MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Serikali ya Rais Magufuli imetoa rai kwa wananchi watakapowaona raia wa kigeni wanaowatilia shaka kuwa wanaishi kinyume cha sheria, kutoa taarifa mara moja katika idara ya uhamiaji kwa kupiga simu namba 0754-026281 na 0715-026281.
Serikari imetangaza kuanza kwa oparesheni kubwa ya kuwasaka wahamiaji haramu wanaoendesha shughuli zao nchini kinyume cha sheria.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji (RIO), John Msumule, alisema oparesheni hiyo iliyoanza jana, inalenga kukamata wahamiaji wanaofanya kazi kwenye kampuni, shule, serikali, taasisi za dini na nyumbani.
“Hatuwezi kukubali wageni kufanya kazi ambazo tayari Watanzania wana uwezo wa kuzifanya. Oparesheni hii itakwenda mkoa mzima na kuwakumba wale wote ambao wanaishi nchini bila vibali vya kufanyakazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya,”Alisema
Aidha, serikali imetangaza kufuta vibali vyote vya muda vya wageni kuishi nchini, baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu mkubwa. Oparesheni hiyo itawahusu wageni wanaofanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, alisema oparesheni hiyo inafanyika kutokana na kuwepo kwa wageni wengi, ambao wanaishi nchini na kuendesha shughuli ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania.
Alisema hali hiyo inaathiri fursa za ajira kwa Watanzania, hasa wenye taaluma na ujuzi wa kuendesha biashara na kazi hizo.
“Pia oparesheni hiyo itawakumba wafanyakazi ambao wameajiriwa kama viongozi katika taasisi na mashirika kinyume cha sheria na ambao wamekuwa wakitumia vyeo vyao kuwanyanyasa wafanyakazi wazalendo kwa kuwadhalilisha, hivyo kukiuka tararibu na sheria,”alisema.
Masauni alifafanua kuwa oparesheni hiyo itakuwa kubwa katika kuwasaka na kuwakamata na kisha kuwafi kisha kortini wahusika wote na kuwarudisha katika nchi zao. ”Wapo wafanyabishara na wafanyakazi wa kigeni ambao wanafanya kazi ambazo sio zile walizoomba kufanya.
Hawafuati sheria na taratibu za nchi za uwekezaji. Tutawakamata na kuwashughulikia. Tunaomba waondoke haraka kabla ya kukumbwa na oparesheni hii,” alionya Masauni. Alisema oparesheni hiyo haimaanishi Tanzania inawachukia raia wa kigeni, bali inalenga kuhakikisha sheria na taratibu za vibali vya kuishi nchini zinafuatwa.
Katika hatua nyingine,Masauni alisema serikali imefuta vibali vya muda vya kuishi nchini baada ya kubaini wageni wengi wamefanya udanganyifu mkubwa.
Alisema wengi wa wageni waliokuwa wakiingia nchini kwa kutumia vibali vya muda, walikuwa wakifanya udanganyifu wa kuvifanyia marekebisho ‘ku- renew’ kila wakati na kufanya waishi nchini kwa muda mrefu wakitumia vibali hivyo vya muda. “Badala yake tutatumia utaratibu wa vibali vipya,”alibainisha.
Katika kudhibiti watendaji wa Idara ya Uhamiaji, wanaojihusha na vitendo vya rushwa na kutokuwa waadilifu, Masauni alisema hivi sasa idara hiyo imeingizwa kwenye mfumo wa kijeshi, hivyo itaanzishwa mahakama ya kijeshi ndani ya idara hiyo.
“Tunajua kuna baadhi ya watendaji wa idara ambao si waaminifu na walikuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa, ikiwemo kuchelewesha kwa makusudi wateja kupata pasi za kusafi ria mahakama hii itawashughulikia,”alisema Masauni.
Baadhi ya Wachina na Wanaigeria waliokamatwa katika nyumba iliyoko Sinza Dar es Salaam