Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,347
- 5,553
OKTOBA 25, mwaka huu ni siku ambayo wafugaji wa Kijiji cha Kegonga, Kata ya Nyanungu, wilayani Tarime, mkoani Mara hawataisahau.
Siku hiyo mifugo takriban 190 ilipigwa risasi na askari wa waliokuwa katika Operesheni Tokomeza Ujangili.
Kama ilivyo kawaida ya wananchi wa kijiji hicho ambao robo tatu ni wafugaji, siku hiyo walipeleka mifugo yao kuchunga kwenye eneo la kilima kilichoko kandokando ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, eneo ambalo kila mwaka wamekuwa wakilitumia kwa ajili ya kuchunga.
Wafugaji hao wanasema wakiwa wanaendelea kuchunga, ghafla waliona magari yakija yakiwa yamebeba askari waliovaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wale wa wanyamapori.
Wanasema magari hayo yalipofika eneo hilo waliona askari hao wakitelemka ndani ya magari yao na kisha kuwafuata mlimani walikokuwa wakichungia mifugo yao.
Bhoke Taroge, anasema siku hiyo alikuwa akichunga na wenzake na ndipo walipofika askari hao na kuwaamrisha watelemshe ngombe wao chini na walipokataa walianza kupigwa na ndipo walipotii amri hiyo.
Tulipowafikisha ngombe hao chini kutoka mlimani walituambia tuwasimamishe ili waanze kuwapiga risasi na sisi walituweka kwenye gari na kisha ndipo walipoanza kuzimiminia risasi. Kwa kweli nililia sana, lakini wengine waliniambia ukilia na wewe utapigwa, anasema Bhoke.
Maria Chacha na Matinyi Kemore nao walikuwa wakichunga mifugo katika mlima huo, ni miongoni mwa walioamriwa kuswaga ngombe na kuwapeleka hifadhini, kisha wakashuhudia walivyopigwa risasi na askari hao pasipo kuwaambia kosa lolote na kisha walipomaliza waliondoka na kuacha mifugo hiyo ikiwa imekufa.
Mimi na Bhoke tulichukuliwa hadi kwenye kambi na walituambia tutoe shilingi laki mbili ndipo tutoke, hatukuwa nazo, tulilala huko hadi asubuhi ambapo wazazi wetu walikuja wakatoa pesa hizo ndipo tukaachiwa na tuliporudi tulikuwa na uchungu mkubwa, kwani mifugo yetu ilikuwa imepigwa risasi, anasema Kemore.
Kama inavyofahamika jamii nyingi za wafugaji wa kabila la Wakurya huchunga mifugo yao kwa ushirika, na ni utaratibu wao kuchunga mifugo kwa pamoja, ni kwa mantiki hiyo askari hao baada ya kukuta kundi kubwa la mifugo hiyo waliamua kuipiga risasi.
Oktoba 29, mwaka huu waandishi wa habari tulifika kijijini hapo ili kujionea hali halisi ilivyo.
Tuliwasili kijijini hapo majira ya saa nne asubuhi na kupokewa na wananchi wa kijiji hicho wakiongozwa na mfugaji Mohere Chacha aliyetupeleka katika ofisi ya kijiji hicho, ambapo tulisaini kitabu cha wageni.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Chacha Tugara, alitukaribisha na kututambulisha kwa baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na wahanga wa tukio hilo waliokuwepo siku hiyo.
Baadaye mwenyekiti huyo alitueleza tukio zima lilivyokuwa huku akionyesha masikitiko makubwa namna walivyokerwa na kitendo hicho ambacho wao walikiita kuwa ni cha kinyama.
Ofisa Mifugo wa Kata ya Nyanungu, Paschal Batholomeo, anakiri mifugo hiyo kupigwa risasi na kwamba amekuwa akiwafanyia upasuaji baadhi ya ngombe ambao hawakufa na kutolewa risasi.
Anasema ataendelea na suala hilo kwani bado wengi walionekana kuendelea kuishi na risasi.
Kwa kweli tukio hili ni la kinyama na linasikitisha sana, baadhi ya mifugo hali si nzuri kutokana na kuishi na risasi sehemu mbalimbali za miili yao, anasema ofisa huyo.
Baada ya kupata maelezo hayo tulianza kutembelea miji ya wahanga hao.
Kila mji wa mhusika tulipoingia tulikutana na vielelezo kama vile ngozi zilizokuwa na matundu, mabaki ya viungo kama vile miguu pembe na nyama.
Takriban kaya 22 tulizotembelea walidai mifugo kama mbuzi hawakuweza kupata hata nyama yake kutokana na kuliwa na fisi.
Kinachotushangaza sisi ni pale askari walipowafuata wachungaji wetu mlimani na kuwalazimisha kuswaga mifugo na kuipeleka hifadhini, kwanza eneo walilokuwa wakichungia mmeliona, wao walikuja na kuanza kuchoma hata nyumba za watu waliokuwa wakiishi hapo mlimani kihalali.
Baadaye walianza kuwalazimisha mabinti zetu wapeleke mifugo hifadhini na walipofika huko walianza kuipiga risasi, kwani mifugo hiyo ndiyo ilikuwa imeficha meno ya tembo, anahoji Mohere Chacha mkazi wa kijiji hicho.
Ilipofika majira ya saa kumi jioni tulimaliza zoezi letu la kutembelea wahanga wote, ikiwa ni pamoja na kufika katika kilima ambacho wananchi hao walikuwa wakichunga mifugo yao kabla ya kuamriwa na askari hao kuitelemsha na kwenda kupigwa risasi.
Tukiwa kijijini hapo tuliuliza kama taarifa hizi serikali ya wilaya inazifahamu, ambapo Diwani wa Kata hiyo, Mangenyi Ryoba, anasema ameshatoa taarifa hizo kwa uongozi wa serikali lakini hakuna hata kiongozi yeyote aliyekuwa amefika hapo.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Allan Kijazi, anasema alikuwa China, hivyo nimtafute Mhifadhi Mkuu wa Serengeti.
Nilipomtafuta Mhifadhi huyo Mkuu wa Serengeti aliyejitambulisha wa jina la Mwakilema, anasema zoezi hilo linaendeshwa kijeshi.
Awali lengo la operesheni hii iliyoanzishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, ilikuwa ni kusaka majangili wanaoua tembo, lakini sikumsikia akisema ngombe wapigwe risasi.
Nashindwa kufahamu nani aliyewatuma hawa waliokuwa wakifanya doria hii kupiga risasi mifugo ya watu na kuiua na mingine kuiachia ulemavu.
Tangu operesheni hiyo ianzishwe kumekuwepo na taarifa kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuua mifugo kwa kuipiga risasi.
Katika Mkoa wa Morogoro iliripotiwa ngombe 80 kupigwa risasi, Wilaya ya Bukombe iliripotiwa ngombe 50 kupigwa risasi.
Kimsingi katika hali ya kawaida kwa mtu anayeweza kuvuta taswira na kulifikiria jambo hili lazima atakuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani suala hili hata mtoto mdogo lazima limtie shaka.
Hawa waliofanya kitendo hiki wanapaswa wachukuliwe hatua kama walivyochukuliwa hatua askari polisi wa wilayani Serengeti waliokamatwa na jino la tembo wakiwa katika harakati za kulitafutia wateja.
Kwa mfugaji ukimuulia mfugo wake ambao ndilo tegemeo lake kubwa tayari unakuwa umemrudisha kwenye umaskini asioutarajia.
Zipo lugha nyingi ambazo sasa zimetungwa na viongozi za kuwatuhumu wafugaji kuwa wengi wao wamekuwa wakiingiza mifugo hifadhini kwa ajili ya kutafuta malisho, siwezi kupingana na hilo lakini swali langu litabaki palepale kwanini ngombe walipigwa risasif
Ujangili bado upo kama alivyosisitiza Rais Jakaya Kikwete bungeni, lakini namshukuru hata yeye kwa kukemea wale wote waliokwenda kinyume cha kile walichoagizwa, naamini wao ni watu wazima na wamesikia, hatutarajii tena kusikia mifugo ya wananchi ikipigwa risasi kwa kisingizio cha kusaka meno ya tembo.