Onyo: Epuka mwanamke anayekupenda kwa sababu ya pesa

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Nov 2, 2012
1,220
1,225
Habari zenu wanajamii forum

Naona sasa suala la kusisitiza mwanaume atafute pesa ili awapate wanawake linchukua kasi sana. Jamani mapenzi sio pesa kama mtu kakupenda kwa kuwa una pesa na maisha mazuri huyo hajakupenda wewe.

Ukiona mwanamke anakupenda kwa kuwa wewe ni mambo safi nakuambia utakuja kuumia maana huyo ni sawa na nyoka wa kufugwa siku akikumbuka porini historia itabadilika.

Tafuteni pesa ili kujikimu na mambo mengine kama kuwasaidia wazazi wenu,jamii,wadogo zako sio ili uwakamate wasichana au wanawake hapo hupendwi wewe inapendwa pesa maana wakati huna kitu hawakuja sasa una pesa wanakuja utasema unapendwa.

Labda kama unatafuta mwanamke wa kukamilisha matamanio yako kwa muda hapo sawa lakini kama mwanamke wa kuujaza moyo wako muombe MUNGU.Wangapi wanapesa na kila kitu lakini mwanamke akishazoea hali hiyo anaanza michepuko,mapenzi mapana wakuu.

Waepukeni watu wanaowafuata kipindi mambo yapo kwenye mstari
 
1466933891387.jpg
 
Pesa ni suala la muhimu katika maisha, lakini upendo ni suala la muhimu katika mapenzi au ndoa. Kwa kifupi maisha bila pesa ni vigumu, lakini pesa pekee yake, pasipo upendo katika mapenzi haiwezekani.
Well said
 
mtafute hela mhudumie wazazi na wadogo zenu, mke na watoto nani ahudumie.... Basi tafuta hela huku ukiwa unaishi home kwenu
 
Pesa ni shida sana huwa sichoki kutafakari ilikuwaje hadi Mzee Machache akaweza kumuoa yule Miss Tz aliepita...Ukichukua Age difference ni kubwa sana kiasi cha kuwa Baba na mtoto wake lakini ndo hivyo pesa iliongea binti yuko ndani leo na Mzee kuonyesha yuko fit kapiga Twins..
 
hakuna ubaya mwanamke akikupendea pesa. zikiisha akiondoka pia hakuna ubaya.
 
Back
Top Bottom