Othman Masoud: Jemedari wa kupigania haki

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2010
Posts
2,202
Reaction score
1,229
Othman Masoud: Jemedari wa kupigania haki

Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman,

Na Ahmed Rajab. MSIMAMO wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ni msimamo wa kizalendo, wa kupigiwa mfano na unaofaa kuigwa na wakuu wengine wa Serikali wenye hisia na nchi yao.

Ni nadra siku hizi, hasa nchini mwetu, kuwaona au kuwasikia viongozi wenye vyeo vikubwa kama hicho cha Mwanasheria Mkuu wakijitokeza wazi, tena bila ya woga, kuitetea misimamo inayopingana na ile ya wakubwa wa nchi. Hivyo, Mheshimiwa huyu yuko katika tabaka la wale waliojitolea kuipigania nchi yao.

Huo ndio uzalendo. Tena ni uzalendo wa hali ya juu. Si tu kuwa mtu ana mapenzi na nchi yake lakini pia kuwa ana moyo wa kujitolea kuipigania nchi yake na kuwa tayari kuziondoa, kuziweka upande au kuzipuuza tafauti zozote zilizopo - ziwe za kidini, za kikabila za kichama au za kiitikadi za kisiasa - baina yake na wananchi wenzake. Daima anakuwa anaiweka mbele nchi yake, naliwe liwalo.

Othman Masoud ameudhihirishia ulimwengu na muhimu zaidi amewadhihirishia Wazanzibari wenzake kwamba yeye ni mzalendo wa aina hiyo. Tena ni mtu mwenye kujiamini.

Nafikiri sababu inayomfanya ajiamini ni kuwa anaamini kwa dhati kwamba anaitetea haki. Hataki kuona dhulma inatendeka baina ya nchi mbili zilizo katika Muungano. Hataki kuiona nchi moja inaidhalilisha nyingine.

Huko kujiamini kwake ndiko kunakomfanya asiwe na hata chembe ya woga kwa kuwakwaa wakubwa wenye sera zinazopingana na msimamo wake. Wale wenye kumbeza na waliojitokeza kimbele mbele kumshauri Rais Ali Mohamed Shein amfukuze kazi wamekosea.
Kwa kuuchukua msimamo aliouchukua Othman Masoud ameonyesha kuwa hana ubinafsi. Hayuko tayari kuiuza nchi yake kwa vijipesa viwili vitatu au kwa ulwa wa aina yoyote ile.

Alipokuwa analihutubia kongamano la Baraza la Katiba la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar, Othman hakutafuna maneno, hakujifanya kibogoyo alipoutamka ukweli na wala hakubabaika kwa namna yoyote ile. Sauti yake ilijaa hamasa ya uzalendo wake; aliyaeleza mambo kwa busara na hikma, tena kwa taratibu.

Kwa ufupi aliililia na kuipigania nchi yake. Hamna shaka yoyote kwamba yeye ni jemedari mzuri wa kuipigania ardhi iliyozikiwa kitovu chake. Inafaa tumshukuru Mungu kwani kila uchao anachomoza jemedari mwingine wa kuipigania Zanzibar yetu. Kila mmojawao akili kichwani. Vipi tushindwe kwenye vita hivi?

Othman Masoud anautetea muundo wa Muungano utaokuwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Katiba iliyo chini ya Jaji (Mstaafu) Joseph Warioba.

Pamoja na kuubainisha msimamo wake kuhusu suala la Muungano Mwanasheria huyo Mkuu zaidi aliutumia wadhifa wake na uweledi wake wa mas'ala ya kisheria kutuelimisha Wazanzibari wenzake kuhusu mambo ya Katiba na jinsi Zanzibar inavyopunjwa ikiwa ndani ya Muungano wa serikali mbili kama ulivyo sasa chini ya ule aliouelezea kuwa "ukoloni kasorobo".

Alieleza pia kwamba muundo uliopo wa Muungano ndio wenye hatari ya kuuvunja Muungano kinyume na wanavyofikiria wahafidhina wa CCM/Zanzibar na wale walio Bara wanaotishwa na wahafidhina hao.

Ninaamini kabisa kwamba itikadi halisi ya wahafidhina hao ni kuendelea kuwa na madaraka ili wayatumie madaraka yao kujichumia mali. Huo ndio mkakati wao na hiyo ndiyo hali halisi ilivyo.

Aghalabu watu wenye kuipenda nchi yao na walio tayari kujitolea mhanga kwa sababu ya nchi yao huwa hawawajali hao wahafidhina. Huwa hawawatii maanani. Wanafanya hivyo kwa sababu katika nyakati kama hizi za uwazi na demokrasia watu wa sampuli ya wahafidhina wetu wenye kuonya kuhusu ‘maafa' mara nyingi, kama si zote, huwa ndio wasioisoma vizuri historia. Matokeo yake ni kwamba huishia kutupwa katika debe la taka la historia.

Kwa upande mwingine, watu wa sampuli ya Masoud Othman, hata kama awali watakumbwa na misukosuko, misukosuo hiyo huwa ya mpito tu kwani huishia kubebwa na umma na kushangiriwa kwa ushindi wao kwa sababu daima wanakuwa wanapigania haki.

