Online post converter, ugonjwa unaowasumbua wengi

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,269
7,773
Hii ni program maalum na inapatikana JF tu. Haihitaji taaluma kubwa sana kujua namna inavyofanya kazi. Unajua inafanyaje kazi? IPO kwa muda gani? Imeanzishwa na nani? Na watumiaji ni akina nani? Imeanzishwa kwa lengo gani? Je watumiaji wanaijua?. Ungana nami:

Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza nilijiunga na jf. Kwa muda mrefu kutokana na kutingwa na shule nilikuwa ni msomaji wa nyuzi mbalimbali pasipo kuchangia wala Ku like. Kwa kipindi hicho chote nimeona kuna app ya kubadili nyuzi.

App hii haipatikani kwenye playstore au sehemu nyingine sasa na Hiyo. Hii ipo vichwani mwa wasomaji wa nyuzi mbali mbali na hujidhihirisha wakati wa uchangiaji.

JINSI INAVYOFANYA KAZI

Hufanya kazi kwa kubadili uzi wowote kutoka katika jukwaa lolote na kuwa ya kisiasa. Mfano katika jukwaa la MMU, mtu anaweza kuomba ushauri juu ya ndoa au mahusiano yake. Katika jukwaa la habari unaweza kukuta kuna taarifa ya serikali juu ya jambo Fulani, au nchi Fulani wamefanya hiki ama kile.

Wakati mwingine huwa ni mambo ya msingi katika jamii,yetu au maisha ya kila siku. Pia inaweza kuwa ni elimu juu ya jambo Fulani has a kilimo,ufugaji, uvuvi,afya, au elimu nyingine sawa na hizo.


Watu huchangia mawazo na kutoa michango yao mbalimbali katika Uzi husika. Mawazo nayo wakati mwingine huwa ni nyongeza ya kile alicho kitoa mleta Uzi au shukrani n.k. lakini katikati ya michango Hiyo au ndani utashangaa kuona mabadiliko makubwa. Yaani lengo la uzi hubadilishwa kwa kiasi kikubwa.

Watu walio athiriwa na mfumo huu, hubadilisha Uzi wowote kuwa wa kisiasa. Huibuka katika kuchangia kwa kutaja chama Fulani, kiaongozi, kambi yake kwa kufananisha na Uzi huo. Mfano utakuta taarifa ya mpango mzuri wa uwekezaji nchini, mtu anakurupuka tu anasema "kwenye Hilo hutawaona wa ufipa ua wa lumumba", au mbowe, lowasa, magufuli n.k wanahusishwa kwenye nyuzi ambazo si za kisiasa. Mpaka mtu unajiuliza wa ufipa au wa Lumumba wanahusikaje na Uzi huu?

Mwanzoni mwa Uzi utapata Mawazo mazuri lakini mwishoni hubadilika na kuwa malumbano ya kisiasa. Unakuta Uzi umeanza na habari nyingine umeisha na habari nyingine     

OMBI LANGU

Niwaombe tuweni na busara katika kuchangia na sio kuleta utani au kubadili lengo la msingi la Uzi. Tuchangie kwa kuzingatia jukwaa na lengo la uzi. Niwatakie ijumaa njema
 
HILO KWA SASA HALIWEZEKANI.TULIOJIUNGA JFORUM MIAKA YA SASA HATUWEZI KUKUELEWA TUMEPATWA NA KANSA YA UKADA UCHWARA.HATUFIKIRI,HATUONI NA HATUSIKII.NAUNGA MKONO NASAHA ZAKO
 
Yaani lengo la uzi hubadilishwa kwa kiasi kikubwa.
Ndio wabongo tulivyo, hebu nenda kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye vikao vya harusi,hata mtu na mkewe hoja inaanza vizuuri kabisa inaishia kwenye siasa.kwa mfano unamchukua changudoa unapatana nae vizuri munafika gesti munamaliza haja zenu anakwambia niongezee hela ukimuuliza kwanini anasema nyinyi si ndio escrow.:)
 
HILO KWA SASA HALIWEZEKANI.TULIOJIUNGA JFORUM MIAKA YA SASA HATUWEZI KUKUELEWA TUMEPATWA NA KANSA YA UKADA UCHWARA.HATUFIKIRI,HATUONI NA HATUSIKII.NAUNGA MKONO NASAHA ZAKO
poa ila nashukuru kwa kuniunga katika kufikisha ujumbe
 
Ndio wabongo tulivyo, hebu nenda kwenye vijiwe vya kahawa, kwenye vikao vya harusi,hata mtu na mkewe hoja inaanza vizuuri kabisa inaishia kwenye siasa.kwa mfano unamchukua changudoa unapatana nae vizuri munafika gesti munamaliza haja zenu anakwambia niongezee hela ukimuuliza kwanini anasema nyinyi si ndio escrow.:)
umeniacha hoi mkuu
 
Back
Top Bottom