Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,005
- 1,489
Habari zenu wakuu?
Utu umekanyagwa ubinadamu umepuuzwa na inavyoonekana hatma ya thamani ya kila kiumbe ipo mikononi mwake yeye mwenyewe.
Hoja yangu inawezekana kuonekana kuwa nyepesi kwa wale watakao ichukulia juu juu ila kwa watakao itafakari wataona uzito na umuhimu wake.
Naamini mlio wengi kama si nyote mnaijua na mnaiona midoli ya kiume na y akike inayotumiwa na wafanyabiashara wa nguo, inapendeza na kuvutia pale inapokuwa imevishwa nguo lakini inakera na kuudhi unapoiona bila mavazi.
Inafikirisha kwakweli hakuna tofauti yeyote na mtu aliekua Uchi, ni uchi zaidi ya uchi wa mnyama. Mdoli wa mwanamama uliochongwa vizuri vizuri kabisa, ukionesha maungo yake ya sirini yote kwa uwazi kabisa umesimamishwa nje ya duka katika ya mji eneo lenye watu umati kila apitae anaona. Mama zao wanaliona ,baba zao wanaliona, wake zao na watoto zao wote wanaliona sisemi wanaliangalia maana wapo wanaolaani sana ila hawana hatua ya kuchukua.
Kuna wakati unaweza kuona hakuna tofauti ya mwenye akili na chizi kwa matendo yao isipokuwa mwenye akili anakusudia na chizi anafanya pasi na lengo maalum.