Otto Warmbier afariki dunia.

Otto Warmbier afariki dunia.

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,805
Otto Warmbier, mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku sita tu baada ya kuachiliwa. Familia yake imetoa lawama dhidi ya kifo hicho katika kile walichokiita unyanyasaji mkali dhidi ya Otto aliokuwa akikabiliana nao alipokuwa mikononi mwa maofisa usalama wa Korea Kaskazini . Akiuelezea utawala wa Korea Kaskazini kama ni wa ukatili mkubwa , Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba Warmbier alikabiliana na mazingira magumu akiwa nchini humo. Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cincinnati. Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wame sema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha ma kubwa ya kuumia neva.

Source: bbcswahili
 
Kwa hili lililo tokea mmarekani anaweza kulipiza kisasi.
 
Apumzike kwa amani...

ila ingependeza ukaweka na picha yake tumuone
 
Halafu kuna baadhi ya wapuuzi wanashabikia Korea Kaskazini

Mkuu pamoja na aliyofanyiwa Dr. Ulimboka lakini bado tunaipenda nchi yetu.
Je unajua wanavyovifanya wao Marekani nyuma ya pazia ambavyo huvioni?
Hata Marekani ukikamatwa kwa kuhisiwa kuwa ni shushushu lazima kwanza uisome namba, kwa hiyo hii haiwezi kufanya overall judgement juu ya Korea.
 
Kiduku the best friend of mine. I hate America from the bottom of my heart. They brought HIV .
 
Back
Top Bottom