Orodha ya majina wanaotakiwa kusahihisha maombi ya mkopo 2019/2020

Alphaking2023

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,093
2,121
ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020
HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019 ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa..

Hatua ya HESLBinafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.

Orodha hii ni ya wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo ya Shahada ya kwanza. Orodha ya waombaji mikopo watakaojiunga na Shule ya Sheria (Law School of Tanzania), Shahada za Uzamili na Uzamivu itatolewa kesho Jumatatu tarehe 30 Septemba 2019.

Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika *bofya hapa.*

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
29 Septemba 2019
 
Uli upload kikiwa kimeshapigwa muhuri?
Hata mimi hapo ndo naona kuna tatizo, maana kwenye ku upload mtu unaweka cheti original kisichokuwa na muhuri halafu kwenye kutuma posta ndo unatuma chenye muhuri

Naona walikuwa wanataka chenye muhuri ndo cha kuupload
 
Utaratibu ilikua ni kwamba unahakiki cheti RITA baada ya hapo ndo unaanza taratibu za ku apply mkopo. Hii inamaanisha kua wakati una upload cheti uta upload kile kilichohakikiwa sio original yani scanned copy of your certified birth certificate.
 
Natatizo ndo liko hapo

Una upload kilichokuwa verified na RITA
 
Hata mimi hapo ndo naona kuna tatizo, maana kwenye ku upload mtu unaweka cheti original kisichokuwa na muhuri halafu kwenye kutuma posta ndo unatuma chenye muhuri

Naona walikuwa wanataka chenye muhuri ndo cha kuupload

kama uliaplod kisichokuwa certified hilo ndo kosa lako,
 
Wasomi wetu sijui wanafeli wapi! yaani mtu anatuma maombi bila kufuata maelekezo, wengine hawakusaini maombi yao, wengine hawakebandika picha zao wala za wadhamini, wengine hawakupeleka mahamani kusainiwa fomu zao, wengine hawakuverify cheti cha kuzaliwa RITA, wengine nakala za vyeti hazisomeki lakini wakatuma tu hivyo hivyo nk. Kwa kweli vijana wetu wanatia aibu.
 
HV UKISHAFANYA HAYO MAREKEBISHO

JE UNA KUSANYA KITABU KIZIMA KAMA MWANZO UNATUMA KUPITIA SANDUKU LA POSTA AU UNAFANYA MAREKEBISHO KWENYE KIPENGELE HUSIKA ULICHO AMBIWA HALAFU UNATUMA ONLINE...???
 
Back
Top Bottom