Online Application form ya Uhamiaji Tanzania

Online Application form ya Uhamiaji Tanzania

Muyobhyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
8,149
Reaction score
6,556
Tafadhali naomba kujulishwa, nimemsikia jana Dr. Mwigulu Nchemba akisema sasa unaweza ukaomba kupitia online, sawa nimekwenda na nimeona hizo form lakini sasa kwa mimi ninayetaka hiyo kubadilisha passport ya kutoka ya zamani kwenda e-passport nitumie ipi

manake kuna vipengele hivi nimevikuta

Mwanzo

Ombi Jipya

Ombi linaloendelea

Ufuatiliaji wa Ombi

kwa mie ninayetaka kubadilisha niende kipengele kipi hapo

asante kwa msaada wenu
 
na sisi ambao tulikuwa hatuna hizo pass ila si vibaya tukawanazo kipindi hichi but kuna kipengele unatakiwa ujaze unakwenda wapi..... kwa mimi sina safari ila naitaka pass sasa nitasema naenda wapi?
 
na sisi ambao tulikuwa hatuna hizo pass ila si vibaya tukawanazo kipindi hichi but kuna kipengele unatakiwa ujaze unakwenda wapi..... kwa mimi sina safari ila naitaka pass sasa nitasema naenda wapi?

Si juzi hapa walisema hadi uwe unasafiri ndio unapewa kile sio kitambulisho.
 
fungua fungua tu utapata jibu.... kama wameshndwa kuonesha watanzania namna ya kuomba na kutoa ufafanuzi kiundani... ina maana wakipokea errors nyingi wataelewa kuwa bado hawajaeleweka...
 
Huu mfumo wao unamapungufu, backend wametumia vanilla php halafu hawako nondo sana kwenye upande wa security. Front end UI haiko friendly kabisa ndio maana hata mtoa maada amekwama.
Sijui walitumia gharama kiasi gani kuunda huo mfumo. Nikisema sana naweza kukamatwa kwa uchochezi ngoja ni mute, wakipigwa wataamka🙄
 
na sisi ambao tulikuwa hatuna hizo pass ila si vibaya tukawanazo kipindi hichi but kuna kipengele unatakiwa ujaze unakwenda wapi..... kwa mimi sina safari ila naitaka pass sasa nitasema naenda wapi?

"passport sio kitambulisho kila mtu akawa nacho, ni pass ya kusafiria, (Magufuli, 2016)" so kama husafiri no need!
 
mie naona kuweka laki na nusu ni kutaka hiyo pesa iende kwenye miradi kama SGR na mengineyo,
 
na sisi ambao tulikuwa hatuna hizo pass ila si vibaya tukawanazo kipindi hichi but kuna kipengele unatakiwa ujaze unakwenda wapi..... kwa mimi sina safari ila naitaka pass sasa nitasema naenda wapi?
kwani anayebadilisha ni sawa na kuomba upya, data na kila kitu si wanacho, nilimsikia yule mama mkuu wa uhamiaji akidai ukishajaza unaenda na kitambulisho chako tu, na vile vile hii form naona kama upo tz unatakiwa uilipie elf 20 hivyo basi ni jumla ni laki na 70 na sio laki na nusu kama walivyosema wao,
 
"passport sio kitambulisho kila mtu akawa nacho, ni pass ya kusafiria, (Magufuli, 2016)" so kama husafiri no need!
mbona huwa kinaombwa sector nyingine ingawa sio lazima lakini kuna kipengele wanauliza kama una passport
 
mie naomba Mwigulu nchemba aje atujibu, na swali kwa watu wanaobadilisha passport zao, nao wanatakiwa waombe upya kama hujawahi omba? swali lipo hapo tu
 
Huu mfumo wao unamapungufu, backend wametumia vanilla php halafu hawako nondo sana kwenye upande wa security. Front end UI haiko friendly kabisa ndio maana hata mtoa maada amekwama.
Sijui walitumia gharama kiasi gani kuunda huo mfumo. Nikisema sana naweza kukamatwa kwa uchochezi ngoja ni mute, wakipigwa wataamka🙄
kweli mkuu nimeona ina mapungufu hii form, watu wa IT wa Uhamiaji waiangalie tena kwa undani
 
Yaani fomu pekee 20000
Ila twaruhusiwa badilisha hata kama haijaisha
 
duh kumbe kwa hili wazee wa "showoff" tumeumbuka.....
usiogope, form ya ni kawaida tu hii, ipo kama uliyoomba hapo mwanzo, sema hii ni online form, sijaona tofauti labda kwa vile sijaclick kule mbele
 
Yaani fomu pekee 20000
Ila twaruhusiwa badilisha hata kama haijaisha
sasa kwenye kubadilishwa hicho kipengele ndio sikioni, swali langu nimeuliza tunaenda kipengele gani manake hapo ni kwa wale wanaoomba upya, na wanaofatilia kama hawajapata majibu,
 
mbona huwa kinaombwa sector nyingine ingawa sio lazima lakini kuna kipengele wanauliza kama una passport

ukishakipata unaweza kutumia, the same as driving licence, ukiwanayo unaweza tumia kama id but kama pia haufungwi
 
Back
Top Bottom