Ongezeko la Kima cha Chini cha Mshahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ongezeko la Kima cha Chini cha Mshahara

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by pareto 8020, Apr 26, 2010.

 1. p

  pareto 8020 Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba msaada kutoka kwa wenzetu wataalam wa uchumi kunielimisha juu ya hili suala la ‘short-notice mandatory imposition of minimum wage’ katika sekta binafsi. Je uamuzi wa namna hii ambao haukupangwa kwa muda mrefu- hauna athari za kiuchumi?
  Kwa kawaida, si kila taasisi ina bajeti zake za mwaka ambazo inapanga ikiwa ni pamoja na mishahara…sasa wanapojikuta wanatakiwa kuongeza mishahara ghafla bila kupanga….mzigo huo anaubeba nani?
  Kwa mtazamo wangu as lay man, mwisho wa siku mzigo wa kuongeza mishahara bila kupanga au kutoa ‘advance notification ya muda mrefu’ utamwangukia mlaji who happens to be mfanyakazi na mwananchi mwingine… kwani leo mtu mwenye kiwanda anayetengeneza unga wa sembe, akitakiwa kuongeza mshahara kwa asilimia 100, atakachofanya, ni kuongeza bei ya bidhaa yake ili amudu hizo gharama mpya….akiongeza bei ya sembe….si mfanyakazi huyo huyo tunayetaka kumuongezea mshahara ili apate unafuu wa makali ya maisha ndio ataelemewa na mzigo wa kununua sembe ile kwa bei ya juu zaidi?

  Kwa maoni yangu, in the future, nyongeza zozote muhimu zipangwe na kuwa communicated well-in advance ili zizingatiwe katika mipango na bajeti za mashirika husika.

  While on the subject suala lingine ambalo ningependa msaada wa ufafanuzi wa wataalam wa uchumi…. Hivi kutakuwa na shida gani endapo kutakuwepo ONE NATIONAL MINIMUM WAGE…itakayotumika katika sekta zote (binafsi na umma). Kwa kutumia lay man’s logic, wafanyakazi hawa (private na public) wote wana operate katika mazingira yale yale….wote wanalipa nauri ya basi ile ile, au wote wananunua mafuta ya diseli au petrol kwa bei ile ile, na wote wananunua sembe kwa bei ile ile….na kulipia umeme kwa gharama zile zile.

  Actually kwa mtazamo wangu, hata within private sector kufanya mgawanyo wa malipo ya different minimum wage kwa sub-sector unaweza kuwa umepitwa na wakati kwani…kwa mfumo wa sasa, assumption ni kwamba sekta zenye faida kubwa basi zinapangiwa minimum wage kubwa, na zile zisizozalisha sana….zinapangiwa rate ndogo…lakini kwa dunia ya leo ambayo mazingira ya biashara hayatabiriki…mfumo huu unaweza kuwa irrelevant….. kwa mfano…sekta ya usafiri wa anga…Imepangiwa mimimum wage kubwa kuliko sekta nyingine…..assumption ni kwamba ni sekta yenye kuzalisha zaidi…lakini ukweli wa mambo ni kwamba….sekta hii inategeneza hasara zaidi (ndio maana ATC na mashirika mengine ya ndege ya nchi nyingine yana survive kwa subsidies)…..au leo sekta ya madini inakuwa categorized kuwa na sekta yenye faida kubwa..lakini kwa hali halisi ya soko la dunia…madini ya vito kama Tanzanite yameshuka bei sana….sasa kuwapangia bei ya juu maana yake ni kufanya washindwe kumudu labour costs na mwisho wake wataishia kupunguza wafanyakazi…

  Tatizo lingine ninaloliona…ni timing…..wakati sote tukitambua kwamba mtikisiko wa uchumi duniani umeathiri sana uzalishaji wa viwanda vyetu…plus changamoto nyingine za ndani kama vile mgawo wa umeme….na ushindani kutoka bidhaa za bei rahisi kutoka nje ya nchi…viwanda vyetu vina hali taabani…if anything vinahitaji kuwa boosted kwa namna yoyote ile ili viendelee kuzalisha na kutunza ajira zilizopo..wakiongezewa mzigo mwingine…tena on short notice….madhara yatakuwa ni makubwa kuliko faida….

  Like I said, pengine sijalielewa somo vizuri…ndugu wachumi nisaidieni kuona kama kuna logic katika suala hili..
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  madhara yapo mengi sana ya kushitukiza upandishaji wa mishahara na inawezekana baadhi ya waajiri wakawapunguza wafanyakazi wao
  kwa mtazamo wangu naona serikali imetangaza ongezeko hili kwa malengo mbalimbali ikiwemo kuonyesha jinsi inavyoshughulikia matatizo
  ya wafanyakazi na pili kuzuia uwezekano wa mgomo, lazima tufike wakati tuangalie kwanini wakurupuke kuongeza mshahara ghafla namna
  hii lazima kuna mapungufu kwenye wizara hii , cha msingi waziri kapuya ajiuzulu kupisha watendaji wengine, au kama yeye atasema ya kuwa
  alitumwa na rais kuwabana wafanyakazi kwa kipindi chote hicho hadi watake kugoma basi wafanyakazi waangalie jinsi gani ya kuchukua
  mahamuzi mazito dhidi ya rais wao,
  upandishaji huu wa ghafla unaweza kusababisha kufungwa kwa baadhi ya viwanda kwa hiyo tukapoteza ajira na kupunguza uzalishaji na kuathiri uchumi wetu
   
Loading...