OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,091
- 114,642
Sitakuwa na maneno mengi, napenda nijikite kwenye hoja na facts. PAC ni kamati ya kibunge yenye jukumu zito la kulisaidia bunge kusimamia serikali katika matumizi ya pesa za umma hususani serikali kuu na mashirika ya umma. Kutokana na unyeti wa kamati umewekwa utaratibu wa kuwa na mwenyekiti kutoka vyama pinzani ili kufanya chama tawala kiwajibike ipasavyo. Ikumbuke kwamba katika bunge la 10 kamati hii ilikuwa chini ya Zitto Kabwe kabla hajavuliwa uanachama na Chadema kwa kile kilichoitwa usaliti.
Zitto Kabwe amerudi tena bungeni kupitia chama cha ACT. Na ni wazi kuwa ameomba kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hii ama nyinginezo. Hoja ya msingi ni kuwa kwa yaliyojiri bunge la 10 na yanayoendelea kujili mapema baada ya Magufuli kushika dola basi Zitto Kabwe anapungukiwa uadilifu na alishindwa kulisaidia bunge kama mwenyekiti wa PAC. Imewekwa wazi kuwa TRA, TPA na Shirika la Reli ambayo ni mashirika ya umma yamehujumu uchumi kwa kiasi kikubwa sana. Aidha ufisadi iliogundulika TRA mpaka kupelekea kusimamishwa kazi kwa Ndugu Bade unazidi kutia mashaka uadilifu wa Zitto. Ikumbukwe kwamba Zitto aliwahi kumsifia Ndugu Bade kwa ''uchapakazi wake'' na hiyo sio ethics. Katika engo nyingine Zitto anatia shaka juu ya uadilifu wake kutokana na haya

- Zitto kupokea tuzo toka NSSF. Katika hali ya kutia mashaka NSSF ilimpatia tuzo Bwn. Zitto Octoba 2014 jambo ambalo kiusimamizi tunaweza sema ni kumfunga mdomo Zitto Kabwe kiasi cha yeye kugeuka kuwa mpiga debe wa NSSF badala ya wanyonge. Kashfa zingine zipo wazi sina haja ya kuzitaka, ikubukwe kuwa Mh.Sugu alimuhusisha Zitto na Leka Lutigite kupokea mkwanja NSSF
- Katika bunge la 10 Mh.Zitto alituhumiwa na Mh.Lusinde kupokea 10m toka kwa Mafisadi wa ESCROW
- Usaliti ndani ya chama chake cha zamani CHADEMA akihusishwa na kuhujumu chama chake.