-Ni watu pekee ambao wako tayari kuandamana kupinga matumizi ya lugha yao wenyewe, na kutetea ya kigeni, haijawahi tokea Dunia hii! only in Africa (Tanzania)
-Miaka yote tumekuwa tukifundishwa na kudanganywa wazungu (wakoloni) walikuwa wabaya kumbe ni uongo, tunafanya yale yale waliyoyafanya na mbaya zaidi tunaharibu angalau wazungu walijenga.....
-Nyerere kaongoza miaka 24, tunadanganywa ndio aliyeunganisha watanzania, wakati Dunia nzima inafahamu huwezi kuunganisha Taifa kwa miaka 20, haijawahi kutokea sehemu yoyote Duniani!
-wahindi < 1% lakini wanamiliki >85% ya uchumi wetu!
-kila kitu kizuri tulichonacho ni tangu wakoloni, Oysterbay, Upanga, Kinondoni, Msasani.. Coco beach ndio beach pekee (public beach) Dar ambayo nayo ni ya mkoloni, ingawaje Dar yote imezungukwa na Bahari tumeshindwa kutengeneza coco beach nyingine..
-Siku zote kujivunia na kupenda kunyang'anya mali za watu wengine badala ya kujenga zetu, mfano tulinyang'anya wahindi nyumba zao Upanga ambazo walizijenga kwa jasho lao!
-Ni watu pekee ambao siku zote tunang'ang'aniza watu wengine watupende na waoe au waolewe na sisi na kulalamika kwamba wanatubagua, lakini huwezi kuta muhindi au mchina au mzungu akilalamika kwa nini watz hawataki kuchanganika nao ingawaje sisi ni zaidi ya 95% ya nchi yote...
Na mwisho na muhimu kabisa nakuuliza wewe unayesoma sasa hivi, ukiwa porini au usiku unaendesha gari ukakuta watu wawili mmoja mswahili mwingine mzungu wanaomba lifti na unaweza kuchukia 1 utamchukua yupi (kuwa mkweli na nafsi yako)