Chanzo: Zanzibar Daima Online

Wakuu pamoja na yote yanayomkuta Mzalendo huyu wa kweli natamani kuwe na sayari nyingine ambayo watu kama hawa wanaweza kuishi. Historia juu yake imeandikwa.
 
mdomo umeponza kichwa huyu mwanasheria katia aibu sana serikali ya mapinduzi
 
Hii inadhihirisha ni kwa kwango gani "MCHAKATO" huu haukukubali mawazo mbadala mbali na yale yaliyotakiwa na chama tawala. Hebu fikiria mwenyewe ni wajumbe wangapi walikumbwa na vitisho katika upigaji kura ktk BMK. Wakawa waoga kwa kuhofia kufukuzwa kazi kama huyu. Kwa namna hii "uhalali" wa katiba kisiasa na kisheria uko wapi? Mungu tujalie tuondokane na vitisho hivi katika upigaji wa kura!
 
Jemadari wa kupigania haki aliyekimbia uwanja wa vita akarudi wakati watu wameshamaliza kazi ndio akataka kuvuruga kazi nzito iliyofanywa...huyo unathubutu kumwita jemadari?...labda jemadari wa kibanda maiti tu.....vinginevyo alikuwa na fursa lukuki ya kutoa maoni na kulazimisha kamati ya maridhiano ikae lakini hakufanya...anastahili kutimuliwa....sasa chukueni makapi lhalafu mumpe ujemedari tutajkutana kwenye sanduku la kura....
Othman Masoud: Jemedari wa kupigania haki

Mwanasheria Mkuu wa SMZ, Othman Masoud Othman,

Na Ahmed Rajab. MSIMAMO wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, ni msimamo wa kizalendo, wa kupigiwa mfano na unaofaa kuigwa na wakuu wengine wa Serikali wenye hisia na nchi yao.

Ni nadra siku hizi, hasa nchini mwetu, kuwaona au kuwasikia viongozi wenye vyeo vikubwa kama hicho cha Mwanasheria Mkuu wakijitokeza wazi, tena bila ya woga, kuitetea misimamo inayopingana na ile ya wakubwa wa nchi. Hivyo, Mheshimiwa huyu yuko katika tabaka la wale waliojitolea kuipigania nchi yao.

Huo ndio uzalendo. Tena ni uzalendo wa hali ya juu. Si tu kuwa mtu ana mapenzi na nchi yake lakini pia kuwa ana moyo wa kujitolea kuipigania nchi yake na kuwa tayari kuziondoa, kuziweka upande au kuzipuuza tafauti zozote zilizopo - ziwe za kidini, za kikabila za kichama au za kiitikadi za kisiasa - baina yake na wananchi wenzake. Daima anakuwa anaiweka mbele nchi yake, naliwe liwalo.

Othman Masoud ameudhihirishia ulimwengu na muhimu zaidi amewadhihirishia Wazanzibari wenzake kwamba yeye ni mzalendo wa aina hiyo. Tena ni mtu mwenye kujiamini.

Nafikiri sababu inayomfanya ajiamini ni kuwa anaamini kwa dhati kwamba anaitetea haki. Hataki kuona dhulma inatendeka baina ya nchi mbili zilizo katika Muungano. Hataki kuiona nchi moja inaidhalilisha nyingine.

Huko kujiamini kwake ndiko kunakomfanya asiwe na hata chembe ya woga kwa kuwakwaa wakubwa wenye sera zinazopingana na msimamo wake. Wale wenye kumbeza na waliojitokeza kimbele mbele kumshauri Rais Ali Mohamed Shein amfukuze kazi wamekosea.
Kwa kuuchukua msimamo aliouchukua Othman Masoud ameonyesha kuwa hana ubinafsi. Hayuko tayari kuiuza nchi yake kwa vijipesa viwili vitatu au kwa ulwa wa aina yoyote ile.

Alipokuwa analihutubia kongamano la Baraza la Katiba la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar, Othman hakutafuna maneno, hakujifanya kibogoyo alipoutamka ukweli na wala hakubabaika kwa namna yoyote ile. Sauti yake ilijaa hamasa ya uzalendo wake; aliyaeleza mambo kwa busara na hikma, tena kwa taratibu.

Kwa ufupi aliililia na kuipigania nchi yake. Hamna shaka yoyote kwamba yeye ni jemedari mzuri wa kuipigania ardhi iliyozikiwa kitovu chake. Inafaa tumshukuru Mungu kwani kila uchao anachomoza jemedari mwingine wa kuipigania Zanzibar yetu. Kila mmojawao akili kichwani. Vipi tushindwe kwenye vita hivi?

Othman Masoud anautetea muundo wa Muungano utaokuwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Katiba iliyo chini ya Jaji (Mstaafu) Joseph Warioba.

