Ongezeko la mshahara Tangu 2015 mpaka 2022

Ongezeko la mshahara Tangu 2015 mpaka 2022

Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
1,742
Reaction score
1,562
Habari zenu wakuu,

Poleni na Hongereni kwa kutumikia Taifa kupitia nyanja tofauti tofauti kuanzia wakulima, wafugaji, mafundi, wafanyabiashara na watumishi wa umma.

Baada ya salam naomba niende kwenye lengo la kuandika maneno yote haya.

Kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa 2022 hakuna zile Annual increments Kwa watumishi wa serikali,

Ongezeko hilo lipo kwa mujibu wa sheria na serikali haikuweza kutekeleza hilo Kwa miaka 7 sasa licha ya kuwa ni utaratibu uliopo kikanuni.

Ni asilimia ngapi ya kiwango cha mshahara ambacho kikiongezwa kinakuwa kimefidia miaka yote ambayo annual increment haikuweza kuongezwa kwa watumishi?

Asanteni sana na karibuni.
 
ni ngumu kufidia kwa miaka yote hiyo maana scale zinatofautiana, cha msingi iongezwe kiasi cha kuendana na hali tuliyopo. Pia serikali izingatie sana kima cha chini maana wanaoumia wengi na wa huku chini huko juu kuna fursa nyingi.
 
Sasa si utupandishie huo mshahara ndugu Mpandisha mishahara? Maana yule jamaa alituumiza kweli kweli! Na huyu mrithi wake aliye tuachia mwenyewe naye yuko busy kujijengea himaya ya kudumu kama mtangulizi wake!
 
Chamsingi sana ni serikali kuongeza kima cha chini cha mishahara na pia kuweka leveling katika ulipaji wa mishahara

Sio unakuta kwamba katika taasisi mbili tofauti watumishi wenye sifa sawa lakn wanatofaut kubwa katika mishahara yao

Kwa kumalizia hali ni ngum saana kwa watumishi wa kada ya chini na ukizingatia tunamikopo yaan 90% tunapokea kuanzia 140000 mpaka 250000 kwa mwez hata sijui tunawezaje kuishi kwa kwel inauma sana..
 
Habari zenu wakuu,

Poleni na Hongereni kwa kutumikia Taifa kupitia nyanja tofauti tofauti kuanzia wakulima, wafugaji, mafundi, wafanyabiashara na watumishi wa umma.

Baada ya salam naomba niende kwenye lengo la kuandika maneno yote haya.

Kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa 2022 hakuna zile Annual increments Kwa watumishi wa serikali,

Ongezeko hilo lipo kwa mujibu wa sheria na serikali haikuweza kutekeleza hilo Kwa miaka 7 sasa licha ya kuwa ni utaratibu uliopo kikanuni.

Ni asilimia ngapi ya kiwango cha mshahara ambacho kikiongezwa kinakuwa kimefidia miaka yote ambayo annual increment haikuweza kuongezwa kwa watumishi?

Asanteni sana na karibuni.
Kusema annual increment ilisimama, sitetei ila huenda labda ni kwa baadhi ya secta za umma, lakini wengine increment ziliendelea na hadi sasa zinaingia.

Kama ni zile nyongeza za mishahara alizoasisi mst. Ally Hassan Mwinyi, alizokuwa akizitangaza kila Tarehe 01/05 hizo sawa ni mwaka wa7sasa ni hola, yaani bila bila.
 
Mbali na upandishaji wa mishahara serikali inaweza kuja na ubunifu kwa kutoa special package ,namanisha mikopo maalumu kwa watumishi yenye Riba ndogo na muda mrefu kuliko hii ya ki biashara.
Mabenki yatapoteza faida nchi itakosa kodi
 
Kusema annual increment ilisimama, sitetei ila huenda labda ni kwa baadhi ya secta za umma, lakini wengine increment ziliendelea na hadi sasa zinaingia.

Kama ni zile nyongeza za mishahara alizoasisi mst. Ally Hassan Mwinyi, alizokuwa akizitangaza kila Tarehe 01/05 hizo sawa ni mwaka wa7sasa ni hola, yaani bila bila.
Sekta gani hizo baadhi?
 
Back
Top Bottom