Godblessme
Member
- Aug 5, 2014
- 22
- 3
Salaam. Unaombwa ufike na mtoto wako mwenye shida ya moyo siku ya JUMATATU, APRILI 18, 2016, SAA 3 ASUBUHI katika KLINIKI YA TAASISI YA MOYO MUHIMBILI ili alazwe kwa ajili ya kuonwa na madaktari wa kigeni wa upasuaji wa moyo. Upasuaji huo wa moyo ni bure ILA utahitajika kuchangia laki tano kwa ajili ya vipimo na utafute ndugu au jamaa wasiopungua watano kwa ajili ya kuchangia damu. Usikose nafasi hii, fika bila kukosa.
Ujumbe huu nimetumiwa kutoka Muhimbili hivi huu ujumbe unaweza kuwa na ukweli? maana niko Sumbawanga nilikuja Muhimbili kwa referral sina ndugu Dar wa kuchangia damu na mtoto anatumia Bima hiyo bure kumbe hakunaga? na mtoto alipewa dawa za miezi 6 imeisha mitatu tu. nisaidieni mwenye kujua au aliyeona ujumbe Kama huu. samahanini kwa ujumbe mrefu.