Pale Tanzania ilipoaibika

Pale Tanzania ilipoaibika

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,998
Ilikuwa ni siku ya aibu kubwa sana ambayo ni wachache wenye macho waliona jinsi Tanzania tulivyoaibika.

Tanzania, ambayo ni hivi karibuni tu tumetoka katika uchaguzi unaonuka uvundo mkali, ambapo jitihada za makusudi zilifanywa kupora uchaguzi mchana kweupe kwa mbinu mbalimbali chafu (kufunga ofisi wiki nzima, kukamatwa wagombea wanapochukua fomu, wengine kuenguliwa kwa visingizio na sio vigezo, na mengineyo mengi kama hayo).

Tanzania kupitia kwa Profesa Kabudi, ilidiriki kuitaka Kenya kujifunza kutoka Tanzania!

Profesa Kabudi ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na hotuba yake fupi katika sherehe ya uzinduzi wa Ripoti ya BBI huko Kenya, kwa kweli alikuwa katika ubora wake katika usanii.

Baada ya kuwa-lecture Wakenya kuhusu ukabila (ambao serikali ya Magufuli inajitahidi kwa nguvu zote kuufufua, na kuongeza bonasi ya ukanda juu yake), aliwainua na kuwaimbisha wimbo wa kuwataka waachane na mambo ambayo serikali ya Tanzania aliyoiwakilisha inayaenzi na kuyaimarisha; kuwatenga watu katika imani zao za kisiasa, kwa mfano, wakati tunaimba MAENDELEO HAYANA VYAMA.

Lakini kubwa sana ambalo hata Profesa Kabudi na ubingwa wake katika usanii hakuliona, ni ile tofauti kubwa kati ya Kenya na Tanzania.

Kwamba pale kwenye meza kuu kulikuwa na Rais, Makamu wake, na kiongozi wa upinzani. Yaani tuseme Magufuli ameketi beneti kabisa na Mbowe, halafu pembeni yupo mama Suluhu.

Halafu katika ukumbi wamejaa viongozi mbalimbali, lakini hasa viongozi wa vyama vyote vya siasa. halaiki kama hiyo tu haijawahi kutokea hapa kwetu na wala hatutarajii kwamba Magufuli atakuwa na uthubutu wa kuiitisha, japo angekuwa na ujasiri hata tone tu ya ule ujasiri wa Kikwete, angeweza kabisa.

Magufuli amekutana na viongozi wa dini, wafanyabiashara, na makundi mbalimbali lakini anaogopa kukutana na viongozi wa siasa kutoka upinzani, ambao wapo kisheria kabisa, na anaidhinisha kila mwezi walipwe fedha ya ruzuku kutoka makusanyo ya kodi.

Siwezi kufikiria kitu cha ajabu zaidi ya hiki. mwenyewe anasema kwa kejeli eti watamchinja! Pengine kweli akikutana nao watamchinja. KISIASA.

Lakini Rais Kenyata na Mzee Raila wamediriki kukutana na kupeana mikono, baada ya Raila kujitangazia urais wa watu (People's president).

Kenyata anasema mwenyewe haikuwa rahisi. Dakika 45 za mwanzo hakuna cha maana walichoongea, kila mtu amejaa hasira.

Lakini walijifungia ndani na hawakutoka humo mpaka wamepeana handshake. Hivyo Magufuli asifikiri wale ni wajinga.

Mchambuzi mmoja alipoulizwa mbona kuna ripoti nyingi tu huko Kenya kwa madhara yaliyotokea huko nyuma, alijibu kwamba tofauti ya hizo ripoti na hii ni kwamba hii inatokana na msukumo wa kisiasa.

Hivyo uwezekano mkubwa wa kufanya kazi. ni sawa na ile serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambayo iliwezekana pale Maalim Seif na Abeid Karume walipokaa pamoja.

Hii ni habari njema sana kwa wapenda demokrasia, wapenda amani, duniani kote. maridhiano ndiyo kauli mbiu.

