Pakistan yawasaidia Taliban

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,092
10,780
VITA DHIDI YA UGAIDI YACHAKACHUKA
Hali ya vita dhidi ya ugaidi sasa si shwari tena.Mambo yanazidi kwenda kombo kwa Marekani,ni wakati wa kutafuta kisingizio na kukimbia kabla haijaumbuka zaidi.
Hii ni kufuatia maandishi ya siri za kivita kuvujishwa hadharani na mtandao wa wikileaks.Kwa upande mwengine mpiganaji maarufu wa Taliban bwana Gulbudin Hekmatyar anasema sababu za Marekani kuingia Afghanistan si shambulio la sept.11.
Katika moja ya maandiko hayo ya siri yapatayo 90,000 Marekani imetajwa kulalamika kuwa maaskari wa Pakistan ndio wanaowasaidia Taliban pamoja na kwamba wanalipwa maelfu ya Dola ili kufanikisha kuwakamata hai au wamekufa.
Ndio maana zipo sababu za kutilia shaka shambulio la Uganda siku ya fainali ya kombe la dunia.Raisi Museveni wa Uganda tayari kapanda kichaa ati ataongeza jeshi lake somalia na kuwamaliza Al shabaab.Hajui kwamba anachezeshwa kwata lisilomuhusu.
 
nyoosha thread yako ktk mtiririko utaoleta maana kwani kichwa cha habari hakihusiani na maudhui, kutoka pakistan kuisaidia taliban mapaka museveni kupambana na al shabab, relation?
 
nyoosha thread yako ktk mtiririko utaoleta maana kwani kichwa cha habari hakihusiani na maudhui, kutoka pakistan kuisaidia taliban mapaka museveni kupambana na al shabab, relation?
Yote ni kitu kimoja;vita dhidi ya ugaidi na kupambana na magaidi.Mwanzo ilikuwa ni Palestina katika mashariki ya kati,ikaingizwa Asia na sasa wahusika wakuu wanaileta Afrika.
 
Ni habari nzuri kwani inahusu maisha halisi ya wanaoua watu wasio na hatia na harakati zote za Marekani kule Afghanstan.

Ni habari nzuri kwani inaonesha ni kiasi gani watu wanauawa na ni operation gani za siri zinaendeshwa ndani ya nchi hiyo ilioanza kubomolewa mwaka 2001.

Ila mleta mada ungeweka kichwa kinachosema kwamba TAARIFA ZA SIRI ZA KIJESHI ZA MAREKANI ZATOLEWA HADHARANI BILA IDHINI.
 
Yote ni kitu kimoja;vita dhidi ya ugaidi na kupambana na magaidi.Mwanzo ilikuwa ni Palestina katika mashariki ya kati,ikaingizwa Asia na sasa wahusika wakuu wanaileta Afrika.

mkuu bado wito wa kutaka unyooshe uko pale pale. Issue za palestina zinaingiaje hapa? palestina ni issues za urithi hakuna ugaidi wowote pale. kama ni ugaidi ni Hamas
 
huyu AMI si mjomba wake MS siku zote vitu vyao vinafanana hasa kwa kunakili na kuandika vitu wasivyotafiti na propaganda za kiaarabu, tena ami ati utukome hapa jukwaani.
 
huyu AMI si mjomba wake MS siku zote vitu vyao vinafanana hasa kwa kunakili na kuandika vitu wasivyotafiti na propaganda za kiaarabu, tena ami ati utukome hapa jukwaani.
Wewe kwani unawawakilisha akina nani hapa jukwaani.Ukiingia pahala kama hapa huwezi kutukosa watu kama sisi,akina AMI.
Hapo kwenye thread yangu paste ni kidogo sana kuliko mambo yaliyofanyiwa utafiti yaliyoambatishwa.
Ikiwa hujatoshesheka msikilize bosi wa WIKILEAKS uone habari zake kuhusu Kenya.Bado tu utakuwa na shaka na mimi?.
 
Ni habari nzuri kwani inahusu maisha halisi ya wanaoua watu wasio na hatia na harakati zote za Marekani kule Afghanstan.

Ni habari nzuri kwani inaonesha ni kiasi gani watu wanauawa na ni operation gani za siri zinaendeshwa ndani ya nchi hiyo ilioanza kubomolewa mwaka 2001.

Ila mleta mada ungeweka kichwa kinachosema kwamba TAARIFA ZA SIRI ZA KIJESHI ZA MAREKANI ZATOLEWA HADHARANI BILA IDHINI.

Bila idhini ya nani??
 
Back
Top Bottom