Katika jamii, mara nyingi watu huogopa kuingilia mahusiano ya watu wengine hususani kama kuna muenendo wa mmoja wao kutokuwa mwaminifu dhidi ya mwenzake. Hii ni kwa sababu taarifa hizo zinaweza kusababisha ndoa/mahusiano kuvunjika na hivyo mtoa taarifa kuonekana ndiyo chanzo cha hilo tatizo ndani ya hiyo ndoa/mahusiano.
Pia tabia za wahusika na ukaribu wa huyo mtu dhidi ya jamii iliyomzunguka ambayo ikingeweza kumpa taarifa za mwenendo mmbaya wa mwenzake huchangia kwa sehemu kubwa. Kuna wengine hawana urafiki wala mahusiano ya karibu na jamii au familia zao, hivyo ni vigumu mtu kujitosa kutoa taarifa.
Binafsi nafikiri mambo haya yafanyike
1. Kila mtu ajitahidi kuwa mwaminifu kwa mwenza wake. Hii itasaidia matatizo yote ya hapo juu kutokuwepo
2. Kila mtu na ajitahidi kuwa na uhusiano mzuri na watu waliomzunguka. Ni rahisi kupewa taarifa kama mwenendo wako unakubalika ndani ya jamii, lakini ukijifanya kiburi utaendelea kuibiwa huku jamii ikifurahia
3. Unapopekea taarifa, ni vzr kuzipokea bila jazba na kuzifanyia uchunguzi kwa undani maana si kila taarifa inaweza kuwa ni ya kweli. Nyingine zinaweza kuwa zina lengo la kubomoa familia zenu. Ktk hili pia, si busara kumshushua/kumsema vibaya mleta taarifa kuwa ni mmbea na amekuja kuigonganisha familia, huwezi jua kuwa inawezekana taarifa hizo ni za kweli
Kwa kusema hayo, binafsi ningependa kuelezwa kama mwenza wangu ni mapepe ili nipate muda mzuri wa kufanya uchunguzi na nikithibitoisha niachie ngazi mapema kabla ya magonjwa hatari hayajanivamia ....
HP