Ongezeko la omba omba feki mijini si la kupuuza

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Kuna jamaa mmoja ombaomba barabara ya morocco -mwenge -tegeta; huwa anashangaza sana na staili yake ya kuomba!
Haya nimaneno yake namnukuu; "Ndugu zangu mwenzenu naomba msaada, mke wangu aligongwa na gari kalazwa mhimbili tulivambiwa akakatwakatwa na mapanga, mimi hapa naumwa sana malaria, presha, U.T.I na typhoid, watoto wamefukuzwa ada shule hawajala siku tatu Leo, naombeni msaada wenu,napokea chochote mwenye mia hata mia mbili!"; mwisho Wa kunukuu!

Huyo jamaa anaomba sanasana kwenye madaladala tena huwa anapanda kwa kugombania,;

Ukitafakali juu ya huyo jamaa kama kweli ni mgonjwa basi kwa magonjwa yake alitakiwa atembee na dripu katundikwa!

anadai watoto wamefukuzwa shule kwa ada, shule gani wakati elimu ni bure?

mke wake kama aligongwa na Gari ailivamiwaje na majambazi akiwa mgonjwa?

Ni maswali yanayoumiza kichwa mwisho mtu unaweza ukaamua kumzaba kibao badala ya kutoa msaada!

Siyo huyo tu, wapo na wengine wengi tu mijini tunakutana nao,
  • Wapo wanaoomba nauli ukiwaambia uwape lifti huwa hawataki,
  • wapo wanaoomba hela ya kula ukiwanunulia chakula wanachokita wanakimwaga! n.k
Hilo limenifanya niwaze ipo haja hawa ombaomba mjini kuwaandalia operesheni maalum!

Haiingii akilini saa 11 alfajili unamkuta ombaomba asiye na miguu au mikono kafika madaraja ya mwendokasi juu akiomba tena kwenye wheelchair, unashindwa kuelewa huyu kapaa au kafikaje pale!

  • kuna wale ombaomba wanaotembea wamebeba watoto mgongoni wakidai wametelekezwa na wanaume kumbe maskini hata hao watoto huwa wanakodi.
  • pale kariakoo kuna jamaa huwa anavizia magari kwenye foleni, akiona dreva anachezea simu anajichomeka ili gari imguse aonekane kagongwa ili mwenye gari alipe;
  • wako watu wametengeneza hadi fomu za hospitali kubwa kubwa kama mhimbili,Ccbrt na aghakan wakidai zimegoma kuwatibia n.k
ifike mahala sasa huu mchezo tuukomeshe!
ipo haja ya kukamata watu wote wanaofanya biashara hizi! hususani wanaodhamini hii biashara haram ya ombaomba!
 
Huyo jamaa kuna siku moja napita huko Dar alizuiliwa na konda kupanda gari na konda alieleza kuna siku mdau kajitokeza waende huko hospitali kuona mkewe ila jamaa akala kona.

Kila siku yeye anatumia hiyo mbinu kuhadaa watu sijui Malaria yake hiyo ni ya kisasa kiasi kwamba akae nayo kila siku.

Kuna mmoja pia yuko Arusha anafunga mkono bandeji na kuimwagia damu sijui ya nini, akikuona na ukiona ule mkono unajua kweli mgonjwa kumbe ni tapeli.

Kuna wanawake pia hutumia watoto wachanga na kueleza kuwa watoto wao ni wagonjwa ili umpe msaada kumbe mwizi.

Siku hizi sisaidii tena uwe unataka msaada kweli au unatapeli.
 
huyu jamaa alishakua maarufu dar kila siku UTI yake haiponi😅😅 nilikutana nae mwaka jana mwezi wa 11 hivi, nimeshangaa mwezi huu tena bado analalamika anasumbuliwa na UTI na watoto wake hawajala siku 3.
 
Kuna maza mmoja yupo k/koo stand ya Magari ya mbagala yomboo... Anaomba nauli anasubiria watu wanaoshuka kwenye mwendokasi alishawahi kuniomba nauli siku tatu mfululizo hyo siku ya tatu mpaka akajistukia mwenyew ...
Na kuna Dada mmoja anapanda daladala za kupitia barabra ya mandela na karatsi LA kuonyesha Mtoto wake anaumwa cancer basi anazikusanyaa pesa kbao vikipita vtuo vtatu anashuka anapanda jingne.. Sasa MTU kama huyu kwa siku anamake sh ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aisee ?
 
ndo hivyo kageuza biashara!
 
huyu jamaa alishakua maarufu dar kila siku UTI yake haiponi😅😅 nilikutana nae mwaka jana mwezi wa 11 hivi, nimeshangaa mwezi huu tena bado analalamika anasumbuliwa na UTI na watoto wake hawajala siku 3.
hahahah!
 
Na hawa wanaozunguka na vi wheel chair kwenye bar na migahawa kwakweli wanakwaza sana

Unakuta mtu umeagiza zako msosi wanakusubiri ukianza tu tonge la kwanza wanakufuata kama siyo kuchumiana dhambi ni nini?

Hivi hawajui kama mambo yamebadilika? 🤷‍♂️

Kwanini wakuchonganishe na Mungu uonekane ni mchoyo na mwenye roho mbaya?
 
nini kifanyike kutokomeza hawa wazugaji?
Mamlaka husika iwafuatilie kwa kufanya upelelezi " kisha wauanike katika jamii endapo itabainika kuwa Ni wazugaji au ni mitaji ya watu "...... ili pindi watakapo kuwa wanaamua kuwachukulia hatua wananchi wasije kutafasiri kwamba serikali inawaonea " endapo watachukuliwa hatua itasaidia kuwa punguza hao omba omba" Maana kuna ambao wataamua kuacha kwa hiyari ili wasikutane na mkono wa sheria .. hata wale ambao huwa wanatamani kujiingiza kwenye huo mkumbo wataachana na huo mpango mara moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom