Pale Tanzania ilipoaibika

Hili mnge waambia viongozi wenu wa vyama. Ndio waliowanyima kuchagua wawakilishi wenu baada ya kususia uchaguzi.
Nini kilichopelekea wao kususa,
Kwann watendaji walizikimbia ofisi zao nchi nzima kwa style iliyofanana
 
Ngumu kumeza, sema ndio hivyo wao wanaona wamepata role model.
 
A
 
Umeondoka Georgina. Umetuachia masikitiko. Georgina wa mamaa...

Aliimba kwa huzuni Jabali la Muziki Marijani Rajab.
 
Naona maandishi yako umeyatoa kwa nyuma kwa fwasi ya dwasi.
 
Umeondoka Georgina. Umetuachia masikitiko. Georgina wa mamaa...

Aliimba kwa huzuni Jabali la Muziki Marijani Rajab.
Dady you always speak hard language,can you let me know what are you meaning?
Am so tired to use my brain to understand you..
 
Dady you always speak hard language,can you let me know what are you meaning?
Am so tired to use my brain to understand you..
No worries baby.

Nimemkumbuka mzee wa busara Dr. Mahiga tu, kuondoka kwake Wizara ya Mambo ya Nje kumetuachia masikitiko.

Dr. Mahiga angeweza kujieleza vizuri zaidi.

Huo wimbo wa Georgina ni wimbo aliimba Marijani Rajab kuhusiana na Georgina, mtoto wa kaka yake Dr. Augustine Philip Mahiga.

Marijani Rajab alikuwa na rafiki yake mmoja aliyekuwa mpenzi wa Georgina. Wakati huo Georgina akiwa anasoma sekondari na anakaa kwa Dr. Mahiga na Marijani Rajab akisoma Tambaza.

Ujana maji ya moto. Sasa huyo binti Georgina akapatwa na madhila ya mapenzi akarudishwa kwao Iringa na familia ya Dr. Mahiga.

Rafiki yake Marijani akamuhadithia kisa Marijani. Marijani akatunga huo wimbo maarufu kwetu sisi vijana wa miaka hiyo.

Kuna mdau aliandika hii story kirefu alipofariki Georgina.

Namnukuu hapa chini.


*BURIANI GEORGINA MAHIGA!!!*

BONGOLANDERS wengi wanaufahamu vizuri wimbo maarufu wa *GEORGINA* ulioimbwa na mmoja wa waimbaji bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania aitwae MARIJANI RAJAB "JABALI LA MUZIKI" akiwa na bendi yake ya Safari Trippers. Ni wimbo ambao hupendwa sana na Wahenga na wala hauchuji licha ya kwamba uliimbwa miaka ya mwanzoni ya 70.

GEORGINA MAHIGA ambaye amefariki wiki hii, alikuwa ni mtoto wa kaka mkubwa wa Mh. AUGUSTIN PHILLIP MAHIGA , Waziri wa Katiba na Sheria.

Je, ilikuwaje hadi JABALI LA MUZIKI kumtungia wimbo Bi.GEORGINA? Ni kwamba Bi.GEORGINA alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Zanaki, Dsm. Akiwa kidato cha pili mwaka 1974 alipata mimba. Mimba hiyo alipewa na Boy friend wake aliyekuwa akisoma kidato cha pili pia shule ya sekondari ya Tambaza na rafiki mkubwa wa JABALI LA MUZIKI ambalo pia lilikuwa likisoma shuleni hapo.

Mama Mahiga akaamua kumpeleka GEORGINA Iringa bila ya akina JABALI LA MUZIKI kujua aliko GEORGINA. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa rafiki yake JABALI LA MUZIKI aliyempa uja uzito huo kwani alikuwa akimpenda kwa dhati ila alikuwa hajui yuko wapi na kila siku alikuwa akilalamika kwa JABALI LA MUZIKI ambalo likaamua kuichangamkia fursa hiyo na kutunga wimbo huo uliotokea kuwa moja ya nyimbo bora za wakati wote Bongo!.

Bi. Georgina alijifungua mtoto wa kiume ambaye bahati mbaya alifariki mwaka juzi.

Mashairi ya wimbo GEORGINA:

_*"Ooh Georgina, siku uliyoondoka uliniacha nalia na machozi, umekwenda kuishi mbali nami, Georgina wa mamaa"*_*X 2*

_*"Sipatii usingizi nikikumbuka tulivyoishi mi na we Georgina"*_*X 2*

_*"Umeondoka Georgina umeniachia masikitiko, ooh nauliza Georgina ni lini utarudi, uniondoe wasiwasi, Georgina wa mamaa" X 2*_

Katika hii picha hapa chini yenye wamama watano waliovalia nguo nyeupe, Bi. GEORGINA ni wa kwanza kushoto wakati wa uhai wake alipokuwa kwenye msiba wa baba yake mwaka juzi.

Bi. GEORGINA amezikwa leo jioni ya jumapili tarehe 4 Agosti 2019 kwenye makaburi ya Kinondoni, Dsm.

Bwana alitoa Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

*ALLEZ ALLEZ ALLEZ LFC!!!*

 
Ahsante sana mkuu, umeandika mambo mazito sana kwa mtazamo wa ndani sana. Sina hakika kama wengi wamekuelewa. lakini endelea kuandika mkuu, yatawasaidia wengi.
Ahsante sana pia kuhusu hiyo story ya Georgina. Nilikuwa pia kijana enzi hizo, nimefurahi sana kupata story kamilifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…