Mwezeshaji1
Senior Member
- Sep 26, 2023
- 141
- 313
Kwakuwa mada za ulimwengu wa visivyoonekana zina mwitikio na walio wengi kuonesha nia ya wazi ya kujifunza, tusiwanyime maarifa💯, kwa kuwa wewe ukipewa bure, sharti utoe bure!
Unajua, kabla sijafahamu ukweli kuwa ulimwengu wa roho UNAONGOZA ulimwengu wa mwili, sikutilia maana saaana, uhusiano wa haya maeneo mawili.
Hivyo chamsingi nimepata riziki, ilitosha kuendelea na hustle, bila kutaka kuyajua haya maeneo.
Ila, sikuacha kukumbuka maono (Live) ambayo nilipata kushuhudia nikiwa na umri wa miaka 8, hivyo sikusahau kabisa ulimwengu wa roho, hata hivyo sikuupa UZITO stahiki.
Nikiwa nje ya mahali tulipoishi, (wakati ule nikiwa mtu mwenye hofu saaaana), yani hata ukitumwa dukani usiku, unaona kana kwamba umepewa adhabu gani!
Wakati nikiwa hapo nje (nyumba za kijijini), nilitazama bafu upande wa juu, na sikuona chochote cha ajabu, wala kushtua na hivyo niliendelea kukaa hapo nje, karibu na mlango wa nyumba - tayari kukimbia ndani if anything.
Ila hali ilibadilika baada ya Mama mzazi (aliyeokoka na hata sasa yu mcha Mungu), kupita na ndoo kwenda kuoga.
Punde si punde, moto ukaonekana ukizunguka bafu, tena unaenda, na unarudia. Nikawa na viulizo (cha ajabu, sikutetereka), huenda ni ukubwa wa butwaa, au ulinzi wa Mwenye enzi Mungu, ambao huo hutuliza nafsi, isitetereke.
Haikuishia hapo, alipoingia Mzee naye akawa anazingirwa hivyo hivyo, akaoga na kuendelea na shughuli.
Ukawa ndio UKOMO wa hofu, na sikuwa na uoga tena (hata hivi leo, siogopi , hata nchi ngeni natoka usiku kwenda kutafuta chakula etc)
Kwanini nasimulia?
Lengo ufahamu;
Hata hivyo , hiyo huwa KIANZIO na usipochukua hatua, hauwezi kufikia viwango vyovyote vingine.
Ya kufanya;
Kwa wote ambao mnasumbuliwa (kunyanyaswa) na nguvu za giza (ulimwengu usioendana na maagizo ya aliyekuumba), ufunguzi utaupata hapa (anzia kwenye neno ukipenda)
View: https://www.youtube.com/live/DMerAu6FVH4?si=C4P_JW6ClV2nFg0J
View: https://www.youtube.com/live/ElTiiLo-muY?si=PUSFM6fRAd9F1pEe
View: https://www.youtube.com/live/QJQCczhT50Q?si=3zYOVvbXr_xfJ4jg

- Unaishi kwenye ulimwengu unaoongozwa na asiyeonekana (asiyefikiwa) kwa jinsi hii ya damu na nyama, hata kama Yeye ndiye alieyeuumba ulimwengu
- Unaweza kuona (nje ya hivi vya kawaida)
- Ukitaka kuona, usiingie huku na kule❌, ila kaa kwa yeye aliyeumba kuona, kusikia na vyoote vilivyomo - hauna sababu ya kupitia mlango wa nyuma , nenda moja kwa moja na nitakuelezea wawezaje.
Hata hivyo , hiyo huwa KIANZIO na usipochukua hatua, hauwezi kufikia viwango vyovyote vingine.
