wa stendi
JF-Expert Member
- Jul 7, 2016
- 26,008
- 28,342
Kweli
Kabudi hana tifauti na Le profesel wa Ze comedy
Kabudi hana tifauti na Le profesel wa Ze comedy
Nini kilichopelekea wao kususa,Hili mnge waambia viongozi wenu wa vyama. Ndio waliowanyima kuchagua wawakilishi wenu baada ya kususia uchaguzi.
AIlikuwa ni siku ya aibu kubwa sana ambayo ni wachache wenye macho waliona jinsi Tanzania tulivyoaibika.
Tanzania, ambayo ni hivi karibuni tu tumetoka katika uchaguzi unaonuka uvundo mkali, ambapo jitihada za makusudi zilifanywa kupora uchaguzi mchana kweupe kwa mbinu mbalimbali chafu (kufunga ofisi wiki nzima, kukamatwa wagombea wanapochukua fomu, wengine kuenguliwa kwa visingizio na sio vigezo, na mengineyo mengi kama hayo).
Tanzania kupitia kwa Profesa Kabudi, ilidiriki kuitaka Kenya kujifunza kutoka Tanzania!
Profesa Kabudi ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na hotuba yake fupi katika sherehe ya uzinduzi wa Ripoti ya BBI huko Kenya, kwa kweli alikuwa katika ubora wake katika usanii.
Baada ya kuwa-lecture Wakenya kuhusu ukabila (ambao serikali ya Magufuli inajitahidi kwa nguvu zote kuufufua, na kuongeza bonasi ya ukanda juu yake), aliwainua na kuwaimbisha wimbo wa kuwataka waachane na mambo ambayo serikali ya Tanzania aliyoiwakilisha inayaenzi na kuyaimarisha; kuwatenga watu katika imani zao za kisiasa, kwa mfano, wakati tunaimba MAENDELEO HAYANA VYAMA.
Lakini kubwa sana ambalo hata Profesa Kabudi na ubingwa wake katika usanii hakuliona, ni ile tofauti kubwa kati ya Kenya na Tanzania.
Kwamba pale kwenye meza kuu kulikuwa na Rais, Makamu wake, na kiongozi wa upinzani. Yaani tuseme Magufuli ameketi beneti kabisa na Mbowe, halafu pembeni yupo mama Suluhu.
Halafu katika ukumbi wamejaa viongozi mbalimbali, lakini hasa viongozi wa vyama vyote vya siasa. halaiki kama hiyo tu haijawahi kutokea hapa kwetu na wala hatutarajii kwamba Magufuli atakuwa na uthubutu wa kuiitisha, japo angekuwa na ujasiri hata tone tu ya ule ujasiri wa Kikwete, angeweza kabisa.
Magufuli amekutana na viongozi wa dini, wafanyabiashara, na makundi mbalimbali lakini anaogopa kukutana na viongozi wa siasa kutoka upinzani, ambao wapo kisheria kabisa, na anaidhinisha kila mwezi walipwe fedha ya ruzuku kutoka makusanyo ya kodi.
Siwezi kufikiria kitu cha ajabu zaidi ya hiki. mwenyewe anasema kwa kejeli eti watamchinja! Pengine kweli akikutana nao watamchinja. KISIASA.
Lakini Rais Kenyata na Mzee Raila wamediriki kukutana na kupeana mikono, baada ya Raila kujitangazia urais wa watu (People's president).
Kenyata anasema mwenyewe haikuwa rahisi. Dakika 45 za mwanzo hakuna cha maana walichoongea, kila mtu amejaa hasira.
Lakini walijifungia ndani na hawakutoka humo mpaka wamepeana handshake. Hivyo Magufuli asifikiri wale ni wajinga.
Mchambuzi mmoja alipoulizwa mbona kuna ripoti nyingi tu huko Kenya kwa madhara yaliyotokea huko nyuma, alijibu kwamba tofauti ya hizo ripoti na hii ni kwamba hii inatokana na msukumo wa kisiasa.
Hivyo uwezekano mkubwa wa kufanya kazi. ni sawa na ile serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambayo iliwezekana pale Maalim Seif na Abeid Karume walipokaa pamoja.
Hii ni habari njema sana kwa wapenda demokrasia, wapenda amani, duniani kote. maridhiano ndiyo kauli mbiu.
Ndicho serikali ya Magufuli ilitakiwa kufanya mara tu baada ya kusikia wapinzani wamesusia uchaguzi.
Maridhiano. Siyo kiburi na ubabe. Eti ukisusa siye twala! huko ni kucheza kamari kwa mambo muhimu ya kitaifa.
Wakenya wamefika hapo kwa historia mbaya sana ya chaguzi zao. Na sisi tunangoja tupite humo humo kwenye machafuko? Vinginevyo basi sisi siyo binadamu, ni robots!
Tulichonacho kinaweza kuwa kibaya kuliko ukabilaTanzania Hakuna ukabila
Usitufananishe na kenya
Tumacho tuzuri, eh?
Naona maandishi yako umeyatoa kwa nyuma kwa fwasi ya dwasi.Ilikuwa ni siku ya aibu kubwa sana ambayo ni wachache wenye macho waliona jinsi Tanzania tulivyoaibika.

