PAC yaendelea kugundua madudu TRL

PAC yaendelea kugundua madudu TRL

EMMA1

Member
Joined
Jan 4, 2015
Posts
39
Reaction score
11
Kamati ya bunge hesabu za serikali imeagiza CAG kufanya ukaguzi maalum wa mchakato wa ubinafsishaji wa shirika la Reli.

Kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za serikali PAC imefanya ukaguzi wa madaraja ya reli ya kati na kuagiza mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi maaluma wa mchakato wa ubinafsishaji washirika la reli kufuatia malalamik o ya baadhi ya mali zilizokuwa za serikali zikiwemo nyumba zimeuzwa kinyemela bila kufuata utaratibu. Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za serikali Zitto Kabwe ameyasema hayo wakati wakifanya ukaguzi wa ujenzi wadaraja la reli kwa kutumia kiberenge kati ya kilosa na mzangaza wilayani Kilosa mkoani Morogoror ambapo amesema kamati imebanini baadhi ya mali nyingi zimepotea bila utaratibu wakati waubinafsishaji.

Aidha Zito amesema kamati imeshangazwa na mpango wa TRL kuzuia wanaosafirisha mizigo kupitia reli kutokuruhusiwa kubeba mizigo ya watu wengine jambo ambalo amesema sio sahihi na mabehewa kurudi tupu yanapotoka mikoani wameshauriana na kuona ili shirika la reli liweze kukua haraka wanahitaji kufanya uwekezaji wakutosha katika reli.

Kwa kampuni hodhi shirika la usimamizi wa reli rahco wamesema wanahitaji trilion 1.5 kwa miaka mitatu kila mwaka wanahitaji bilion 500 ili kuimarisha miundombinu ya reli na kuomba serikali kutenga bujeti ya kutosha kwani kwa sasa wanapata kiasi shilingi bilioni kumi tu kwa mwaka na safari za treli zinafanyika mara mbili kwa wiki.
 
Kila kona shida ni ni balaa kwenye
 
Hivi kwa nini makosa mengi ya nchi hii yanafumbuliwa na Zito ni kwamba wengine hawayaoni au????
 
Bila shaka wale matajiri walioshika nchi na wana magari ya kubebea mizigo lazima washinikize hili bila kujali hasara inayopata TRL na wananchi kwa ujumla. hii nchi kizunguzungu.

Aidha Zito amesema kamati imeshangazwa na mpango wa TRL kuzuia wanaosafirisha mizigo kupitia reli kutokuruhusiwa kubeba mizigo ya watu wengine jambo ambalo amesema sio sahihi na mabehewa kurudi tupu yanapotoka mikoani
 
Wale wahindi wamekomba vyuma vyote vilivyokuwepo hapa nchini kuna zile gari moshi yaliyokuwa yanatumia kuni kujiendesha matanki ya chuma yote yalibebwa kupelekwa india na kupata chuma cha pua ambacho kwa sasa kupatikana nyumba wameuza magenge yote wameua ambayo yalikuwa yanasaidia sana kuangalia reli na kufanya ukarabati,TRC lilikuwa sherika linafanya kazi vizuri mabehewa ya uganda yalikuwa yanakuja huku tanganyika kubeba mizigo na kwenda uganda lakini sasa hivi hawaji tena huku wanaenda mombasa,ukipita stastion mbalimbali utatamani wajerumani waje waendelee na reli yao
 
Kamati ya bunge hesabu za serikali imeagiza CAG kufanya ukaguzi maalum wa mchakato wa ubinafsishaji wa shirika la Reli.

Kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za serikali PAC imefanya ukaguzi wa madaraja ya reli ya kati na kuagiza mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi maaluma wa mchakato wa ubinafsishaji washirika la reli kufuatia malalamik o ya baadhi ya mali zilizokuwa za serikali zikiwemo nyumba zimeuzwa kinyemela bila kufuata utaratibu. Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge hesabu za serikali Zitto Kabwe ameyasema hayo wakati wakifanya ukaguzi wa ujenzi wadaraja la reli kwa kutumia kiberenge kati ya kilosa na mzangaza wilayani Kilosa mkoani Morogoror ambapo amesema kamati imebanini baadhi ya mali nyingi zimepotea bila utaratibu wakati waubinafsishaji.

