Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,590
- 8,718
Open Univ inasaidia sana. Rais Karume (mstaafu) alikuwa akisoma pale, sijui kama alimaliza au la. Shamuhuna naye aligraduate pale mwaka juzi nk. Wazee wanapiga miasainimenti, matesti, matekihome, mayuii, masaplimentari kama kawaida. Jaji naye anagonga msuli.
Kuwa na chama cha upinzani ambacho upande wa pili wa Muungano (Zanzibar) hakina hata sheha (mjumbe wa nyumba kumi), wala muwakilishi hata mmoja wala mbunge hata mmoja. Halafu kinaamini kabisa hicho ndio chama mbadala cha Watanzania...kwi kwi kwi teh teh teh!
Kuwa na naibu spika mvuta sigara kubwa,
V
SENGEREMA
Kuwa na Mbunge anaeishi Mary USA kutuwakilisha kwa viti maalum.
1. Nchi inayojitapa kuwa ina serikali sikivu lakini serikali hiyo haitaki kusikia au kuongea na makundi yenye madai na kukimbilia kuwaziba sauti watu wake mahakamani ili isiwasikie.
2. Nchi yenye raisi asiye jua chanzo cha umasikini wa watu wake. Kumbuka ile kauli ya jk alipo hojiwa na mwandishi wa france.
3. Nchi yenye raisi ambaye amesha wahi kuwaomba wezi wa fedha kurudisha walichoiba huku wezi wa ndala na wakwapua simu wakipigwa ban (kuchomwa moto).
4. Nchi yenye usalama unaoruhusu ndege ya nchi nyingine kuingia kwenye anga yake kuja kubeba wanyama hai walio ibiwa na viongozi waandamizi wa serikali.
5. Nchi yenye bunge lenye spika ambae akitaka hoja iungwe mkono akiwahoji watu sauti za siooooo zikiwa kubwa kuliko ndio walio sema ndio hata kama ni wachache wanashinda. Kumbuka hoja ya wenje jana.
6. Nchi ambayo mnajimu mkuu ameshawahi kutangaza kumlinda raisi kwa ulinzi usio onekana. Achilia mbali ule wa vifaru na mizinga.
7. Nchi ambayo wakati wa uchaguzi viongozi wa chama tawala huwatishia watu kuhusu kuingizwa nchini makundi ya kigaidi huku wakijua kuna vyombo vya usalama.
Hii ndio Tanzania bana!!! Kwi kwi kwi kwi!!!
....Raisi kubadilishana neti na madini, Raisi hajui kwa nini nchi yake ni maskini, Rais kuwa na ndoto ya kuleta timu kubwa na tajiri duniani kuja kushangaa umaskini wetu..!
Naibu Spika = Jobu Ndungai
Sigara Kubwa = Bangi aka Ganja
Nimejitahidi kurahisisha kwa zomba na ritz
Kwi kwi kwi kwi teh teh teh.