Dady you always speak hard language,can you let me know what are you meaning?Umeondoka Georgina. Umetuachia masikitiko. Georgina wa mamaa...
Aliimba kwa huzuni Jabali la Muziki Marijani Rajab.
No worries baby.Dady you always speak hard language,can you let me know what are you meaning?
Am so tired to use my brain to understand you..
Ni kweli hana ufahamu!Na kweli. Halafu anaongea kwa mbwembwe utazania hana ufahamu hata kidogo
Ahsante sana mkuu, umeandika mambo mazito sana kwa mtazamo wa ndani sana. Sina hakika kama wengi wamekuelewa. lakini endelea kuandika mkuu, yatawasaidia wengi.No worries baby.
Nimemkumbuka mzee wa busara Dr. Mahiga tu, kuondoka kwake Wizara ya Mambo ya Nje kumetuachia masikitiko.
Dr. Mahiga angeweza kujieleza vizuri zaidi.
Huo wimbo wa Georgina ni wimbo aliimba Marijani Rajab kuhusiana na Georgina, mtoto wa kaka yake Dr. Augustine Philip Mahiga.
Marijani Rajab alikuwa na rafiki yake mmoja aliyekuwa mpenzi wa Georgina. Wakati huo Georgina akiwa anasoma sekondari na anakaa kwa Dr. Mahiga na Marijani Rajab akisoma Tambaza.
Ujana maji ya moto. Sasa huyo binti Georgina akapatwa na madhila ya mapenzi akarudishwa kwao Iringa na familia ya Dr. Mahiga.
Rafiki yake Marijani akamuhadithia kisa Marijani. Marijani akatunga huo wimbo maarufu kwetu sisi vijana wa miaka hiyo.
Kuna mdau aliandika hii story kirefu alipofariki Georgina.
Namnukuu hapa chini.
![]()
Marijani Rajabu | Lyrics, Song Meanings & Music Videos
Marijani Rajabu (born in Kariakoo, Dar es Salaam, Tanzania, 3rd March 1955-1995) was a popular dance musician and singer. As a member of The Trippers (later known as Travel Trippers), he was most known for composing and performing songs such as Georgina, Rosa Go To School, and Spear In The...sonichits.com
*BURIANI GEORGINA MAHIGA!!!*
BONGOLANDERS wengi wanaufahamu vizuri wimbo maarufu wa *GEORGINA* ulioimbwa na mmoja wa waimbaji bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania aitwae MARIJANI RAJAB "JABALI LA MUZIKI" akiwa na bendi yake ya Safari Trippers. Ni wimbo ambao hupendwa sana na Wahenga na wala hauchuji licha ya kwamba uliimbwa miaka ya mwanzoni ya 70.
GEORGINA MAHIGA ambaye amefariki wiki hii, alikuwa ni mtoto wa kaka mkubwa wa Mh. AUGUSTIN PHILLIP MAHIGA , Waziri wa Katiba na Sheria.
Je, ilikuwaje hadi JABALI LA MUZIKI kumtungia wimbo Bi.GEORGINA? Ni kwamba Bi.GEORGINA alikuwa akisoma shule ya sekondari ya Zanaki, Dsm. Akiwa kidato cha pili mwaka 1974 alipata mimba. Mimba hiyo alipewa na Boy friend wake aliyekuwa akisoma kidato cha pili pia shule ya sekondari ya Tambaza na rafiki mkubwa wa JABALI LA MUZIKI ambalo pia lilikuwa likisoma shuleni hapo.
Mama Mahiga akaamua kumpeleka GEORGINA Iringa bila ya akina JABALI LA MUZIKI kujua aliko GEORGINA. Ilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa rafiki yake JABALI LA MUZIKI aliyempa uja uzito huo kwani alikuwa akimpenda kwa dhati ila alikuwa hajui yuko wapi na kila siku alikuwa akilalamika kwa JABALI LA MUZIKI ambalo likaamua kuichangamkia fursa hiyo na kutunga wimbo huo uliotokea kuwa moja ya nyimbo bora za wakati wote Bongo!.
Bi. Georgina alijifungua mtoto wa kiume ambaye bahati mbaya alifariki mwaka juzi.
Mashairi ya wimbo GEORGINA:
_*"Ooh Georgina, siku uliyoondoka uliniacha nalia na machozi, umekwenda kuishi mbali nami, Georgina wa mamaa"*_*X 2*
_*"Sipatii usingizi nikikumbuka tulivyoishi mi na we Georgina"*_*X 2*
_*"Umeondoka Georgina umeniachia masikitiko, ooh nauliza Georgina ni lini utarudi, uniondoe wasiwasi, Georgina wa mamaa" X 2*_
Katika hii picha hapa chini yenye wamama watano waliovalia nguo nyeupe, Bi. GEORGINA ni wa kwanza kushoto wakati wa uhai wake alipokuwa kwenye msiba wa baba yake mwaka juzi.
Bi. GEORGINA amezikwa leo jioni ya jumapili tarehe 4 Agosti 2019 kwenye makaburi ya Kinondoni, Dsm.
Bwana alitoa Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!
*ALLEZ ALLEZ ALLEZ LFC!!!*
View attachment 1276111