Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri

Hivi ni kweli bei ya mbege imeshuka kwa asilimia 75?

Inadhirisha ni jinsi gani unatumia kichwa kufugia nywele, badala ya kutumia kichwa kujadili mawazo yenye tija.. Gambaz mnamatatizo sana.
 
Tanzania bwana. Watu wameona wanaingiliwa kwenye ulaji wao tayari oporesheni tokomeza wameitokomeza !!!? Cheza na majangili wewe!!!.
 
Noted: ccm=serikali=sotoka.
obvious,
wanachama (gambaz) +wafuasi=sotoka
 
WASIFU WA LUKOSI 1.Huyu jamaa alikuwa polisi akafukuzwa sababu ya ajali katika msafara wa pm wakati ule John Malecela na kukimbilia Botwana ...

Mkuu hapo kwenye red; are you serious? Mbona anatemaga sana pumba tofauti na age yake? IQ yake lazima itakuwa extremely very low! Kubwa-jinga type.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ni janga la Taifa. The guy is butterfingered and forbearing. Sometimes You can't differenciate him with klutzy.

God forbid, ninatumaini Waziri Mkuu wa aina ya Mizengo Pinda atakuwa wa kwanza na mwisho nchini. It's pathetic to say the least.

Maamuzi ya huyu jamaa yako kisiasa utadhani ni katibu mkuu wa CCM anaogopa kukosa wanachama wakati ni mtendaji Serikalini.

Huwa wakati mwingine nashindwa kuamini kama ni mwanasheria ambaye anafahamu kazi ya serikali ni utekelezaji ndani ya rule of the law ambapo kila mtu yuko accountable under the law.

Sheria hazina siasa, na serikali ikianza kuweka siasa kwenye sheria inafikia sehemu hata wananchi wanashindwa kutofautisha kati ya chama na serikali. Hili ndilo linalofanyika Tanzania kwa sasa ambapo watu wanavunja sheria wakitegemea hawawezi kushughulikiwa kisheria(kesi ya malori na barabara).

Mawaziri kama Magufuri na Mwakyembe wakichukua maamuzi ya kiserikali kisheria, anawapiga stop for apparent NO sensible reason. Kwa nchi kama Tanzania inayopitia mpito wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, huwezi kuwa na viongozi wakuu wa nchi ambao character zao zinakaribia kufanana halafu mambo yakaenda vizuri na kwa kasi kuendana na mapitio ya nchi. Tanzania ya sasa inahitaji Rais au Waziri Mkuu ambaye ni mkali lakini pia awe firm and fair. Mh. Lowassa was one of them.

Nenda mbele, rudi nyuma. Mh. Lowassa alikuwa ni aina ya Mawaziri wakuu wanaohitajika kwa Tanzania ya sasa. Take it or leave it. Tangu aachie madaraka, utawala wa Rais Kikwete ndipo ulipoanza kuwa butu katika maamuzi magumu.

Kuna watu huwa wanadai Mh. Lowassa ni fisadi lakini wameshindwa kubainisha ufisadi wake uko wapi na hasa ikichukuliwa kuwa sheria za maadili ya wafanyakazi ( wabunge) zinawataka kuweka kila wanachomiliki na kama ikitokea wamedanganya na ikagundulika, basi kuanzia siku hiyo waliyogundulika ubunge wao unakoma na wanapelekwa mahakamani. Kwa nini hajapatikana mtu wa kudhibitisha kama kweli Mh. Lowassa ni fisadi pamoja na kuwa na maadui kwa makumi na mamia wa kisiasa?. Habari zinakuwa niza kiudaku na hearsay zaidi ya ukweli.

Hata Dr. Slaa alichagiza kuhusu sheria ya maadili kuhusiana na kadhia ya utajiri wa Mbowe lakini cha kushangaza pamoja na kudai Mh. Lowassa ni fisadi hajaweza kuitumia hii sheria kuchukua mkondo wake,
 
...mbunge wa
Busega Dk.Titus Kamani
(CCM),aliifananisha
serikali ya CCM na
ugonjwa wa miguu
na midomo kwenye
mifugo,maarufu
kama "Sotoka",ambao miaka ya
nyuma ulikuwa
ukiua ng’ombe
wengi...

HERI MIMI SIJASEMA!