Ndicho serikali ya Magufuli ilitakiwa kufanya mara tu baada ya kusikia wapinzani wamesusia uchaguzi.

Maridhiano. Siyo kiburi na ubabe. Eti ukisusa siye twala! huko ni kucheza kamari kwa mambo muhimu ya kitaifa.

Wakenya wamefika hapo kwa historia mbaya sana ya chaguzi zao. Na sisi tunangoja tupite humo humo kwenye machafuko? Vinginevyo basi sisi siyo binadamu, ni robots!
 
Kwanza ni makosa kuita ule ni uchaguzi.Neno sahihi ni uchafuzi.Tafsri ya uchaguzi ni kitendo cha watu kupewa haki ya kuwachagua wawakilishi wao pasiposhuruti yaani kwa hiari,na sio watu kulazimishwa kuchaguliwa wawakilishi wao.Pale haki ya watu kuchagua imeporwa.
 
Hwawa wat wanaandaliw wakaongee nini ila waandaaji wanasahau kuwa speach nyingine zinadepend na mazingira. Ni kwa mfno ap kabudi kaandaliwa aongee ivyo ila mazingira yanapinga anachokiongea ila kwakuwa ni msomi ( wasiofikiria) anaongea tu alivyopangiwa.
 
Tanzania Hakuna ukabila
Usitufananishe na kenya
Wala hatuwezi kujifananisha na Kenya. wale wapo mbali sana. kule kuna binadamu aisee. sina hakika kama Tanzania nzima siyo Serengeti na ngorongoro na mikumi. sisi wote ni nyumbu na pundamilia tu
 
Hwawa wat wanaandaliw wakaongee nini ila waandaaji wanasahau kuwa speach nyingine zinadepend na mazingira. Ni kwa mfno ap kabudi kaandaliwa aongee ivyo ila mazingira yanapinga anachokiongea ila kwakuwa ni msomi ( wasiofikiria) anaongea tu alivyopangiwa.
Na kweli. Halafu anaongea kwa mbwembwe utazania hana ufahamu hata kidogo
 
Kwanza ni makosa kuita ule ni uchaguzi.Neno sahihi ni uchafuzi.Tafsri ya uchaguzi ni kitendo cha watu kupewa haki ya kuwachagua wawakilishi wao pasiposhuruti yaani kwa hiari,na sio watu kulazimishwa kuchaguliwa wawakilishi wao.Pale haki ya watu kuchagua imeporwa.
Ni kweli. Ule siyo UCHAGUZI, ni UCHAFUZI.
 
Sasa unataka Tanzania tuwe na maridhiano kama Kenya? Hivi unafahamu kwa nini hao viongozi wapo pale? Mambo usiyoyajua bora kukaa kimya. Tanzania ndio baba lao kwa Demokrasi Afrika kama hufahamu uliza.
 
Ujui maana ya demokrasia
 
Sasa unataka Tanzania tuwe na maridhiano kama Kenya? Hivi unafahamu kwa nini hao viongozi wapo pale? Mambo usiyoyajua bora kukaa kimya. Tanzania ndio baba lao kwa Demokrasi Afrika kama hufahamu uliza.
Najua kuna tofauti kubwa kati ya vyama vya siasa Kenya na Tanzania. lakini wana matatizo yao katika mfumo wao. kitu kikubwa THEY ARE TALKING ABOUT IT!!! Sisi Rais wetu anajipongeza kwa KUPORA? nakubaliana na wewe kwamba Tanzania ni BABA LAO KATIKA UPORAJI WA DEMOKRASIA KATIKA DUNIA. nimefanya marekebisho machache kwenye kauli yako. chini ya Magufuli sasa tumeingia viwango vya uporaji vya kidunia
 
Kama huzijui siasa za Afrika unaweza kuendelea kuzicheza bila kujua!

Hujiulizi kwa nini maridhiano haya yanayotokea Kenya hayakufanyika wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kenyatta?

Rais yoyote wa Afrika anapoingia kwenye awamu yake ya mwisho ya uongozi kikatiba huwa anaanza kujiandaa na maisha ya uraiani kwa kuanza kujenga mazingira ili aonekane aliwaunganisha wananchi!