Pamoja na kuubainisha msimamo wake kuhusu suala la Muungano Mwanasheria huyo Mkuu zaidi aliutumia wadhifa wake na uweledi wake wa mas'ala ya kisheria kutuelimisha Wazanzibari wenzake kuhusu mambo ya Katiba na jinsi Zanzibar inavyopunjwa ikiwa ndani ya Muungano wa serikali mbili kama ulivyo sasa chini ya ule aliouelezea kuwa "ukoloni kasorobo".

Alieleza pia kwamba muundo uliopo wa Muungano ndio wenye hatari ya kuuvunja Muungano kinyume na wanavyofikiria wahafidhina wa CCM/Zanzibar na wale walio Bara wanaotishwa na wahafidhina hao.

Ninaamini kabisa kwamba itikadi halisi ya wahafidhina hao ni kuendelea kuwa na madaraka ili wayatumie madaraka yao kujichumia mali. Huo ndio mkakati wao na hiyo ndiyo hali halisi ilivyo.

Aghalabu watu wenye kuipenda nchi yao na walio tayari kujitolea mhanga kwa sababu ya nchi yao huwa hawawajali hao wahafidhina. Huwa hawawatii maanani. Wanafanya hivyo kwa sababu katika nyakati kama hizi za uwazi na demokrasia watu wa sampuli ya wahafidhina wetu wenye kuonya kuhusu ‘maafa' mara nyingi, kama si zote, huwa ndio wasioisoma vizuri historia. Matokeo yake ni kwamba huishia kutupwa katika debe la taka la historia.

Kwa upande mwingine, watu wa sampuli ya Masoud Othman, hata kama awali watakumbwa na misukosuko, misukosuo hiyo huwa ya mpito tu kwani huishia kubebwa na umma na kushangiriwa kwa ushindi wao kwa sababu daima wanakuwa wanapigania haki.

Chanzo: Zanzibar Daima Online

Wakuu pamoja na yote yanayomkuta Mzalendo huyu wa kweli natamani kuwe na sayari nyingine ambayo watu kama hawa wanaweza kuishi. Historia juu yake imeandikwa.
 
Kumbe ha jamii foram kuna wahafidhina wa ccm nilidhani wote ni mapatriotism duuuh tukiendelea kushabikia ushenzi wa awa jamaa hatuta fika mbali!!!!!!
 
- Jemadari alikuwa Mrema tu wengine wote wanafiki tu huyu mbona hakusema mapema kuwa hakubali msimamo wa bosi wake angekuwa shujaaa lakini sivyo alivyofanya ni ujuha mtupu!!

Le Mutuz
 
Mkuu MJINI CHAI huyu OTHMAN MASOUD NI MZALENDO NA SHUJAA , MPAKA SASA HUYU ANAMFUATIA MAREHEMU KARUME KWA USHUJAA .
 
angepelekewa na mikataba ya madini,werema anaogopa kwenda Kuchunga mifugo huko kongoto
 
Si halmashauri ya Wilaya yangu imuchukue kusimamia Haki na Sheria Ndogondogo, NYOTA HII HAIPASWI KUZIMA HATA SEKUNDE MOJA
 
- Jemadari alikuwa Mrema tu wengine wote wanafiki tu huyu mbona hakusema mapema kuwa hakubali msimamo wa bosi wake angekuwa shujaaa lakini sivyo alivyofanya ni ujuha mtupu!!

Le Mutuz

[MENTION]Le Mutuz[/MENTION]...angetolea wapi maoni hayo wakati mumetawaliwa na zomea zomea.....?mnavutiwa sana na kauli za "ndiyooooo..." basi hamtaki kusikia tofauti.kwangu nadhani alitumia busara ya hali ya juu kwa kutoa maoni yake kupitia kura yake.....kushindwa au kushinda ni matokea lkn jamii nzima inajua msimamo wake....Huyu ni shujaa!
 
juha ni wewe KJ usiyeweza kuelewa chochote.

- Jemadari alikuwa Mrema tu wengine wote wanafiki tu huyu mbona hakusema mapema kuwa hakubali msimamo wa bosi wake angekuwa shujaaa lakini sivyo alivyofanya ni ujuha mtupu!!

Le Mutuz
 
Kwa ujumla hicho chanzo cha habari ni cha muda mrefu kidogo..........lakini kila ukisoma unaona taswira ya uzalendo alionao mzalendo Othman Masoud Othman..............Ukichangan ya na bandiko la Pasco Plus video crip..........aaah utajua namaanisha nini......! Mzimu huu utawamaliza wengi..............! kila anajegusa muungano ''yanampata''..............kun a nini hapa..............?
 
Last edited by a moderator:
- Jemadari alikuwa Mrema tu wengine wote wanafiki tu huyu mbona hakusema mapema kuwa hakubali msimamo wa bosi wake angekuwa shujaaa lakini sivyo alivyofanya ni ujuha mtupu!!

Le Mutuz
Mkuu mpaka leo bado hujamjua mrema tu.......wengi ambao hawakumjua walikuwa na mategemeo juu yake ya kuwa atakuwa mzalendo wa kweli lakini baada ya kujua ya kuwa ni Mganga njaa (msaka tonge) watu walimkimbia na mpaka leo amebaki hivyo.........wewe hili hulijui mkuu......?
 
Back
Top Bottom