Huyo dr Kamani angekuwa CDM alafu ndo anaikosoa sijui kingemkuta nini?CCM baba lao katika Uvumilivu wa kukosoana
 
Nini lawama?Kama unao uwezo wa kisiasa ni bora ukajiunge au ujiingize ktk siasa kuliko kuwakosoa hao watu wenu au ni bora ungeenda bungeni ukawapigia kelele humo humo ukapata na posho.(mzee wa Gambosh macho makavu)
 
ila jamani km umemsikia mbunge (ccm)
kangi lugola akiongea basi sidhani km unaweza kuishabikia ccm.
inauma sn jamani.


eti askari wamepiga risasi na kuuwa ng'ombe 60za mzee m1 wa miaka zaidi ya 60.
hiv huyu mtu amekua maskini ghafla ataisjije?!!
cku zinakuja .....
 
Tanzania bwana. Watu wameona wanaingiliwa kwenye ulaji wao tayari oporesheni tokomeza wameitokomeza !!!? Cheza na majangili wewe!!!.

Mimi nimeshangaa sana mkuu manning. Yaani nimewangalia jana wakati wanajadili..hakuna hata mbunge mmoja aliyejaribu kuonyesha ubaya wa ujangili na hali ilivyokuwa mbaya sasa hivi....wala kuonyesha kwamba ni kwa nini hii operation ni muhimu.

Mi nadhani kwenye.operation kama hii haiwezi kukosa majeruhi na kuisitisha pamoja na kiwalaumu watekelezaji kwa maaana ya JWTZ Polisi na askari wa wanyamapori ni kuwaondolea morale kabisa

Wabunge.wameshindwa kuona ni kwa nini ujangili uliokithiri utaathiri sana utalii.ambao unachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.

Suala la ujangili limeshakuwa systemic...wamekamatwa watu hapa lakini unasikia wanaachiwa au watu wanalobby waachiwe..huo.ni.udhaifu wa utekelezaji wa sheria na ingepaswa wahusika wote waadhibiwe vikali....

Suala la mifugo kuingi hifadhini ni kinyume cha sheria ya wanyamapori ..so ikikamatwa ndani inabidi mwenye nayo alipe faini nk...kuwaachia namna hii inaset precedent kwamba unaweza tu ukaswaga mifugo yako hifadhini kisha ikaachiwa kiroho safey. Kila siku watu wanahubiriwa wapunguze idadi ya mifugo lakini wapi....matokeo yake ndo kama hivi.

Kikubwa ninachoona hapa ni uchaguzi unakaribia na kura za wafugaji.ni muhimu sana...
 
Last edited by a moderator:
Umetoa hoja ya msingi,kama mtu huna la kuchangia ni bora ukakaa kimya
 
kumbe Lukosi ndio mtu wa namna hiyo!!!! daaa, aiseee kumbe ndio maanaa!.
 
Ni kweli kabisa kuwa tuheshimu utu wa binadamu na tusifanye mizaha ambayo haina tija.
Lakini pia Lukosi ajaribu kuangalia the way anavyo comment humu ndani ya jamvi,he is opening a lot of warfronts bila sababu!!
 
kosa kubwa ni kuingiza majeshi mengine katika mambo ambayo hawakusomea.
Polisi pamoja na udhaifu wao lakini angalau wana uelewa kiasi wa sheria lakini jwtz wapi na wapi.
Hili ndilo kosa ambalo hata mtwara limefanyika na madhara yake karibuni yatakuwa wazi.
 
Reactions: BAK
Unataka kusema Lukosi alijilipua kama Mkongo, Msudan, au Mnyarwnda? Kuna haja ya kufuatilia taarifa zake hapa London ili Home affairs waweze kujua kuwa jamaa huyu ni mtanzania na si mkimbizi aliyetoka katika nchi ya vita ili asiendelee kupewa status ya ukimbizi wa uongo na kula pesa za walipa kodi wa Kiingreza.
 
Ukweli ni kuwa hizi operesheni zimegusa maslahi ya wakubwa; namely Katibu mkuu Kinana, Lukuvi, nk.
Tulisikia taarifa wabunge hapo kusini wanahusika na ujangili. Then tunajua Kinana ndiye kinara wa ujangili Tz, alafu tukasikia msaidizi wa Lukuvi kahusika. Tungetarajia nini katika hili.
Najua hili la operesheni kimbunga limeingizwa tu kutupoteza maboya but ukweli ni kwamba kinacholengwa hapa ni kuondoa hii operesheni ya kupinga ujangili.
Makinda amekubali hili suala lijadiliwe na kamati iundwe kwa sababu mbunge mwenzake wa Iringa, Lukuvi ameguswa. Najua hata kamati itakayoundwa itakuwa imeshaandaliwa tayari na taarifa yao wataandikiwa...
 
Pinda kawa waziri mkuu mwenye mikosi na misukosuko kulipo wote waliomtangulia
inaonekana ni kweli hicho kiatu hakimtoshi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…