Jambo lako lina utata kidogo, na ili upate majibu ya kuridhisha unahitaji kutoa ufafanuzi wa maswali kadhaa. Hali ya kipato ya mume ipo vipi? Familia ya mwanamke kiuchumi ipoje? Hiyo tabia alianza lini? Au ndo tabia yake siku zote? Kama hali ya mwanaume ni nzuri kiuchumi basi ujue kinachomweka hapo ni pesa tu na si kingine. Maana kama mtu humpendi kinachokukalisha ni nini? Pia kama ke kwao kupo hovyo lazima atarudi tu. Ila kama hiyo tabia ya kuchonga mdomo aliianza tangu mwanzo wa ndoa basi huyo ni tabia yake na hata kwa mwanaume mwingine atafanya hivyo hivyo. Lakin kama alibadilika mwishon basi ni wazi kuna kitu hakipendi kwenye hiyo ndoa ila kusema direct anashindwa. Ni vizuri tukawajua wenza wetu kabla ya kuchukua maamuzi makubwa kama ndoa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.