SEMKIWA3
Senior Member
- Feb 17, 2019
- 103
- 59
Habari za leo wanaJF.
Ni siku kadhaa zimepita sasa tangu serikari yetu tukufu ya Tanzania imetoa onyo la kusitishwa kwa matumizi ya mifuko ya plastiki na nailoni.Hili ni jambo jema kabisa kwa faida ya jamii yetu ya sasa na vizazi vijazo.Pia niunge mkono juhudi za serikari yetu katika kufanya kufanikisha zoezi hili.
Uzii huu nimelenga zaidi katika kuangalia faida na hasara za Onyo hili kali kutoka kwa serikari yetu ambalo kila raia wa Tanzania natumaini analifahamu kwa sasa na pia tunajua msimamo wa serikari katika hili.
Kwa upande wangu nitaelezea zaidi upande hasara,alafu nitaomba wanaJF wenzangu mchangie hoja kwa pande zote mbili yaani faida na hasara,mimi nitaongelea baadhi ya hasara ninazoziona katika jamii yangu ya huku Koromije lakini pia sisi kama watanzania tunatakiwa tuliongelee hili swala kwa kina zaidi.
Zifuatazo ni baadhi ya hasara zitakazoikuta jamii ya watanzania kutokana na onyo la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki.
1.Ukosefu wa ajira;
Hii ni kutokana na wafanyakazi wengi ambao walikuwa wameajiriwa katika viwanda vya kuzarisha mifuko ya plastiki kusimamishwa kazi kwa ajiri viwanda vimefungiwa.
2.Kushuka kwa pato la taifa.
Hii ni kutokana na ukosefu wa kodi zilizokuwa zikikusanywa kutoka kwa wafanyakazi,wafanya biashara na viwanda kwa ujumla wa vinavozalisha mifuko ya plastiki.
3.Mtazamo hasi kutoka kwa wajasiriamari wadogo wadogo.
Kama ukienda masoko ya Dar kuna wale vijana wanajiita Wakazi au Kariakoo,ambao huwa wanauza mifuko ya plastiki,hawa ndugu zetu wamejikita sana katika hii biashara na inawawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku,baada ya onyo hili kali kutoka serikarini tutegemee kuona mitazamo hasi ya hawa vijana.
4.Upungufu wa misitu asiria.
Japo sijafahamu zaidi tamko la serikari kuhusu mbinu mbadala baada ya kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki.Kwa haraka haraka mimi naona kuwa njia mbadala itakuwa ni matumizi ya karatasi kama vile bahasha katika kufungia na kufungashia bidhaa,hizi karatasi ni matunda tuyapatayo kutokana na miti au misitu,hivo basi kama serikari itaamrisha kuhusu matumizi ya karatasi,hivyo basi tujiandae na tatizo la uharibifu na upungufu wa misitu yetu.
Nawasilisha,leteni nondo zingine.