Pale busara inapotoweka Maafa yaja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pale busara inapotoweka Maafa yaja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shayu, Oct 26, 2012.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Katika maisha yote kutoka karne nyingi busara ndio imekuwa kiongozi na mlinzi wa vizazi vingi.
  Mataifa mengi yalijengwa, kukuzwa, kulindwa na kuongozwa na busara. Na pale busara inapotoweka baadae ya vizazi huwa hatarini.


  Watu wenye maono ni muhimu katika Taifa lolote pasipo maono Mataifa huangamia na kupotea kabisa. Na sisi kama Taifa tunachangamoto hiyo. Tunachangamoto kubwa ambazo viongozi wengi wa Taifa hili sidhani kama wanazifikiria pengine wanafikiri nchi hii itajiongoza yenyewe bila maono.

  Taifa hili linahitaji mwelekeo na mwelekeo huu utakuwepo pale tu watu stahili watakapoingia madarakani na wale waliopo madarakani kuwaachia kapteni anayeweza kuongoza meli kuipeleka katika nchi istahiliyo na kuzuia mawimbi yaliyopo sasa hivi.

  Katika Taifa hili ni lazima tuelewe kwamba sio kila mtu anastahili kuwa kiongozi.


  Uongozi ni jukumu kubwa sana na yeyote yule anayetaka kuongoza watu lazima ajue ni wapi anataka kuipeleka jamii yake na Taifa lake, ni aina gani ya Taifa analotaka kulijenga na ni jinsi gani ataunganisha watu wa makabila tofauti na dini tofauti waje pamoja katika lengo moja la ujenzi wa Taifa letu kuelekea sehemu fulani.


  Ili tuendelee lazima tujue ni wapi tunataka kwenda. Hatujawa taifa ili tutafute mkate tu, Tumekuwa Taifa ili tufikie kilele fulani cha mafanikio na hili haliwezi kufanikiwa kama hatutaweza kuunganisha vipande vinavyotengeneza Taifa hili. Bila kuelewana sisi kwa sisi na kuwa na lugha moja kamwe hatutaweza kulijenga Taifa hili. Ni lazima tutambue kwanza sisi ni ndugu na tuthaminiane na kuheshimiana. Ni lazima tutambue kwamba tuna majukumu ya pamoja ya ujenzi wa Taifa hili na vizazi vyetu vijavyo vinatutegemea sisi ili kujenga mazingira mazuri kwao.


  Ni lazima tujenge upya familia zetu katika misingi imara, ni lazima tujenge upya mahusiano yetu kama tunataka Taifa hili liendelee. Tutakapo kuwa na order pamoja na harmony katika jamii yetu ni hatua ya kwanza kwa Taifa letu kuendelea.


  Wajibu kwa familia ni msingi imara wa ujenzi wa Taifa bora. Ni jinsi gani tunawalea watoto wetu katika Utaifa na maadili bora? familia zetu hazijajengwa katika misingi ya utaifa. Watoto wetu wanajikulia kama uyoga bila malezi bora ya kuheshimu utaifa wao na uzalendo, bila maadili na discipline.

  Ni muhimu kuwa na wajibu wa pamoja katika maendeleo ya Taifa hili, tukifahamu kwamba tunatengeneza baadae ya watoto wetu. Taifa hili tutaliendesha kwa akili zetu na busara zetu na tutaliua pia kwa ujinga wetu. Ni lazima turudishe akili zetu na tuanze kufikiria. Tunahitaji mabadiliko ya fikra na moyo. Tunahitaji kupendana na kuthaminiana. Tunauwezo wa kukaa pamoja na ku plan future ya Taifa letu kama watu wenye akili timamu. Taifa letu halina maaadili hakuna Order. Hatutaweza kuendelea bila ya vitu hivyo viwili.


  Wote tunashuhudia jinsi Taifa hili linavyo mong'onyoka. Ni dhahiri tunahitaji juhudi za makusudi ili kuleta watu wetu pamoja wa dini zote na kabila zote na matabaka yote ili tuwe na lengo moja la ujenzi wa Taifa letu. Ambalo ni muhimu sana kwetu. Mimi binafsi silijui Taifa lingine lolote zaidi ya hili. Nimekula na kukuzwa na chakula kinachoota katika ardhi hii na nina amini katika Taifa hili na bado nina matumaini tunaweza kubadilika. Nina amini Taifa hili linauwezo wa kuwa kama Taifa lolote lingine kubwa. Ni umoja wetu na nia yetu ya kutofifia ya kuleta mabadiliko ya maisha yetu. Ni muhimu wazazi wa Taifa hili kuwa wamoja na kutilia mkazo jinsi tunavyowakuza watoto ambao ndio viongozi wa baadae. Baadae ya Taifa hili iko chini ya vizazi vijavyo pia. Tukijitayarisha Taifa hili nina uhakika lina uwezo wa kuwa super power. Ni kujipanga tu na jitihada zetu. Ni lazima tuwe Taifa la watu wenye Malengo.


  Najua watu wa serikali mnaweza kusoma wakaraka huu tunahitaji tubadilishe mawazo yetu, tunavyofikiri sivyo. Ubinafsi hautotupeleka popote. Ni sawasawa kukata mti tuliokalia wenyewe. Tunauwezo wa ku organize watu wetu ili kujiletea maendeleo yetu wenyewe. Ni lazima tufuate njia iliyo salama njia hii hapana tutapigana wenyewe kwa wenyewe. Amani ya nchi ikitoweka ni vigumu kuirudisha. Furaha haitokani na wingi wa mali alizonazo mtu akizungukwa na maskini kibao bali furaha ya Taifa hutokana na mafanikio ya pamoja.

