Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,741
- 218,332
Taarifa iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema mbele ya maelfu ya wananchi huko Tabora , ambayo imetoka Jeshi la Polisi , imeeleza kwamba Chadema hairuhusiwi kufanya mikutano ya hadhara kwenye baadhi ya maeneo ya Majimbo ya Kaliua na Bulyankulu .
Moja ya kata zilizozuiliwa ni Kata ya Milambo , kwenye kijiji cha Kasuveta , kwa madai kwamba hicho ni kijiji wanachokaa Wakimbizi ambao hawahusiki na siasa za Tanzania .
Hata hivyo, Lissu amefichua kwamba kwenye kijiji hicho kuna vituo kadhaa vya kupigia kura, ambavyo vinatumika wakati wa Uchaguzi Mkuu , kura ya Mbunge na Rais hupigwa kwenye kijiji hicho , sasa kama ni cha Wakimbizi , hao wanaopiga kura za Mbunge na Rais ni akina nani ?
Lissu amefichua kwamba Vijiji hivi vinavyosingiziwa kuwa vya Wakimbizi ndio machimbo ya Wizi wa kura yanayotumika kuwasaidia Wagombea wa ccm .
Toa maoni yako