka kidedea wewe endelea kujiamini na jeshi lakini utanikumbuka humo ndani ya jeshi kuna siri hujui
 

Mwanangu mwanza sehem gani?nipo mwanza mwanangu Kilimahewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…