Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
ONDOA HOFU AKILI YAKO ELEKEZA KWENYE KILE UNACHOWEZA KUKIFANYA KIUFASAHA
Unajua ili ufanikiwe ni lazima uweze kufanya mambo makubwa, ambayo hujawahi kuyafanya kwenye maisha yako. Kwasababu ukiendelea kufanya kile ambacho unafanya, utaendelea kupata matokeo ambayo unayapata sasa.
Lakini unapofanya mambo haya makubwa na mageni kwako, mara nyingi unakuwa huna uhakika na matokeo unayotaka kupata.
Hujui kama kweli utapata kile unachotazamia kupata.Tofauti na kufanya kile ulichozoea kufanya, ambapo kwa asilimia kubwa una uhakika na matokeo.Hivyo basi unapofanya jambo jipya na kubwa, unaweza kuweka akili yako kwenye moja ya maeneo haya mawili;
1. Unaweza kufikiria sana kuhusu yale matokeo ambayo unataka kuyapata na hivyo kupata hamasa ya kuendelea zaidi, japo ni wachache sana wanaofanya hivi.
2. Unaweza kufikiria sana kuhusu kile usichokijua, kile ambacho huna uhakika nacho, na hii inakukatisha tamaa kuendelea na hapa ndipo watu wengi wanapokuwepo.
Unaweza kufikiria yale matokeo unayotaka kupata au unaweza kufikiria kile usichokijua ambacho kinaweza kutokea.
Kufikiria usichokujua, hakuna msaada wowote kwako, zaidi ya kukuogopesha na kufanya uone mambo ni magumu sana.
Kufikiria yale matokeo makubwa unayotegemea kupata, kunakufanya uone inawezekana na hivyo kuweka juhudi zaidi.
Muda wote ifanye akili yako ifikirie zaidi kile ambacho unategemea kupata na sio kile ambacho unahofia.