diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
SERIKALI imenunua korosho gha tani 214,269.684 zenye thamani ya Sh bilioni 717.1 sawa na asilimia 89.3 ya lengo la uzalishaji wa zao hilo. Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba ametoa takwimu hizo bungeni wakati anajibu swali la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). Mdee alitaka kujua hadi sasa ni kiasi gani kimetumika kununua korosho na fedha hizo zimetoka katika chanzo kipi na tani ngapi zimenunuliwa.
Mgumba amesema kiasi hicho kimenunuliwa ni kwa makadirio ya uzalishaji ya korosho msimu wa mwaka 2018/19 ambacho ni zaidi ya tani 240,000 za korosho gha. Amesema ununuzi wa zao hilo unafanywa na taasisi ya serikali ambayo ni Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ambayo malipo yanaingizwa kwenye akaunti ya wakulima. Hadi Januari 30, mwaka huu, Sh bilioni 424.8 zimewekwa kutokana na mauzo ya korosho tani 134,535.4.
Amesema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ni taasisi ya kibiashara yenye lengo la kupata faida na mtaji wake unaotokana na ruzuku kutoka serikalini na mikopo kutoka taasisi za fedha kama Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), NMB na CRDB. Amesema jumla ya wakulima 390 wameshalipwa hadi kukia Januari 30 mwaka huu. Aidha, vyama vya msingi 603 vimelipwa kati ya vyama vya msingi 605 vilivyohakikiwa.
Amesema Operesheni Korosho inatarajia kukamilika Februari 15, mwaka huu. Akiuliza swali la nyongeza, Mbunge wa Ndanda, Cecily Mwambe (Chadema) alihoji kwa nini serikali iliahidi kununua korosho kwa Sh 3,300 lakini inalipa kwa Sh 2,600. Mgumba amesema ni kweli Rais John Magufuli aliutangazia umma kwamba korosho itanunuliwa kwa bei hiyo na kinachofanyika ni kwamba wakulima wanalipwa bei hiyo, isipokuwa kwa korosho daraja la kwanza. "Korosho daraja la pili wanalipwa asilimia 80 ya bei hiyo, ambayo ni sawa na Sh 2,640 na korosho za daraja la chini wanarudishiwa wakulima, kwani serikali haiwezi kulipa vigae na mawe badala ya korosho,” amesema.