Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 752
- 3,096
Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesema Wapalestina hawataki msaada wowote kutoka kwa Marekani, baada ya Washington kutangaza kuwa itapunguza kiwango cha msaada wake wa kibinadamu kwa wananchi wa Palestina.
Saeb Erekat amesema: "Tumeiandikia barua rasmi Marekani kuitaka isimamishe misaada yake yote kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kwa kuwa kukubali misaada hiyo kutakuwa na taathira hasi kwa Wapalestina."
Amesema jambo jingine lililowapelekea kukataa misaada ya Washington ni Sheria ya Kupambana na Ugaidi ya ATCA iliyopasishwa na Rais Donald Trump wa Marekani Oktoba mwaka jana, ambayo inampa uwezo raia yeyote wa Marekani wa kuishtaki taasisi zinazopokea misaada hiyo ya US.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA
Mwaka uliopita, Marekani ilitangaza kukata misaada yake kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), uamuzi ambao ulikosolewa vikali na jamii ya kimataifa, ikiwemo ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Wadadisi wa mambo wanasema uamuzi wa Marekani wa kukatisha misaada yake kwa Wapalestina ni kujaribu kuwarubuni kimabavu ili wakubaliane na mpango wa "Muamala wa Karne" wa kuitokomeza kikamilifu kadhia ya Palestina.