Kumbuka baada ya Rais Kenyatta kushinda Urais wa awamu ya pili ndio akaanza kutafuta majadiliano na kambi ya Odinga kwa sababu haikuwa tena kikwazo kwake.

Rais Kenyatta kwa sasa hana hofu ya kupoteza madaraka na kwa sababu hiyo ndio maana ukiangalia mapambano yamehamia kwa Makamu wa Rais Ruto na Odinga kwa vile wanajiandaa kugombea Urais.

Kinachoshangaza unatoa lawama kwa Prof. Paramangamba kama vile alijipeleka bila kualikwa kwenye mkusanyiko huo! Kama Wakenya wanadhani wao ni bora zaidi ya Tanzania, kwa nini waliwaalika viongozi utawala wa Tanzania kama ndio wageni Mkuu wakati kwa mtazamo wako kuna nchi nyingine zilizobora kwenye nyanja za kisiasa!

Kambi ya Ruto na Odinga kwa sasa hawakai hata meza moja na kila siku wanarushiano lawama na matusi.
 
Rudia ulichoandika nimetoka kapa.
 
Brother nafikiri umeaibika wewe na hii thread yako. Wala sijaelewa ulikiwa unataka kuleta ujumbe gani.
 
Kama huzijui siasa za Afrika unaweza kuendelea kuzicheza bila kujua!

Hujiulizi kwa nini maridhiano haya yanayotokea Kenya hayakufanyika wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kenyatta?

Rais yoyote wa Afrika anapoingia kwenye awamu yake ya mwisho ya uongozi kikatiba huwa anaanza kujiandaa na maisha ya uraiani kwa kuanza kujenga mazingira ili aonekane aliwaunganisha wananchi!

Kumbuka baada ya Rais Kenyatta kushinda Urais wa awamu ya pili ndio akaanza kutafuta majadiliano na kambi ya Odinga kwa sababu haikuwa tena kikwazo kwake.

Rais Kenyatta kwa sasa hana hofu ya kupoteza madaraka na kwa sababu hiyo ndio maana ukiangalia mapambano yamehamia kwa Makamu wa Rais Ruto na Odinga kwa vile wanajiandaa kugombea Urais.

Kinachoshangaza unatoa lawama kwa Prof. Paramangamba kama vile alijipeleka bila kualikwa kwenye mkusanyiko huo! Kama Wakenya wanadhani wao ni bora zaidi ya Tanzania, kwa nini waliwaalika viongozi utawala wa Tanzania kama ndio wageni Mkuu wakati kwa mtazamo wako kuna nchi nyingine zilizobora kwenye nyanja za kisiasa!

Kambi ya Ruto na Odinga kwa sasa hawakai hata meza moja na kila siku wanarushiano lawama na matusi.

Ruto na odinga ni janga kwa ustawi Wa Kenya wafikirie wengine,wote ni wanavisasi dunia ilishatoka huko.
 
Mie naona ule uteuzi ndio ulikuwa uchaguzi wenyewe,

maana hata wale waliojitokeza ili kuwapigia kura hawakupiga maana waliambiwa mgombea alipita bila kupingwa!!

Sasa je waliompitisha bila kupigiwa kura na wapiga kura, alipita lini kwenda kwenye hatua ya kuwa mtunukiwa ushindi huo wa bila kupigiwa kura?
 
Kwanza ni makosa kuita ule ni uchaguzi.Neno sahihi ni uchafuzi.Tafsri ya uchaguzi ni kitendo cha watu kupewa haki ya kuwachagua wawakilishi wao pasiposhuruti yaani kwa hiari,na sio watu kulazimishwa kuchaguliwa wawakilishi wao.Pale haki ya watu kuchagua imeporwa.
Hili mnge waambia viongozi wenu wa vyama. Ndio waliowanyima kuchagua wawakilishi wenu baada ya kususia uchaguzi.
 
Back
Top Bottom