Pakacha lazidi kuvuja: Trilioni 3/- zapotea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pakacha lazidi kuvuja: Trilioni 3/- zapotea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Blood Hurricane, Jul 3, 2012.

 1. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  WAKATI Serikali ikithibitisha uwezo wa kukusanya takriban Sh. trilioni nane kutoka vyanzo vya ndani vya mapato katika miezi 12 kuanzia wiki ijayo, uchambuzi wa misamaha ya kodi nchini unaonyesha kuwa takriban Sh. trilioni tatu zimekuwa zikipotea kutokana na biashara za kimataifa, pamoja na uzembe katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, Raia Mwema limeelezwa.

  Katika mchanganuo huo ambao pia umezungumziwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye pia ni Mbunge, James Mbatia, taasisi ya Aga Khan inayoendesha baadhi ya huduma za kijamii, zikiwamo hospitali, nayo imetajwa kuhusika katika kundi la NGOs zinazokwepa kulipa kodi kwa kiwango kinachostahili.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Mbatia, bungeni, wakati akichangia mjadala wa bajeti kuu ya Serikali, wiki iliyopita, takriban Sh bilioni 7.5 zinapotea kupitia kundi hilo la NGOs.

  Katika maelezo yake bungeni, Mbatia aliishambulia taasisi ya Aga Khan inayoendesha huduma za hospitali kwa gharama kubwa nchini wakati ikiwa inapata misamaha ya kodi nchini. Aga Khan pia inaendesha huduma za ukumbi kwa ajili ya shughuli mbalimbali nchini, ukiwamo ukumbi wa Diamond Jubilee, ulipo jijini Dar es Salaam.

  Huduma hiyo (ya ukumbi), kwa mujibu wa Mbatia, imekuwa ikitozwa gharama za juu bila kujali kuwa taasisi hiyo imekuwa ikipata misamaha ya kodi.

  Pamoja na mchango wa Mbatia bungeni, Raia Mwema limepata nyaraka inayoonyesha namna baadhi ya sekta nchini zinavyovujisha mapato ambayo yangeweza kuchangia bajeti ya nchi na hatimaye kupunguza kiwango cha utegemezi kutoka kwa wahisani wa nje ya nchi.
  Biashara za kimataifa
  Katika eneo la biashara za kimataifa, takwimu zilizopo ambazo baadhi ni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonyesha kuwa, upotevu wa mapato umekuwa ukiongezeka kutoka jumla ya Sh. bilioni 359 mwaka 2006 na 2007 hadi Sh. bilioni 616.5 kati ya mwaka jana hadi Februari mwaka huu.

  Taasisi za Serikali kati ya mwaka 2011 hadi mwanzoni mwa mwaka huu zilikuwa zimesababisha ukosefu wa mapato kwa kiwango cha Sh. bilioni 5.184, wakati mashirika ya umma yakisababisha upotevu wa Sh. bilioni 5.153.

  Aidha, kupitia eneo hilo hilo la Idara ya Forodha kwa upande wa Biashara za Kimataifa, takwimu zinaonyesha kuwa baadhi ya taasisi za kidini nazo zimo kwenye ufujaji wa mapato ya nchi, na kati ya mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu, milioni 114 zimepotea huku, Sh. bilioni 7.5 zilizopaswa kukusanywa kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) zikiishia katika ‘mifuko' ya wajanja.

  Miradi ya wafadhili nayo imekuwa sehemu ya upotevu wa mapato makubwa ya Serikali na katika kiwango cha jumla cha upotevu wa Sh. trilioni tatu, miradi inayofadhiliwa na nchi wahisani, ujanja umefanyika na upotevu wa Sh. bilioni 170 kati ya kipindi kisichozidi miaka miwili, kati ya mwaka huu na mwaka jana.

  Uchochoro mwingine wa upotevu wa mapato ni baadhi ya ofisi za balozi za nchi mbalimbali zilizopo nchini na katika eneo hili, Sh. bilioni 4. 62 zilizopaswa kukusanywa zimeliwa na mafisadi.
  Bidhaa mbalimbali zinazoagizwa na kuingizwa katika majeshi ya ulinzi na usalama, ambako huku kumekuwa na maduka maalumu ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wanajeshi, nako imebainika kuwa takriban milioni 885 hazijakusanywa.

  Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwenye majeshi, katika eneo linalohusu bidhaa za kimataifa zinazoingiwa na kampuni au watu binafsi nchini takriban Sh. bilioni 150.2 ‘zimeliwa.'

  Sekta ya madini ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na watu wa kada mbalimbali nchini nayo imepoteza mapato ya Sh. bilioni 92.7, wakati kituo cha uwekezaji nchini kikifanikisha upotevu wa Sh bilioni 179.8.

  Idara ya Mapato ya Ndani
  Mchanganuo huo wa upotevu wa mapato pia unahusisha eneo la Idara ya Mapato ya Ndani na takwimu zikionyesha kuwa eneo hili limepoteza takriban Sh. trilioni 1.05, ambazo pia zinajumuisha upotevu wa Sh. bilioni 429.2 kutokana na misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

  Chanzo: Raia mwema.
   
Loading...