Onyo: Dr. Magufuli asizomewe tena

Kura asipewe na azomewe tu,nami nasema mzomeeni tu kwa sababu hakuna namna nyingine"(Pinda voice)
 
Onyo wape ccm waache kusumbua wananch kipindi cha uchaguzi
 
Tatizo lakee anapenda sana mikutano isiyo rasmi, haya mambo yake ya kusimama barabaran na kusema watu ndo wamemsimamisha aache... .. .
 
 
Kwa hiyo darasani ulusomea matusi
 
Ile ndo mitaa ya kuanza nayo ukiingia, viroba vya asubuhi vile, mitaa ya wanadarisalama huwa hawazomei wao wanangoja kukukata tu, hiyo itakuwa moshi ndogo ubungo
 
Kistaarabu na matusi yote hayo tunayoyasikia kila siku? Labda utueleze kama ustaarabu unaosema sio tunaoufahamu wengine.
 
Na mwanza Nyegezi stand kwenye mkutano wa wenje alizomewa.alikuwa anatoka sengerema
afadhali mkuu ulikuwepo, maana nilichangia hili la Magufuli kuzomewa Mwanza kuna jamaa linajiita jingalao likawa linanibishia! Tena mkuu alizomewa kuanzia Buhongwa, Mkolani, Nyegezi stand na Mkuyuni!
 
Azomewe tu maana hamna namna!! Ccm imechokwa si yeye...
 
Kama una busara ungewashauri kwanza kina nape, lusinde na mwigulu na wengine waache kumtukana lowassa kwenye majukwaa ya kisiasa ningekuona wamaana. Magufuli kuzomewa ni sawa kabisa maana hao niliowataja wanamtukana lowassa na magufuli akiwemo yy anakenua tu kwahiyo hayo ndo malipo yake.
 
Mzee naona umejaa upepo.

Lowassa ni kama maji: usipoyakoga utayanywa, usipoyapikia ugali utapikia mihogo.
 
Job nilikuwepo alizomewa sana na wenje alikuwa hajafika bado akuwa nganza na mnangani
 
Zomeeni tuu, tena sana maana baada ya tarehe 25 October,mtakuwa msibani kuomboleza kushindwa,WAKIWA NYIE!
 
Tumechoshwa na vitendo vya kuzomewa kwa mgombea wetu. Kuanzia kule Mbeya na hata hapa Dar es Salaam,Dr. Magufuli amekuwa akizomewa na kuoneshwa wazi kuwa hatakiwi. Yeye hujikaza kisabuni tu. Hutetemeka lakini huimarika.
Mkuu umeuliza maswali muhimu sana na japo ndipo pa kuanzia. Nini kimeondoa utiifu kwa CCM? Hilo ndilo tatizo halisi wala si kuzomea. Kuzomea ni dalili tu ya tatizo ulilouliza

Pili, kuzomea kuna ukakasi gani zaidi ya matusi? Mbona alikuwepo wakati utenzi wa matusi ukisomwa?

Tatu, kuzomea sioni tatizo, tatizo ni kama kuna mtu analeta vurugu. Hata jana Rais wa China alizomewa kule UK lakini hakuna aliyerusha mawe au ngumi, inakubalika

Nne, Magufuli pia ana sehemu yake. Ukiji behave kama mtu wa kijiweni, watu wa kijiweni wata ku treat kama mwenzao. Sasa anapopiga push ups majukwaani badala ya kueleza sera tayari anakaribisha watu wa vijiweni. Hapo ndipo wanakuja na mizigo yao ikiwemo hiyo ya kukosa uvumilivu. Si mwenzao? Wanamshangilia akipiga push ups, kumzomea ni opposite ya hilo, akubali kuwa naye ni sehemu ya tatizo
 
Sasa mgombea anapopiga push-up,badala ya kutangaza sera, wananchi tufanyeje? Mnadhani sisi ni mbumbumbu kiasi hicho? Rais wa Kuwait ni Sadam, reli zitajengwa kwa kiwango cha lami, sisi ni malofa, wanaume wabebe mimba,kweli? Tunyamaze? Tumelogwa? Mgombea akiongea kistaarabu nasi tutakuwa wastaarabu...angalia hadhira kabla ya hotuba,,,, jiongeze...
 
Kuzomewa si kosa bali ni hisia kuwa hukubaliki n hatukutaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…