This is not rocket science...
Kama wananchi wenyewe wanaishi kwene nyumba za udongo na kuezekwa kwa nyasi, sidhani kama utapata darasa lenye hadhi ya juu ktk maeneno hayo.
Kama serikali haina fedha za kutosha, ni ndoto vilevile kuwa na miundombinu murua ya kielimu.
Kama raia wenyewe ni dhaifu, kifikra na kimwili, ni wazi hawaezi kustushwa na mazingira mabovu yanayowazunguka.
Kama una serikali dhaifu, isiyo na mipango, isiyowajibika, yenye 'thinkers' dhaifu..well u can expect everything to go wrong.
Kama hakuna vifaa vya ujenzi maeneo husika (?) lol..
Sasa swali bado nauliza ..which is which..hapo mwene makosa zaidi ni nani?
Ni rocket science kwa watu wa dunia ya tatu. Kama ulibahatika kuangalia 'state of union' Obama alieleza kwa kirefu sana tatizo la elimu kwa marekani, kupungua kwa ufaulu, umasikini unaotokana na elimu na ushindani kutoka nchi za Asia. Akaeleza mipango ya kuinua elimu kwa miaka 25 ijayo akitoa namba na mipango kamili kwa kuanisha nini kianze na kipi kifuate na kumalizia. Hiyo ni marekani yenye uwezo mkubwa sana lakini bado wanaamini kumkomboa mmarekani ni kwa njia ya elimu na si vinginevyo. Obama amepingwa kwa mambo mengi lakini hili la elimu si republican au tea party wote kimya.
Angalia nchini mwetu, zaidi ya kusomewa tarakimu bungeni kuna mipango gani endelevu ya kutoa elimu bora na kwa muda gani(vision)? jibu ni hakuna. Jiulize utajengaje madarasa na kujivuna umeinua elimu kama wanafunzi wanashinda madarsani wakitongozana, kama shule hazina vitabu n.k. Kama kungeuwa na vision walimu wangeanza kuandaliwa miaka 10 kabla ya mpango ili wakati ukifika kila kitu kipo tayari.
Leo kuna wanafunzi wengi hawaendi high school kwasababu idadi imekuwa kubwa kuliko, hapo kuna vision.!
Lakini jiulize kwanini ujenzi wa madarasa umekuwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi na baada ya hapo kimya? Je wanafunzi hapo pichani juu wamekosa madarsa kwasababu eneo lao halina wapiga kura au.!
Ukitaka kumuondoa mtu kwenye nyumba za nyasi mpe elimu. Nilikotoka nyumba za nyasi ni nadra kwasababu kuna aliyewaonyesha kuwa elimu ni ukombozi hata kama huna rasilimali za kutosha, tena kwetu ardhi ni ugomvi. Kwahiyo hao wananchi wa masasi hawatatoka katika nyumba na madarasa ya majani kwasababu wamesusiwa kimipango au kuhamasishwa ili wajiletee elimu.Wanahamasishwa kujenga ofisi za chama na kata.
Unaposema serikali haina pesa,inabidi nicheke kidogo. Inapata wapi pesa za kujenga nyumba za wabunge Dodoma na ofisi huko majimboni?
Inapata wapi pesa za kuunda tume tusizojua matokeo yake? inapata wapi pesa za kulipa richmond milioni 150 kwa siku bila kufua umeme? Inapata wapi utayari wa kulipa bilioni 100 Dowans? Inapata wapi pesa za kununua ndege ya rais huku waziri mkuu wa uingereza akisafiri na commercial airline? inapata wapi pesa za kuwalipa watu 320 wanunue mashangingi yenye thamamani ya millioni 200 kila moja? yaani shangingi 1 linaweza kujenga shule 7 zenye thamani ya milioni 30.
Inpata wapi pesa za kuendesha ofisi ya bunge Dodoma na ndogo Dar, waziri mkuu Dodoma na ndogo Dar, Ikulu Dodoma na nyingine Dar, kwa mantiki gani. Inapoteza kiasi gani bila kujua (rejea CAG) ripoti.
Hakuna kitu kinaitwa matatizo ya vifaa vya ujenzi hata siku moja, kama pesa zipo vifaa hivyo vitafika. Nimewahi kwenda milima ya uluguru kileleni na kule upareni kuna shule nzuri sana, nyumba za kuishi nzuri sana n.k.
Serikali kama muundo hauna matatizo, tatizo lipo kwa watendaji wa serikali ambao nathubutu kusema hawajui dira ya maendeleo ya kumkomboa mwananchi. Wao maisha yao ni kufikiri jinsi ya kukwapua na kujenga mahekalu wakiwa na uhakika watoto wao watasoma nje au kwenye shule bora. Wizi wote unaouona ni uchoyo, ubinafsi na roho zisizojali. Watoto wao wanapata nafasi zote za serikalini au bungeni si kwasababu hawana uwezo bali walipata fursa ambayo mtoto wa nanyumbu hakuipata. Na wanajua kuwa njia rahisi ya kumtawala mnanyumbu ni kuwaacha watoto wao kwenye nyasi.
Kama unadhani si kweli nakuomba unipe vision ya elimu Tanzania katika miaka 10 tu ijayo! kama ipo au umeisikia.
Kwa swali lako la mwisho, (1) Serikali inapesa (2)Hakuna kitu kinaitwa uhaba wa vifaa(3)uchoyo na ubinafsi ndio umetamalaki miongoni mwa viongozi (4) Serikali haina vision ya kumsaidia asiyejitambua na hivyo asiyejitambua hajui kuwa hajitambui na hata tambua kwasababu hana mtambuzi.