Palestina akubaliwa kuwa mwanachama wa ICC

Palestina akubaliwa kuwa mwanachama wa ICC

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,232
Reaction score
3,334
Palestina kuwa mwanachama wa ICC

141209072749_icc_afp__640x360_afp_nocredit.jpg


Umoja wa mataifa umedhibitisha kuwa Palestina itakuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICC iliyo chini ya amri ya Roma kuanzia tarehe 1 mwezi Aprili mwaka huu.

Hii ni kulingana na taarifa kutoka kwa katibu-mkuu wa Umoja huo Ban ki-Moon, iliochapishwa katika mtandao wa mkataba wa Umoja wa Mataifa.

Uwanachama wa ICC utaiwawezesha Palestina kufuatilia mashtaka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Israeli katika siku zijazo.
Lakini pia utayawezesha makundi ya wapiganaji wa Kipalestina kushtakiwa.
150102175742_palistinians_icc_640x360__nocredit.jpg

Rais wa Palestina Mahmoud Abass alituma maombi ya kujiunga na mahakama ya uhalifu wa kivita wiki iliyopita, jambo lililoikasirisha Israeli.

Hatua hiyo inajiri huku Marekani na Israel zikipinga hatua hiyo na kusema kuwa itachochea uhasama kati ya Israel na Palestina.

Tayari Israel imesitisha fedha za kila mwezi za Palestina ambazo imekuwa ikichukua kama kodi kwa niaba yake.
Wiki iliopita waziri mkuu nchini Israel Benjamini Netanyahu alisema kuwa hatokubali wanajeshi wake kufikishwa mbele ya mahakama hiyo.

Chanzo: BBC
 
Baada ya Hamas kupata kichapo mwaka jana naona wamehamua kutafuta pa kukimbilia. Ingawa watakafikishwa ICC ni Hamas maana Waisrael tayari wamesema hawataruhusu askari wao apelekwe huko
 
Hivi kweli Bensouda anaweza kumfungulia mashtaka Netanyau kwa kufanya mauwaji ya halaiki huko Gaza?
 
Israel is not a member of the international court and refuses to recognize its jurisdiction. The ICC has no police force and no authority to go into Israel and arrest suspects however it could issue international arrest warrants that the European Union and other countries would be willing to enforce. That is the position of which Israel is frightened.
 
Hivi kweli Bensouda anaweza kumfungulia mashtaka Netanyau kwa kufanya mauwaji ya halaiki huko Gaza?
Nadhani unatakiwa ujifunze maana za maneno. Unajua maana ya neno halaiki?
 
By the way who are major financiers of the PA?
 
Baada ya Hamas kupata kichapo mwaka jana naona wamehamua kutafuta pa kukimbilia. Ingawa watakafikishwa ICC ni Hamas maana Waisrael tayari wamesema hawataruhusu askari wao apelekwe huko
dogo Hamas alishinda ile vita, Israel alibaki kupiga majumba tu:A S wink:
 
Back
Top Bottom