maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kwa maadili ya kanisa katoliki padri ambaye kwa kawaida hula kiapo cha kujitoa sadaka kwa Mungu, anachukuliwa kama mtumishi wa bwana ambaye hutakiwa kuwa mtiifu na mwaminifu kwa waumini na kwa kanisa.
Kinyume chake, katika kanisa parokia ya Kirumba kuna paroko ambaye ameamua kwa tamaa zake kulitia najisi kanisa kwa kujitwalia mwanamke na kuishi naye kwa siri kinyumba mtaa wa Mwembe Sangara kinyume cha mwenendo, maadili na sheria za kanisa katoliki.
Paroko huyu ambaye imedokezwa kuwa hii ni tabia yake ya muda mrefu tangu huko alikotoka, amekuwa ni kero kwa waumini wake ambao sasa hawana hamu hata ya kusikiliza mahubiri yake, kuungama ama kutubu mbele zake.
Namwomba baba askofu Ruaichi wa jimbo Kuu la Mwanza alichunguze jambo hili na achukue hatua kabla waumini waliochukizwa hawajachukua hatua ambazo zitaliaibisha kanisa.