Optatus Fwema , Mchora katuni aliyezuiliwa Rumande aachiwa kwa dhamana

Mkuu wangu Tate Mkuu hebu vuta pumzi kwa nguvu uupe ubongo utulivu....🀣

Kwani ile picha haina DHIHAKA NA KEDI yoyote ile?!!
Ongea ukweli komredi wangu....
Yaani inawabidi watawala wetu pamoja na polisi, wafikie sehemu wapuuzi baadhi ya hivi vitu vidogo vidogo na ambavyo havina tija, wala athari zozote zile kwenye jamii.

Mfano ni hizo katuni, jogging ya Bawacha, nk! Yaani havina athari yoyote ile. Kwa mfano hizo katuni, ni watu wachache sana huvutiwa kuzisoma na kuelewa!

Kwa nini zisipuuzwe tu! Kama Magufuli na ubabe wake wote ule, alichagua kuzipuuza! Maana alikua anafahamu fika namna anavyo chorwa!! Chifu Hangaya anashindwa wapi?
 
Sawa mkuu....ndio sanaa ilivyo....

Kinachogomba ni hiki.....

Ukiiangalia ile sanaa ya ndugu yetu unapata tafsiri nyingi mno....mathalani:-

1)Wako walio na mamlaka/uamuzi zaidi ya "kiongozi"....
2)Kiongozi "yupoyupo tu"...

Sasa yote hayo.....msanii ana ushahidi pasi na Shaka?!!

Ana "yakini" isiyo na shaka?!!!

Maswali mengi anaweza akaulizwa na akaishia kujibu tu kuwa ni "HISIA" bila ya "UHALISIA"....

HESHIMA NI KITU CHA BURE MKUU...

HII NI AFRIKA.....

Wenzetu wa nje...hukohuko TUNAKOIGA ULIBERALI ULIOPITILIZA.....walishawahi kuwachora vibaya mpaka MANABII NA MITUME wanaoheshimiwa na DINI zao....gharama yake kila mtu anaijua......
 
Mkuu wangu Tate Mkuu....

Unaweza kunikumbusha ni katuni gani hayati Magufuli ALISHAWAHI KUCHORWA ikiwa na UJUMBE "aila" ya huo wa ndugu yetu??!!
 
Mkuu wangu Tate Mkuu....

Unaweza kunikumbusha ni katuni gani hayati Magufuli ALISHAWAHI KUCHORWA ikiwa na UJUMBE "aila" ya huo wa ndugu yetu??!!
Kipanya alimchora sana Hayati enzi za uhai wake! Akiwa na bichwa lenye kome kubwa! Kiasi mpaka baadhi ya wadau tulihofia labda angekamatwa! Lakini wapi.

Kuna siku Hayati mwenyewe akawatahadhalisha kwa utani kuacha kumchora mbaya kupitiliza! Sema ndiyo hivyo tena, sina utaalam wa kuweka hizo katuni humi jukwaani.
 
Ni hivi , huyu Jumbe Brown anataka watu wote waishi kama anavyotaka yeye , hili jambo halitawezekana kamwe
😳😳
Hapana.....

Hapanaaaaaaa......

Hapana mkuu RBC ...

Siwezi kutaka watu waishi kama mimi!!

Siwezi.....

Ila......

Hivi kukumbushana kuwa fulani alikosea alipotoa DHIHAKA NA KEDI iliyopitiliza ni kosa?!!!!

Hivi ile sanaa iko sawa kabisa kwetu Watanzania....Waafrika?!!!

Hivi tumefikia kiwango kikubwa cha uliberali uliopitiliza wanaoishi wenzetu ughaibuni?!!!

Hivi ndio uhuru huo "kumdhalilisha kiongozi"?!!!

Tunauhitaji huo uhuru wa KUDHALILISHANA HIVYO?!!

Hivi kusema "fulani" anaendeshwa kwa "rimoti" na mtu baki....mtu baki kabisa ni Sawa kwako?!!

Si HISIA?!!.

Kuna USHAHIDI?!!!

Mtu anaweza kuutoa MAHAKAMANI?!!!!Khaaa 😳 😳

Ninaamini hujakuja KUTETEA na silaha ya "OBSCURANTISM"......

#SiempreJMT
 
Mkuu wangu Nyboma...huwenda kweli "nimesherehesha" kusema AMETUKANA....ila ukiiangalia ile picha inatoa tafsiri nyingi mno za KEDI NA DHIHAKA....nakosea komredi?!!!
Vipi kile kibonzo cha Masoud Kipanya hakikuwa na dhihaka ndani yake? Why huyu na si Kipanya? Ama neno KIWETE ndio limeleta sintofahamu?
 
Hivi Jumbe Brown nani kakwambia ile cartoon ni kiongozi wetu ?!. Mchoraji yeyote akichora huchora kiongozi wetu ?
 
Kuna jambo linashangaza na kustusha sana.
Uhuru wa kujieleza ama kutoa maoni unaopigiwa kelele na vyombo vya habari unahusu maslahi yao yanapoguswa.

Tangu kukamatwa, kuachiwa kwa dhamana na kushtakiwa kwa msanii Optatus Fwema hakuna chombo cha habari kilichoripoti jambo hilo.

Vyombo vya habari huripoti mwenendo wa kesi zinazoendelea mahakamani lakini vimekwepa kutoa taarifa kwa umma muendelezo wa hii kesi. Nakumbuka nmna wahariri walivyodhibiti utoaji wa taarifa za ukamatwaji na kunyimwa dhamana kwa Oppter.

Wachora vibonzo wanajipanga kuhusu mahusiano yao na mwenendo wa media houses za Tanzania
 
Kesi dhidi ya Optatus Fwema inaendelea mahakama ya hakimu Mkazi Kinondoni.

Upande wa Mashtaka hadi sasa umeshindwa kumsomea maelezo ya awali
 
Ngoja tuone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…