Ya kufanya;
- Jiunganishe na aliyekuumba , huyu atakupa kuona yale ambayo hauwezi kwa jicho la damu na nyama - fuata utaratibu aliouweka , YEYE ameamua tuunganishwe nae kwa njia ya kuamini ule ujio wa Kristo , tambua nafasi ya Kristo katika unganiko la rohoni (Yesu amekuwa badala ya mwanakondoo, ng'ombe au njiwa asiye na mawaa, ambaye ungehitaji chinja, damu isiyo hatia ikutakase, ndio upate unganiko na aliye juu), hivyo amekupa "express but EFFICIENT" namna ya kuungana.
- Unachotakiwa ni kufahamu huu ukweli halafu amua kuunganishwa nae, naamini unaweza amua rohoni, hata hivyo unashauriwa kusema kwa sauti, uweze kutangaza uhusiano wako mpya. Tumia maneno haya "BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAUNGAMA DHAMBI ZANGU NA KUMAANISHA KUZIACHA, NAPOKEA ZAWADI YA WOKOVU, NAKUTAMBUA KUWA BWANA NA MWOKOZI, NA KWAMBA ULIKUFA, NA SIKU YA TATU UKAFUFUKA, ILI NIPEWE HAKI. ASANTE KWA KUNIKOMBOA, NA KUANZIA SASA, NIMEKUWA MWANA" - Kufahamu zaidi hili, soma yahana 3:16
- Hapa unakuwa tayaaari, kuanza uhusiano utakaokupa FAIDA ambazo haujawahi kuwaza, hata uambiwe unaweza usielewe, inabidi ushuhudie wewe mwenyewe. Kuanzia hapa, umekuwa connected na "divine intelligence", unaweza fahamu ya siri, kupitia kwa roho anayeingia ndani kwako. (Hii roho hukuongoza katika maisha unayotakiwa kuishi, usiseme "sitaweza kuacha hili au lile", wewe kubali ile sadaka (mwanakondoo aondoaye dhambi), hii ya 'utaachaje hili au lile", utabadilishwa taaratiiibu kwa usaidizi wa roho mtakatifu, huku ukifurahia uhusiano (au tuseme kifurushi chako ulichosubscribe kwa kutambua uhusiano wa Kristo katika kukupa macho ya rohoni)
- Anza kukua (lazima ule ndio ukue), tafuta mtu aliyekuwa akulishe - hapa anza kwa kufungua maandiko, hata kama hauelewi, Omba usaidizi kwa Roho aliye ndani (anaitwa ROHO MTAKATIFU) huku unakula kwa wachungaji ATAKAOKUONGOZA huyo Roho wa BWANA.
- Kumbuka passport/stamp ya kufikisha uyaombayo ni lile jina , YESU, hivyo uombao usiache stamp (mfano: naomba haya katika Jina la YESU", amen.
- Ufahamu wako utaanza kuona vitu ambayo haukuona KABLA na itakupa kukua MNO (kiroho/kikazi na kibiashara).
- Usaidizi wa kuanzia namna ya kuongoza biashara, hadi mke/mume wa kuoa, hauna jambo ambalo utakosa ushauri (labda usisikilize), utaokoa pesa, muda na kuepusha MAJANGA.
- Ukiwa na shida , kimwili , kiroho , kiuchumi , hauko mwenyewe ...muhimu SANA ule kutoka kwa aliyekuwa kiroho (ili ufahamu ulimwengu wa aliyekuumba unafanyaje fanyaje kazi, ndio ufurahie yaliyomo). Usiridhike ,una mengi ya kufahamu na ukawa na 'a competitive advantage' , unapokuwa popote (kijamii, kikazi na kibiashara )
- Utakuwa na amani ,ambayo haiondoki hata wakati wa shida.
- Utaanza kulala kama vile haudaiwi choochote (na nuru itakuja usoni, ukionekana watu wanajua umeshajipata).
- Vile vitu (tabia/mazoea) ulikuwa unaona hautaweza kuviacha , vinaondoka VYENYEWE, unakuwa bora zaidi ya wa hapo awali. NA,
- Utaona mambo yajayo kabla hayajatokea (maono, ndoto au sauti yenye kukupa taarifa nini ufanye), hautakuwa GIZANI tena!