Palestina imekataa mazungumzo na marekani.

Palestina imekataa mazungumzo na marekani.

Drax001

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Posts
454
Reaction score
240
Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais Marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu ili kujadili uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia Yerusaleam kuwa mji mkuu wa Israel.
Ikulu ya Marekani imesema, uamuzi huo uliofikiwa na Palestina utakuwa hauna maana kwa kuwa hawataweza kupata suhulu ya mgogoro huo.
Makamu wa rais wa Marekani ana mpango wa kwenda katika ukanda huo wa mashariki ya kati lakini kiongozi wa ngazi za juu wa Palestina ,Jibril Rjoub amesema kuwa kiongozi huyo hakaribishwi Palestina.
Hatua hiyo imekuja mapema baada ya rais Trump kutangaza kuwa anautambua mji wa Yerusaleum kuwa mji mkuu,
Ambapo mpaka sasa Wapalestina takriban 31 wamejeruhiwa katika makabiliano yaliyozuka Ukanda wa Gaza na maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayotawaliwa na Israel kuhusu mji wa Jerusalem.
 
Waarabu huwezi kuongea nao mkasikilizana! Wanawezana wao kwa wao tu maana wote ni wazee wa kujitoa mhanga!
Waachane na mazungumzo hayo ambayo miaka nenda miaka rudi hayajawahi kuzaa matunda!
Kama waarabu hawaelewani wao kwa wao unategemea vipi waelewane na Israel? Ni kuwaacha wayamalize na Allah wao!
 
Ukisusa wenzio wala. . Maalim Seif maamuzi yake ya kususa susa yanaharibu dunia
 
Kwa kweli sasa ile option ya mwisho ya wapalestina ya kuvunja mamlaka yao ya ndani ( Palestinian Authority) na Kuanza kudai kuwa raia huru ndani ya ardhi nzima ya Israel na Westbank umewadia. Marekani Siyo honest broker wa amani!
 
Waarabu huwezi kuongea nao mkasikilizana! Wanawezana wao kwa wao tu maana wote ni wazee wa kujitoa mhanga!
Waachane na mazungumzo hayo ambayo miaka nenda miaka rudi hayajawahi kuzaa matunda!
Kama waarabu hawaelewani wao kwa wao unategemea vipi waelewane na Israel? Ni kuwaacha wayamalize na Allah wao!
Let i feed ur mind coz ur EMPTY CONTAINER, find this documents google or wherever...
- Ashkenazi jew.
- Balfour declaration. After that come back to the thread
 
Akifa mpalestina mmoja waisrael lazma wafe 10 na kuendelea hio ndio itikadi ya wapelestina wanaithamini saaana damu yao
Ndio maana unaona hata mtt wa miaka 10 nae anapigana hata arushe jiwe tu
Hapo truph kakalia kifuu cha nazi
 
Marekani inachafua dunia tujiandae na sisi wa dunia ya tatu tukiona vita vya marekani na N.k vimeanza tunatoa viwanajeshi vyetu kwenda kuisaidia North Korea
 
Akifa mpalestina mmoja waisrael lazma wafe 10 na kuendelea hio ndio itikadi ya wapelestina wanaithamini saaana damu yao
Ndio maana unaona hata mtt wa miaka 10 nae anapigana hata arushe jiwe tu
Hapo truph kakalia kifuu cha nazi
Umezungumza kinyume! Jiulize tangu machafuko haya ya juzi yalipoanza ni waisrael wangapi wamekufa na ni wapalestina wangapi wamekufa!
Kwa taarifa yako waisrael waliikufa ni 0 wapalestina waliokufa ni 4, Waisrael waliojeruhiwa ni 0 wapalestina waliojeruhiwa ni zaidi ya 200! Sifurahii hilo ila narekebisha madai yako!
 
Jerusalem ndo capital city ya Israel haina ubishi
 
Waarabu huwezi kuongea nao mkasikilizana! Wanawezana wao kwa wao tu maana wote ni wazee wa kujitoa mhanga!
Waachane na mazungumzo hayo ambayo miaka nenda miaka rudi hayajawahi kuzaa matunda!
Kama waarabu hawaelewani wao kwa wao unategemea vipi waelewane na Israel? Ni kuwaacha wayamalize na Allah wao!

Mkuu muogope sana Mungu...huyo unaemkashifu ndie anaekufanya ule,upumue uishi na kadhalika,,, na sio binadamu mwenzio, mpaka umefikia kujua kuandika na kusoma ni kutokana na huyo unaemkashifu...bila yeye sisi binadamu sio chochote....so tumia lugha nzuri yenye kumpendezesha Mungu aliekuumba,, na pia heshimu dini za watu n.k. Ahsante Mkuu
 
Maamuzi ya Marekani yanazidi kuuvuruga uhusiano wao, wanataka wakutane nao waongelee nini wakati wanazidi kuyafanya majadiliano yawe magumu.
 
Saudi anaua watu Yemeni no one anaandamana.Unajua Netanyau hajawapiga wapalestina siku nyingi,so walichofanya ni kuwagadhibisha ili wawatagwe vizuri.Maana jamaa hana mchezo kwenye kushusha mabomu.
 
Saudi anaua watu Yemeni no one anaandamana.Unajua Netanyau hajawapiga wapalestina siku nyingi,so walichofanya ni kuwagadhibisha ili wawatagwe vizuri.Maana jamaa hana mchezo kwenye kushusha mabomu.
Umesahau,waisrael walivyopigwa mpaka wakaomba,mapigano yasitishwe.
 
Back
Top Bottom