kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Onyo kali la Kamanda wa IRGC kuhusu hatua tarajiwa za wakuu wa Marekani
Apr 07, 2019 15:01 UTC
Meja Jenerali Mohammad Ali Ja\\\'afari Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran (IRGC) ametoa onyo kali na kusema: "Iwapo Marekani itatekeleza hatua yake tarajiwa ya kuiweka IRGC katika orodha ya makundi ya kigaidi, basi ifahamu kuwa haitapata utulivu katika eneo."
Meja Jenerali Mohammad Ali Ja'afari Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa kauli hiyo Jumapili kufuatia kuenea taarifa kuhusu hatua tarajiwa ya Marekani ya kuweka jina la IRGC au SEPAH katika orodha ya makundi ya kigaidi na kuongeza kuwa: "Iwapo upuuzi kama huo utafanyika, wanajeshi na maafisa wa usalama wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi hawatakuwa na utulivu tena."
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea kusema kuwa, kwa mujibu wa sera za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, iwapo Wamarekani watahatarisha usalama wa taifa wa Iran basi kutachukuliwa hatua za kukabiliana na hilo.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ametahadharisha kuwa, iwapo Marekani itatangaza IRGC kuwa kundi la kigaidi, basi itakuwa imejiingiza katika kinamasi.
Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumapili, Zarif amesema makundi yanayomuunga mkono Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni yanajaribu kuikinaisha Marekani iiweke IRGC katika orodha ya makundi ya kigaidi. Ameongeza kuwa: "Iwapo Rais Donald Trump wa Marekani atachukua hatua kama hivyo basi Washington itakuwa imeingia katika kinamasi." Amoneya kuwa hatua kama hivyo itakuwa na matokeo mabaya kwa wanajeshi wa Marekani katika eneo.
Gazeti la Wall Street Journal Jumamosi liliandika kuwa, serikali ya Marekani inalenga kushadidisha mashinikizo dhidi ya Iran kwa kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika orodha ya makundi ya kigaidi. Gazeti hilo limedokeza kuwa Marekani inapanga kutangaza uamuzi wake huo Aprili 8.
Sent using Jamii Forums mobile app