Out of my league!

saa nyingine ndo yale yale ya 'kusubirishana'.....leo uko out of his/her league, kesho umo ndani.....
Labda ni hisani ya ule mfumo wa premier leagu..msimu huu uko relegated, msimu ujao uko promoted, either way, haileti maana yoyote katika maisha ya kisasa where anyone is someone
 
Thanks gusy ila naona mmebase zaidi kwenye reaction za wanaotongozwa na watongozaji....na inaonekana though sio sahihi ila tumejifunza kukubali kwamba hiyo ndio hali halisi na kuna watu hiyo ni asili yao so we are kinda used to it!!!
Binafsi nilikua naongelea in general....mimi niliwahi kumuona mkaka anamwambia mdada ''anti samahani'' kabla yule dada hata hajajua yule kaka anataka nini akaanza kumporomoshe maneno hayo....''we vipi unataka kuongea na mimi kitu gani....unaona tunafanana wewe''.Imagine kama huyo dada nguo yako ilikua imekaa vibaya huyo kaka akataka kumrekebisha anakua amemkomoa nani?
 
My Dear Lizzy,

Tena wapo wengi sana wa aina hiyo lakini nikwambie tu kitu kuwa "Hayo ni maneno ya mkosaji".

Inakuwa kama hadithi za sungura vile alivyoshindwa kufikia ndizi akasema sizitaki mbichi hizi.

:twitch:Maneno ya mkosaji hata kwa mtu usiyemjua Dearest??
 
Maneno
" . . . mi sio saiz yako" au "mi sio rika lako" au " au " hatuendani kabisa" ni lugha nyingine ya mtu kusema SIHITAJI LOLOTE KUTOKA KWAKO.
Na wakati mwingine hutumia kama njia ya kukupima kujiamini kwako kama upo tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali ktk maisha???
So usiumize kichwa kwa kumtafutia jibu la kejeli au dharau badala yake mpe jibu la kuonyesha HOW WISE YOU ARE

Na pia kukutokea mambo kama haya usione kama ni mkosi fulani ktk maisha yako, bali ni kila mtu anakutana navyo. Jaribu kuona ni namna gani utaweza kupambana na watu wa aina hiyo lakin IN A WISE WAY

Nawakilisha

Kama humuhitaji mtu au kitu kutoka kwake vipi mtu asimwambie hivyo hivyo badala ya kumkejeli au kumwonyesha dharau?
Binafsi kama nna mtu ntajibu siko available na mtu asipoelewa nampotezea!
Kama sihitaji au sitaki ntamjibu hivyo kwamba kwa wakati huu niko bize na mambo yangu kwahiyo sihitaji kua na mtu au sitaki!Atakavyoichukulia ni juu yake.....binafsi nakua nimekua muungwana na hiyo inaniacha na amani!!!

Kuhusu kutumika kama changamoto.....changamoto gani ya kumfanya mtu ajisikie yeye sio??Well I guess wengine wanaweza kusukumwa na hayo maneno kufanya zaidi ila je kama huyo mtu hayuko kwenye nafasi ya kubadilisha hicho unachomdharau nacho....kwa mfano sura , huoni kwamba ataishia kupewa msongo wa mawazo tu?
 
Back
Top Bottom