  Tunauwezo wa kuwa Taifa imara kama tukipendana na kuchukuliana kama ndugu ambao hatma yao ni moja. Ni lazima tunyanyuane wenyewe kwa wenyewe. Roho ya Taifa hili lazima inyanyuke upya. Kama sisi ni Taifa sisi ni ndugu. Enzi za utawala wa kisultani wa kutawala kwa kujinufaisha lazima uishe ije enzi ya kutumikia, enzi ya uongozi na heshima. Enzi za viongozi na wananchi kuwa kitu kimoja.


  Taifa hili linahitaji mabadiliko makubwa ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kama nilivyoongea katika maandiko yangu mengi kuhusu familia naipa nafasi kubwa sana katika uwezo wake wa kujenga Taifa imara. Kama wazazi wakiwa na uwezo wa kutwala nyumba zao na ku discipline watoto wao na kama wao wenyewe kwa wenyewe wakiwa na mahusiano mazuri na mashirikiano tutakuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza future yao kwa pamoja ili baadae na wao wawe na majukumu ya kutengeneza baadae nzuri kwa wanaokuja. Ni lazima tujue kwamba familia ni sehemu ndogo ya Taifa. Uongozi mbovu unatokana na familia mbovu tulizo nazo. Watoto wetu wanakuwa kama uyoga bila discipline.


  Taifa hili ni kama mbegu zilizomwagwa shambani bila mpangilio, mazao yakakua ovyo ovyo. Taifa haliwezi kuendelea hivyo. Ni lazima tuanze na mabadiliko ya watu. Ni lazima tuanze na fikra na maadili ya watu. Ni lazima tuzingatie umuhimu wa familia na social order. Ni lazima tukubali tumezaliwa hivyo kutoka kwa wazee wasio zingatia umuhimu wa familia, wasiojali familia. Tunahitaji mabadiliko ya fikra kwakuwa hii inaleta social disorder. Wazee wanaoona kuwa na nyumba ndogo ni sahihi. Tunahitaji mabadiliko. Watoto wetu wanahitaji malezi bora ili wawe viongozi bora.


  Watu wanafikiri kwamba pesa ni kila kitu. Wanatafuta hata kwa njia zisizostahili hata kama zitatugawa na kuweka rehani baadae yetu kama Taifa. Kama tutakuwa na fikra hizo Taifa hili halitokalika kama tukifikiri kwamba utu wa mtu unatokana na mali alizonazo hatutakaa pamoja kutakuwa na struggle zisizoisha tutapigana tu, ujambazi utaongezeka na uuzaji wa madawa ya kulevya. Tukifikiria kuhusu vitu kwamba thamani ya mtu hutokana na vitu alivyonavyo. Ni muhimu thamani ya mtu itokane na yeye alivyoleta mabadiliko katika jamii yake. Tunauwezo wa kupambana na rushwa tukiwa na mtazamo tofauti. Hatutaweza kujenga jamii zetu katika misingi ya uovu.

  Ni aibu kwa kiongozi kuwa mwizi badala ya kuleta mabadiliko katika Taifa lake. Au kufikiri kwamba nafasi ya urais au uongozi mwingine ni nafasi ya umaarufu usio na tija na kufanya anasa. Mtu anayefikiri akipata Urais amepata nafasi ya kufanya anasa ni lazima atapoteza mwelekeo wa uongozi wa Taifa, atajihatarisha mwenyewe na Taifa lake lote.Huwezi kumantain Order katika Taifa kama unapenda starehe. Akili ya kiongozi lazima iwe ''vigilant'' ni muhimu viongozi kujiepusha na starehe za aina zote. Akiendekeza starehe kuna hatari ya watu anaowaongoza kuwa subjects wake badala ya kuwatumikia. Uchumi na maendeleo ya Taifa hili yatakuja tu kama tusipoangalia faida binafsi bali maendeleo yetu kwa pamoja kama Taifa.

  Kutokana na kukosekana kwa uongozi wenye maono sasa hivi na kukosekana kwa maadili kwa vijana waliopo kama hatua dhabiti hazijachukuliwa na kama watu wenye maono na busara hawatapewa nafasi natabiri MUANGUKO wa Taifa hili. Natabiri vita. Na hadi tuje tupate akili itachukua miaka na tutateseka sana. Ni wakati sasa wa kubadili fikra zetu na aina ya maisha tunayoishi. Tufikirie Utaifa na sio ubinafsi.
   
 2. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  naona umeficha fedha kwenye kurasa za kitabu!! hazitaibiwa kwani hawataziona kwasababu vitabu havipendwi na watanzania wengi.
  HAKIKA UMENENA YAMPASAYO KUNENA MTU MWENYE BUSARA!! YOU ARE A GREAT THINKER OF OUR TIMES.
   
 3. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Thanx brother. Mungu awe pamoja nawe.
   
 4. T

  Temporary New Member

  #4
  Nov 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It is him who hold wisdom on his Hand. It is him who direct the ways of men. What a gift you can give to humanity than wisdom? isn't true that ignorance and foolishness brings into humanity destruction? But wisdom heals and restore the bones of men to healthy condition. By wisdom people build their nations and maintain their progress. Wisdom is the source of joy and happiness but foolishness is the source of sorrow. Oh people come and see the light of wisdom so that you may live. The greatness of wisdom you can not measure but fools ignore wisdom until destruction come upon them. If we value wisdom as much as we value Gold and silver, then we can be healed and our country, our economy and our progress restored and maintained. Our eyes must be on this country. We must put all of our attention on this Nation. if we want to progress. This needs change of mind and hearts. We can inspire each other to build this Nation and to love our country. My brother Good thoughts are food for the soul & patriotism is the love of your own nation, that deep desire to see your country move forward.
   
 5. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #5
  Nov 17, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180

  thanks you.
   
Loading...