Operation ya uzazi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operation ya uzazi.

Discussion in 'JF Doctor' started by Kashaija, Sep 12, 2008.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimewahi kusikia mara nyingi kwamba watoto wanaozaliwa kwa operation ya kupangwa (yaani mama tangu anavyoanza kuhudhuria Cliniki daktari anamwambia kutokana na nyonga yako au kutokana na njia ya uzazi kuwa ndogo huwezi kujifungua kawaida mpaka kwa operation). Hivyo huyu mama anaendelea kulea mimba mpaka tarehe ikifika anaenda kufanyiwa operation bila hata kuhisi uchungu.

  Swali, je ni kweli mtoto anayezaliwa katika hali hii anakuwa na akili sana kuliko wanaozaliwa kawaida?
   
 2. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  kashaija sio kweli watoto wa ceasean section wana akili kuliko wengine ila chances za wao kupata damage ya kichwa wakati wa kuzaliwa ni ndogo sana. Kumbuka mtoto azaliwaye njia ya kawaida anakumbwa na mengi kama njia kuwa ndogo hivyo daktari hulazimika kutumia vitu vingine kama vacuum ama kumuongezea mama njia. Njia ya vaccum huwa na athari kama hatatumika kwa utaalamu kwani mtoto huweza kuminywa kichwa na kuharibu ubongo,nimewahi kushuhudia mtoto aliyezaliwa kwa msaada wa vacuum aliharibika vibaya kichwa na hadi leo hayuko sawa.
  Tukirudi kwenye swali letu la msingi, uzazi wa kawaida ni mzuri sana iwapo hakuna complications. Na mtoto wa operation ana less risk. Ila naye ana risk zingine zinazohusiana na operation. So its all about proper maternal care,proper hospital and proper birth monitoring process.
   
 3. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2008
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Operesheni ya uzai ya kupangwa(Elective Caesarean section) ni upasuaji ambao huwa umepangwa kabla ya uchungu kuanza,hivyo huwa hakuna dharura.Ziposababu nyingi za kufanya Elective C/S ambazo ni za kidaktari na nyingine ni binafsi(mgonjwa anaomba mwenyewe),This is a common occurence in developed world.Siku hizi pia wapo wanaoomba Elective C/S kama njia ya kupunguza uwezekano wa mama mwenye VVU kumwambukiza mwanae wakati wa kuzaliwa (C/S reduces chances of transmission of HIV by 50%)
  Tukija kwenye swali lako;jibu langu halitakuwa la moja kwa moja,kuna mambo kadhaa ya kutizama:-
  Uwezo wa akili wa mtu huchangiwa pia na vinasaba(genes )za wazazi wake.
  Pia Uwezo huo huchangiwa na mazingira anayokulia mtoto n:k

  Inaweza kutokea wakati wa kujifungua mtoto akapata kitu kinaitwa BIRTH ASPHYXIA hii kwa lugha rahisi ni kuwa mtoto anachelewa kulia baada ya kuzaliwa(meaning alishindwa kupumua vizuri na hivyo ubongo kukosa hewa).Brain damage katika umri mdogo wa mtoto huwa ni permanent hivyo huweza kusababisha utaahira (degree of severity hutofautiana kutoka kkuwa na uwezo mdogo darasani mpaka wale wanaoshindwa kujimudu kabisa)

  Zababu za mtoto kushindwa kupumua imeadiately baada ya kuzaliwa ni nyingi ikiwemo prolonged Obstructed labour (kama ulivyosema nyonga ndogo nk),Mtoto kulala vibaya (breech presentation) na nyinginezo

  Conclusion:Hakuna ukweli kuwa watoto waliozaliwa kwa elective C/S wana akili zaidi ya wale waliozaliwa kawaida
   
Loading...