Pacha azindukia makaburini kabla hajazikwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pacha azindukia makaburini kabla hajazikwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Dec 7, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Tukio la kusikitisha limeibua hofu, simanzi na maswali ya kila aina baada ya kudaiwa madaktari wa hospitali ya Temeke kuruhusu mazishi ya mapacha wawili...kabla ya mmoja wa kuzinduka muda mfupi kabla ya hajazikwa.

  Mtoto huyo, ambaye hadi anataka kuzikwa alikuwa na umri wa siku moja, alishangaza wazikaji baada ya kuonyesha dalili za uhai wakati akiandaliwa kuwekwa kaburini.

  Alikuwa bado anapumua na baadaye akaonyesha kufungua macho, kitendo kilichostua wazikaji na kuamua kumkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Watoto hao mapacha ni walizaliwa na mama aitwaye Aisha Jabir, mkazi wa Mbagala ambaye alipelekwa hospitalini hapo Jumamosi ya juzi kwa ajili ya matibabu.

  Baadaye mama huyo alilazwa na saa 11:00 alfajiri ya jana alijifungua mapacha hao, na inadaiwa kuwa madaktari walisema watoto hao walifia tumboni mwa mama yao kabla ya kuzaliwa.

  "Baada ya kupata maelezo kutoka kwa watalaam wa afya, tulianza kushughulikia taratibu za mazishi na ilipowadiwa saa 3:00 asubuhi, tukaenda chumba cha mochwari na kuchukuwa miili ya watoto na kuelekea Charambe kwa mazishi," alisema mtoa taarifa.

  "Ndugu yangu!!!,katika maisha yangu sijawahi kukutana na tukio la aina hii, tulichimba kaburi moja kwa ajili mazishi yao na tukiwa makaburini tukaanza shughuli za mazishi na baada ya kumweka mtoto mmoja kaburini, tukamfunua wa pili ili tumvishe sanda, kabla ya kumweka shimoni ndipo tukabaini kuwa yu hai." Alisema mtoto huyo alipofunuliwa alionekana anapumua na baada ya kupigwa mwanga wa jua akafumbua macho.

  "Siwezi kusema kilichotea baada ya hapo, isipokuwa tulimkimbiza Hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi huku mmoja ambaye alishafariki dunia akazikwa," alisema. Baada ya kufikishwa Temeke, madaktari waliamua apelekwe Muhimbili kwa matibabu zaidi.


  Chanzo: Alasiri
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Niliposikia mahojiano na wanafamilia... nilijiuliza maswali mengi sana.
  Hivi vifo vya watoto wachanga/ infant mortality rate ambayo huwekwa kwenye takwimu zetu, wahusika huwa wanajiridhisha na sababu za vifo?
  Ni watoto wangapi huzikwa wakiwa hai kwa sababu ya uzembe wa wauguzi/madaktari? Ni watanzania wangapi hujaribu kufungua mashtaka inapotokea hali kama hii?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Angekuwapo Yesu karibu hapo angesemwa kamfufua, na yeye angekubali miujiko.
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Unmeritorious, mental encapsulated unimpromptu fatuous kooky and imbecilic preposterious idea of absolute nothingness thickheaded asinine oafish.
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Vera,

  Hili ni zaidi kwa watoto. Lakini hata watu wazima kibao wanazikwa kabla ya siku zao kwa sababu hatuna jinsi ya kuhakikisha vifo.
   
 6. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dah ! wakubwa wa mjengo wa tiba hapo temeke inakuwaje tena mbona hii inataka kuwachafulia wakati tunawajua mko safi sio kama wale wa mwananyamala ingawa na nyie mh! lakini poa tunaomba ufafanuzi wa hili
   
Loading...