Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,114
- 219,213
Ile kampeni ya CHADEMA ya kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu na ulazima wa Katiba Mpya, imeshika kasi huko Chato ambako ilipangwa kufanyika mikutano mitano kwa siku moja tu.
Pamoja na kukodi waganga, wachawi na maharamia waliolipwa ili kuchoma magari ya CHADEMA kwa lengo la kumtisha Lissu, lakini jambo hilo limeshindikana na Lissu kaingia Chato kwa kishindo kikuu, huku umati wa watu ukimfuata kila mahali.
Pamoja na elimu kubwa aliyoitoa kuhusu Katiba Mpya na Mkataba wa kudhalilisha nchi wa Bandari na DP World ya Dubai, Mh. Lissu amewaambia watu wa Chato kwamba Magufuli ndiye aliagiza watu wamshambulie kwa risasi ili wamuue na kwamba alimwagiza Job Ndugai aliyekuwa Spika wa Bunge kwamba baada ya Lissu kuuawa asifanyiwe uchunguzi wowote na azikwe haraka kwao Ikungi.
Hata hivyo Lissu amedai kwamba, kifo hicho cha kupangwa kilishindikana baada ya Mungu kukataa njama za Shetani.
Wakati Lissu akimwaga maneno hayo watu wengi hawakuonyesha kushangaa maana ni kama walikuwa wanaelewa kila kilichosemwa. Jambo lingine ambalo Lissu amelisema kuhusu Magufuli A.K.A Jiwe ni hasara kubwa aliyoisababisha baada ya kuvunja Mikataba ya Makampuni ya Wazungu kwa ushauri wa akina Kabudi, Osoro na Mruma. Bali Lissu amesema pamoja na uharamia huo wa Magufuli bado hakuuza Bandari za Tanganyika.