Onyo kwa wanaochukua wake za watu

Onyo kwa wanaochukua wake za watu

Tuko watu tuna tabia ya kuchukua waume za watu na wake za watu! Na tunafikia mahali tunajivuna na kujipigapiga vifua kwamba! Hakuna mwanaume au mwanamke unayeshindwa kumpata ukimtaka!

Sababu zozote za kuchukua mke wa mtu au mume wa mtu hazikubaliki mbele za MUNGU! Kwanini unatumia uzuri wako, pesa zako, umaarufu wako kuchukua wake za watu na waume za watu? Na unajigamba kwamba hakuna mwanamke mwenye uwezo wa kukukataa!

Kama wewe unachukua wake za watu na waume wa watu juwa wewe ni mfu, huwezi kupona! Litakupata janga lolote la kukufutilia mbali katika uso wa dunia, ni laana! Usiseme ananijipendekeza mwenyewe, hiyo sababu haiwezi kuiponya nafsi yako.


Kama wewe unatembea na mke wa mtu au mume wa mtu, unatakiwa kuacha mara moja na kumrudia Mungu kwa toba nzito! Muache huyo mke wa mtu au mume wa mtu! Hata kama anakupenda sana! Muache!
Tulia! Mungu atakupa wa kwako! Kwani wanawake wameisha au wanaume wameisha? Wasiwasi wako tu! Na hata kama unaye mumeo au mkeo acha tamaa wewe; kaa na wa kwako, jivunie wa kwako! Jiamini.


#msgDelivered

mbona kama mahubiri haya>..?
 
Sante mkuu...binafsi nmekuelewa.....mleta mada
 
clearly mtoa mada hajui ile feeling ya conquest...ebu jaribu kwanza. some things cnt b explained they cn only b felt
 
Wakati wa Yusufu lilikuwepo li mke wa mfalme ambalo lilijipeleke lenyewe kwasababu tu! Yusufu alikuwa mzuri wa uso! Yusufu alijua akikubali umauti ni lazima! Soma kwa wakati wako maandiko haya Mwanzo 39:6-20!
Kashaiga mbona leo una hasira sana
Member wanauliza UMEGONGEWA
nakushauri tumia Kater**o
km ni kibamia yupo Mchina

km Maandiko mtafute Daud aliyemchukua Mke wa mwanajeshi (Mhiti)
na bado Daud alimpeleka mstari wa mbele ili akafe abaki na mke wa mtu
Bado alikuja zaa mtoto Sulemani (Mfalme) baada ya mtoto wa kwanza MUNGU kumchukua km adhabu)
ukinyang'anywa (kugongewa)Mke jua sio wa kwako hamlingani tafuta Saizi yako

 
Back
Top Bottom