Onyo kwa EAC kuhusu sarafu MOJA

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Shirika la fedha duniani limeonya jumuiya ya Afrika Mashariki dhidi ya kuharakisha mpango wake wa kutaka kuwa na sarafu moja
Mataifa ya jumuiya hiyo yalIanzisha mkakati wao wa kutaka kubuni sarafu moja inayoweza kutumika katika nchi wanachama ili kurahisisha biashara katika kanda hiyo.
Mataifa tano wanchama wa jumuiya hiyo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana, yalitia saini mkataba wa kuanza mkakati wa kutafuta sarafu moja katika kipindi cha miaka kumi ijayo , mpango wanaotumai utapanua biashara katika kanda hiyo nzima.
Mpango huu utashuhudia nchi hizo zikiwianisha sera zao za kifedha na kuchumi na kuweza kubuni benki kuu moja.
Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda tayari husoma bajeti zao kila mwezi Juni.
Ushauri huu kutoka kwa shirika la fedha duniani, unakuja wakati kanda ya Ulaya ingali inakumbwa na matatizo ya kiuchumi kutokana na viwango vikubwa vya madeni yao huku mataifa wanachama wakikabiliwa na ukosefu wa ajira.
Mkuu wa shirika hilo ambalo yuko ziarani Kenya, Christine Lagarde amesema kuwa kuwianisha sera za kifedha ni wazo zuri lakini pia ni changamoto kubwa.
Bi Lagarde alisema itakuwa muhimu kwa Kenya kutoa funzo kutoka katika mataifa ya Euro ambayo yanatumia sarafu moja na kusoma aina ya changamoto zinazokabiliwa nazo.
Ziara ya Bi Lagarde nchini Kenya ni kama jambo la kawaida kwa shirika la fedha duniani kuhakikisha kuna uthabiti wa kiuchumi katika sehemu mbali mbali duniani.
Kenya ni nchi ya pili kwa ukubwa kwa uwekezaji katika kanda ya Afrika Mashariki.
Kuweka wazi soko la pamoja la biashara kwa mataifa wanachama wa mataifa ya Afrika Mashariki itakolesha biashara na kuinua maisha ya watu wa kipato cha kadri ambao wanastawisha zaidi uchumi.

chanzo: Onyo kwa EAC kuhusu sarafu - BBC Swahili - Habari

 
Naunga mkono suala la kutokuwa na sarafu mmoja kwasasa ni mapema mno. Kuna vitu ambavyo inabidi muwe mmevifikia kwa kila nchi ili muweze kuwa na sarafu mmoja.
Vitu hivyo ni kama vifuatavyo;
1. Kuwa na central bank mmoja na ni kuajili ya kuangalia na ku shauri kuhusu mzunguko wa hela na kudhibiti inflation
2. Kuwa na bajeti yenye nakisi inayokaribiana ili kuweza kudhibiti madeni ya serikali.
3. Kuwa financial regulatory mmoja kwa ajili ya prudential regulatory na financial conduct authority.
4. Taxation system inayofanana isiyokuwa na upendeleo kwa eneo Fulani.
5. Kuwa na mamlaka ya madeni ya serikali mmoja kwa jumuiya yote kwa ajili ya ku issue new debt na kudhibiti debt kwa eneo zima kwa serikali zote ku depend kwenye hiyo taasisi ili kudhibiti madeni na kutoa mikopo mipya kwa serikali.
6. Namengineyo
Tukiweza kutimiza hayo hapo juu tunaweza kufikilia kuwa na sarafu mmoja za ya hayo tuta ingia kwenye matatizo kama ya Eurozone . Tujifunze kutokana na wenzetu wa Eurozone.
 
naunga mkono uwepo wa sarafu moja utasaidia kuiimarisha tsh dhidi ksh na hela ya rwanda
 
Back
Top Bottom