Aidha Zito amesema kamati imeshangazwa na mpango wa TRL kuzuia wanaosafirisha mizigo kupitia reli kutokuruhusiwa kubeba mizigo ya watu wengine jambo ambalo amesema sio sahihi na mabehewa kurudi tupu yanapotoka mikoani wameshauriana na kuona ili shirika la reli liweze kukua haraka wanahitaji kufanya uwekezaji wakutosha katika reli.

Kwa kampuni hodhi shirika la usimamizi wa reli rahco wamesema wanahitaji trilion 1.5 kwa miaka mitatu kila mwaka wanahitaji bilion 500 ili kuimarisha miundombinu ya reli na kuomba serikali kutenga bujeti ya kutosha kwani kwa sasa wanapata kiasi shilingi bilioni kumi tu kwa mwaka na safari za treli zinafanyika mara mbili kwa wiki.

Kipindi hicho cha ubinafishaji bingwa wa kuachia ngazi ndo alikuwa waziri husika
 
Hivi kwa nini makosa mengi ya nchi hii yanafumbuliwa na Zito ni kwamba wengine hawayaoni au????

Mh.Zitto ni mwenyekiti wa PAC na ndiye mnenaji wa PAC, Makamu wake ni mh.D.Filikunjombe. Kamati hiyo ina wajumbe 22. Kati yao wajumbe 19 ni wabunge wa CCM.

PAC inafanyakazi kama timu. Pia ni miongoni mwa kamati zenye wajumbe wazalendo kweli kweli.

Ila pamoja na hayo niliyoyaandika, uongozi wa kamati unachangia sana uwajibikaji wa kamati husika, mathalan, usitegemee kamati yoyote chini ya mh.Lowassa,ama A. L. Mrema inaweza kuonesha vionjo vya uzalendo. kamati ya namna hiyo inakuwa imekosa MORAL AUTHORITY.
 
Ungesema Zitto ni kichwa ukaishia hapo ungeeleweka tu. Unapoanza kuwaingiza akina Mbowe unaonekana uko emotional na chuki binfsi

Ur right, kama ingebidi basi angezungumzia udhaifu wa .... badala ya watu ambao wala hawako madarakani kiserikali.
 
Huyu Zitto anafahamu gharama za special audit, au yeye anaangalia mijisifa yake tu... waTanzania wanatakiwa kujua audit za vitu vilivyopita miaka kibao havi-add value kwa wananchi ni matumizi mabaya au ufisadi wa Madaraka... Kwanza auditor wenyewe wataishia kusema hatujaona nyaraka x, y, z... let think carefully... wanasiasa vijana wazuri lakini pia wana-mihemuko ya ki....
 
Last edited by a moderator:
Ungesema Zitto ni kichwa ukaishia hapo ungeeleweka tu. Unapoanza kuwaingiza akina Mbowe unaonekana uko emotional na chuki binfsi
mkuu nimekuelewa vizuri ila kiukweli kabisa ugomvi wa mbowe na Zitto ni madaraka tu. na sioni sababu ya msingi kuanza kumtafutia fitna wakati wote kwa 100% wameshiriki kukijenga chama. huwezi kuubeza mchango wa Zitto kwa chadema kama ilivyo kwa slaa na mbpwe pamoja na kuwa wamemzidi umri.
ndo maana nikaweka wazi kuwa fitna zote hizi juu ya Zitto ni mbowe na misukule yake kama lema, pengine wanatamani hata angemfuata chacha wangwe huko alipo.
 
kama ulivyo abunuas. mada inahusu cag ambaye ni mtumishi wa serikali na mahesabu ni ya trl ambayo iko chini ya serikali. sasa unapoingiza mbowe na hao wengine inamaana hujielewi. kwani mbowe ni waziri au naibu wa usafirishaji?au yeye anahusika vipi na madudu ya trl? gt hapishi mada bali anachangia mada kwa hoja mujarabu
 
Huyu Zitto anafahamu gharama za special audit, au yeye anaangalia mijisifa yake tu... waTanzania wanatakiwa kujua audit za vitu vilivyopita miaka kibao havi-add value kwa wananchi ni matumizi mabaya au ufisadi wa Madaraka... Kwanza auditor wenyewe wataishia kusema hatujaona nyaraka x, y, z... let think carefully... wanasiasa vijana wazuri lakini pia wana-mihemuko ya ki....

hivi trc haina internal auditor?
 
Umeendika shudu ...shudu....!!!!!!!
Kama hujaelewa mada ni mara 10000 zaidi kukaa kimya .kusoma Ya wenzako na kujifunza pia..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom