Open university tusaidieni kwenye hili la Moodle

mwamasangu

Member
May 12, 2017
36
28
Mimi mwanafunzi wa CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA. Kwanza nakipongeza chuo kikuu huria kuanzisha utoaji wa elimu kutumia e-learning (Moodle).

Mimi ninayefanya kazi katika taasisi binafsi ni tatizo kupata ruhusa ya kwenda masomoni au kusoma.

Hii ilinishawishi kupitia rafiki yangu aliyenieleza kuwa Open University of Tanzania wameanzisha utoaji wa elimu kupitia online yaani moodle. Nilienda chuoni kufuatilia na kupata maelezo ya kina kuhusu kusoma kutumia moodle ukiwa nyumbani. Nilipata maelezo na kuambiwa nitasoma kupitia online na kufanya assignment zote zinazowekwa na Mwl husika ktk somo au course unayosoma. Na mwisho kabisa utahtaj kufanya mtihani tu.

Na hizo assignment zitakuwa kama course work japo utahitaji kuzitetea kipindi cha Face to Face session. Nilishukuru na kuona hii mbona rahsi kwangu ambaye nimeajiriwa kwenye mabenki. Nilianza kusoma kusoma na tulienda vizuri tu. Sasa kipindi hiki cha face to face nimepata mkanganyiko ambapo hatukufanyiwa mahojiano ya hizo assignment na mwisho wa siku centre yangu ikaniambia hizo assignment nilizofanya kuna uwezekano zisihesabike kwenye course work kwa sbb walimu kwanza hawakutuassess pili wengine waliweka assignment moja au mbili ambapo zinatakiwa tatu.

Baadae tukaambiwa tusajili test mwezi wa tano mwishoni ambapo mimi nilijiandaa tangu siku nyingi ofisini kwangu nitaomba ruhusa mara moja tu kama wiki mbili kwa ajili ya mitihani sasa kuna test ambazo ni kama wiki mbili pili kuna mtihani wa kufunga semester. Je katika yote hayo kutokuwa assessed au mwl kuweka assignment moja...sisi wanafunzi sio kosa letu. Tulio kwenye sector binafsi hasa benki hiki nikilio kwetu. Wanafunzi wengi walipenda hii moodle....swali ambalo najiuliza je walijiandaaa au kuna tatizo??? Tatu chuo kitusaidie kupata ufafanusu mzuri maana ukitembelea centre kila wakati unapata majibu tofauti tofauti na inachanganya kweli kweli.

Nauomba uongozi wa chuo kikuu utusaidie hili suala lisijitokeze tena au basi moodle iondolewe tu tusome tukijua kuna test na annual....badala ya kukomaa na online harafu mwishoni tunapelekwa direction nyingine.

Ni mimi mwanafunzi wenu!! Tusaidieni nawapenda sana
 
Tatizo kuu la open university wengi wanaosoma hapo malengo yao makuu siyo kuongeza ujuzi bali kupanda vyeo na mishahara tu maana 98% ni wafanyakazi, thats why na chuo kinaendesha mambo hovyo hovyo.

OUT ilikuwa miaka hiyo siyo sasa,kwa sasa ni mwendo kwa ku.solve past paper tu ili itimie miaka yako 3 upate degree yako basi ili upandishwe cheo kazini kwako.
 
Tatizo kuu la open university wengi wanaosoma hapo malengo yao makuu siyo kuongeza ujuzi bali kupanda vyeo na mishahara tu maana 98% ni wafanyakazi, thats why na chuo kinaendesha mambo hovyo hovyo.

OUT ilikuwa miaka hiyo siyo sasa,kwa sasa ni mwendo kwa ku.solve past paper tu ili itimie miaka yako 3 upate degree yako basi ili upandishwe cheo kazini kwako.
Skills unaweza kupata inategemeana na mtu. Hata huko vyuo vingine hamna lab...nenda TIA nenda IAA nenda UDSM wanafunzi wanaosoma MBA na hawa wa open wanaosoma MBA yaweza kuwa sawa tu.
 
Back
Top Bottom